Hawa Ghasia kwa hadhi gani aliyonayo ya kumwambia Mzee wetu Warioba afunge mdomo? Yeye asubiri 2015 inakuja arudi kuwa bibi shamba ,maana shemeji hatakuwepo tena Magogoni.Wewe ndo unajiita unafikiri?? kwani hayo maswali si aliyajenga katika kujibu hoja? aliyaulizia wapi hayo maswali? chooni? ni kwamba hana majibu ya hoja na maswali yanayoulizwa kuhusu rasimu ya tume yake. Hawa Ghasia ana haki ya kumuambia afunge mdomo wake kwa kuwa anachokifanya ni kupigia debe serikali 3 badala ya kujibu hoja za msingi. Kwa hiyo wewe umemuona Hawa Ghasia kakosea kwa kumuambia Jaji Warioba afunge mdomo wake kisa ni former PM? na sio Tundu Lissu aliyemuambia Mwl Nyerere muasisi wa taifa letu kuwa alikuwa akiishi kwa uwongo na kuwalaghai watanzania?
Moja ya kosa ililofanya tume ni kuacha mapendekezo mengine muhimu katika Rasimu hii, mfano mmoja mpaka sasa kuna serikali 2 sasa kwanini nayo isiingizwe ili wajumbe wachambue mapungufu yake na mazuri yake wananchi tupambanue, huwezi kungo,oa mfumo uliopo kwa Rasimu tuu bila ya kuwepo majadiliano, huo ni uhunu mkubwa kbs ambao tume imefanya na ndio nasema chanzo cha mgogoro huo ni tume. Sasa kwa kuwa jambo laenyewe limeenda kwa wadau wenyewe unategemea litapita kimya kimya? Haiwezekani.
Warioba amevurugwa kwa kiasi kikubwa sana anashindwa afanye lipi kwenye maisha yake alivyodanganya alijua kuwa kazi imeisha kumbe alikuwa anajaribu kina cha maji kwa miguu yote miwili.
Tume ya jaji warioba upande wa mfumo wa muungano wamekosea mh mbunge, alafu si wananchi wote walopropose serikali 3,
Hiyo kitu italigawa taifa in the longrun it is obvious.
Ondoa hoja uchwara hapa, watu ujibu hoja kwa hoja na si tabo na taarabu. Kwanza nani alikwambia Warioba ndiye aliyeandika Rasimu ya Katiba. Hii Rasimu imeandikwa na watu wanaoheshimika, mbona hamtaji Jaji Mkuu mstaafu Agustino Ramadhan ambaye alikuwa makamu Mwenyekiti, ni mtu mashauru sana hapa nchini, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi huru za Afrika hivi sasa Umoja Afrika AU Dk. Salim Ahmed Salim si mtu wa kubeza mataifa yanamheshimu sana, wako waadhili wa sheria, mhadhiri wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Paramagamba Kabudi na marehemu Dk. Sengodo Mvungi si watu wa kuokoteza. Kwa hiyo unapokuwa unabeza husiangalia kwa kukaririshwa na kuwa kasuku. Hapa ulipo sidhani hata siku moja utawahi kuwafikia watu hawa kwa sifa hata upande mlima Kilimanjaro
Huwa najiuliza ulinzi anaoutegemea Warioba ni wa Mungu ama ni wa hao hao anao pambana nao???
Au kuna nini kinachoendelea??? Maana dunia ya sasa kuondoana maisha ni sekunde tu.
Mkuu, wanamsubiri mwenyekiti aokoteze majibu toka kwa 'intellectually dishonest' ndipo wacopy n paste.Nishawahi 'kusikia'-ukiwapa SMZ wawe na serikali yao, Tz bara itakosa mapato mengi ya wahisani, zenji itakuwa tishio kijeshi, na itatumia effective rasilimali zao za baharini, mafuta na gesi.
Hii kitu Kikwete and his team hawataruhusu kamwe wajitenge. Lakini ukweli ni kwamba unapokuwa na nchi mbili huru...huwezi kukwepa serikali tatu.
Na hayo maswali ya Jaji Warioba hakuna mwana CCM atayeweza kuyajibu pale Bungeni miaka 100. Mchakato ulikuwa wa wazi, ni wapi Sinde kaingiza wazo lake la serikali 3 ?
Halafu hao wabunge wa CCM mbona kama siwaelewi, ni kweli Rasimu inataka Muungaano uvunjwe? manake ndo wanachoshupalia. Serikali 3 haivunji Muungano bali inaboresha tu. Ujio wa Yesu si kutengua torati ni kuiboresha.
Tanganyika haikwepeki katu.
Kwa taarifa yako Rasimu hii kwa sura ya kwanza na sita haitaji hata phd ya kuichambua inajionesha wazi mapungufu yake, Kwanza kwa takwimu za maoni hazijakidhi uwakilishi, pia muundo wenyewe na mambo ya msingi kuhusu Manufaa na hasara za kuwa na serikali tatu, kama katiba pia kuna hofu ambayo hata tume imekili juu Ya uhai wa serikali yenyewe sasa kwa nn msikubaliane na maoni ya wanaotaka serikali mbili? Ni ubishi ambao hauna maana yeyote na kutaka kuwabebesha mzigo watanzania kwa manufaa ya kisiasa, ni dhahili kbs msingi wa hoja ya serikali tatu ni hitaji la kisiasa, na tunaposema ki siasa nina maanisha kuwa kuna kundi linataka kutawala au kuwa sehemu ya utawala kwa kupitia katiba lakini cyo kwa manufaa ya wananchi ambao ndio wadau wa hiyo serikali yenyewe.. kuna hoja ya tume kuwa haya ni maoni ya wananchi , tujiulize ni mwananchi gani wa kawaida ambaye ana kero za maji, afya, elimu ,ajira ,malipo ya uzeeni , mishahara kwa watumishi kama wa elimu na kadhalika akaona Jibu la kuwa na serikali ya tatu atapata ufumbuzi?,, hii c kweli kbs, wakati wa mchakato tulimbiwa tupunguze madaraka ya Rais,halafu leo wajumbe wengine wanasema kuwa Rais wa jamhuri amepokonywa madaraka, na wakati huo huo tunaongeza serikali ingine,, jambo lingine tume inasema serikali washirika zitasimamia mambo yao ya maendeleo huku serikali.za mitaa ambazo ndizo karibu na wananchi mnaziondoa hii imekaaje? Ki uhalisia tunahitaji mjadala mpaka juu ya Huu muundo na mm naona kuna haja ya kurudi kwa wanachi juu ya hii sura ya kwanza na sita na cyo kuwaa hia wajumbe wa bunge maalumu sababu wengine wanakichukulia ki siasa zaidi.
Warioba amezeeka,tena mbaya zaidi amezeeka ubongo! tofauti na Hayati Baba wa Taifa Julius K.Nyerere ambaye inasemekana kadri alivyokuwa anazeeka ndivyo akili yake ilivyokuwa inakuwa kali kama ''WEMBE"! Kama kweli maswali hayo yametoka kwa WARIOBA basi naomba apumzike! Ni maswali ya KITOTO kabisa! Swali lake la kwanza, katiba hiyo haijatokana na Wananchi wa Tanzania! Tunakubali ni wananchi kwa maana ya Warioba na wajumbe wake wa Tume basi! Yako wapi maoni ya Mabaraza ambayo ndiyo yalikuwa uwe msingi wa rasimu ya pili! WARIOBA JIBU HILO KWANZA!
Jibu ni NDIO.
Takwimu za tume ya Warioba zina makosa, tena makosa makubwa ambayo yanafanya kila hitimisho lililoegemea takwimu hizo kuwa na makosa. Tena mbaya zaidi ni kwamba makosa yao si ya kibahati mbaya ya kiubinadam, isipokuwa ni ya makusudi na yaliyopangwa ili tu yaakisi utashi wao binafsi kwa kutumia mwamvuli wa utashi wa wananchi. Huku ni kuwahadaa watanzania na kuwafanya ni mbumbumbu kwa kugeuza maoni yao binafsi kuwa ni ya wananchi kama wanavyotaka kutuaminisha.
Na hata kama takwimu zao zingekuwa ni sahihi, lakini bado hitimisho lao la serikali 3 halikubaliani na takwimu zao wao wenyewe japo ni za nadharia tu na si uhalisia.
Huyo Jaji Warioba ni miongoni mwa watu waliokuwa washauri wa Baba wa Taifa enzi za utawala wake, sasa inakuwaje watoto waliozaliwa miaka ya hivi karibuni waruhusiwe kusimama Bungeni na kumshambulia kuwa hana nia nzuri na taifa, ingekuwa hivyo si angeanza enzi hizo ? Ikumbukwe kuwa sio mfano mzuri mtu mzima kama yule kusemwa vibaya kiasi hicho, inatoa mafundisho mabaya kwa kizazi kijacho kwa maana kuwa hakitakuwa na heshima kwa watu wazima.
Umesema vema kuwa hawa ni watu wenye taaluma, weledi na heshima zao. Lakini tusiwe watumwa wa fikra kwa kujaji mtu kwa weledi na sifa zake, kumbuka hapa hatujaji mtu isipokuwa kazi yao, hivyo tutaijaji rasimu kwa maudhui na mantiki yake badala ya kumuangalia mtu usoni. Tuanze hoja kama ifuatavyo;.....
Kumbuka rasimu ya kwanza ilibeba maoni ya wananchi waliyoyatoa kwenye mikutano ya tume.
Rasimu ya pili ilitakiwa ibebe maoni ya wananchi kwenye mabaraza ya katiba. Lakini cha kushangaza, kwa makusudi kabisa tume iliyarudia maoni yaleyale ya wananchi kwenye mikutano yake kutengeneza rasimu ya pili na maoni ya mabaraza ya katiba yakawekwa kando.
Kumbuka maoni ya wananchi kwenye mikutano ya tume haikuwa na utaratibu maalum kiuwiano katika uwakilishi na pia mikutano hiyo ya tume haikuweza kufanyika katika maeneo yote ya Tanzania, ndio maana hata matokeo yake yanatiliwa shaka kitakwimu.
Maoni ya mabaraza ya katiba yalikuwa na utaratibu maalum kiuwiano katika uwakilishi na pia yalifanyika katika wilaya zote za Tanzania, hivyo basi maoni haya ndiyo yangetoa matokeo sahihi yanayoakisi utashi wa wananchi.
Kuna swali muhimu sana ambalo Jaji Warioba na wenzake wameshindwa kulijibu, sitokaa katu kuiamini rasimu ya tume kuwa ni maoni ya wananchi mpaka wajibu swali lifuatalo;
SWALI: "Kwanini tume haikuyaingiza wala kuzingatia maoni ya mabaraza ya katiba katika rasimu ya pili? hali ya kuwa ndiyo maoni pekee ambayo yamezingatia kwa usahihi uwiano wa uwakilishi kwa Tanzania nzima, na badala yake wametumia maoni yaleyale yaliyotumika kutengeneza rasimu ya kwanza ambayo yametokana na mikutano ya tume"
Maoni mengi ya mabaraza ya katiba yamependekeza serikali 2, kutoingizwa kwake kwenye rasimu inaniaminisha kuwa tume ilikuwa inachagua kipi cha kuingiza na kipi cha kuacha ili kuakisi utashi wao binafsi.
Kilichofanywa na tume ni kiini macho kwa kutuaminisha kuwa rasimu ya katiba imetokana na wananchi hali ya kuwa ni maoni yao binafsi.
" Katika kero ambazo wamekuwa wanatueleza wanajeshi ni kupiga mizinga 21 kwa amiri jeshi huko dar.....na amiri jeshi mwingine huko Zanzibar.....amiri jeshi kwa kawaida huwa mmoja ...mjitahidi kuwaondolea wanajeshi kero hii" - Warioba