Maswali fikirishi Juu ya Tozo za Majengo kupitia mfumo wa kununua Luku

Kaudunde Kautwange

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
1,600
1,567
Kuanzia leo Agosti 20, 2021 rasmi serikali imetangaza kuanza kukusanya kodi ya majengo kupitia ununuzi wa umeme kwa njia ya Luku.

Ni wazo jema lakini limegubikwa na utata, ni wakati sasa wa serikali kujitokeza hadharani na kutolea ufanunuzi na kujibu hoja hizi hapa chini:

1. Tozo ya majengo imepanda toka elfu 10 hadi elfu 12 kwa Mwaka, ambapo mnunuzi atakatwa elfu 1 kila mwezi,

Swali:
Kuna Jengo la kupangisha, lina namba moja ( Namba ya Jengo) lakini mwenye Jengo ameamua kila mpangaji kumuwekea Luku yake, hivyo kila mpangaji atakapo nunua Luku, atakatwa elfu 1, Je hii sio double tax kwa Jengo moja!? Vivyo hivyo kwenye frame za maduka!

2. Kwa nyumba za Ghorofa, kila sakafu itawajibikia kulipia elfu 60 toka elfu 50 ya awali kwa Mwaka,

Swali:
Ziko ghorofa zenye zaidi ya apartment moja kwenye sakafu, na kila appartment ina Luku yake, na kwa manunuzi ya umeme, elfu 5 itakuwa inakatwa, Je hii pia sio double tax kwa sakafu moja!?

3. Kwa mfumo huu, Je wale ambao Nyumba zao hazina umeme, maana yake automatically watakuwa hawalipi hii tozo!??

4. Kuna wastaafu baadhi ambao wamepewa msamaha wa tozo hizi za Majengo, je kwa Mfumo huu, ni dhahiri kuwa msamaha umeyeyuka automatically!??

Nikipata majibu, nitafurahi sana:

Cc: TANESCO
Cc: TRA
 
Hongera kwa Watanzania wote kwa mafanikio ya kuchangia tozo ya Sh. Bilioni 48.
Hakika maendeleo hayana chama, tuijenge nchi yetu.
Chonde chonde tunawataka viongozi wetu wawe waadilifu na waaminifu ktk Fedha hizi za umma.
 
Kumbe nchi yetu inaweza kutoboa kwa hii tozo, kama mwezi mmoja tu na nusu tumechangia Billioni 48 sasa je tukienda mwaka mmoja si nchi yetu itapiga hatua kubwa sana ktk maendeleo!
Hongera kwa Watanzania wote kwa Uzalendo wa kweli.
Sasa tunawaomba viongozi wetu wazisimamie pesa hizi kwa umakini, isiliwe hata sh 1 au kutumiwa vibaya.
 
Back
Top Bottom