Maswali 7 ya Jaji Joseph Sinde Warioba

Maswali 7 ya Jaji Joseph Sinde Warioba

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ameuliza maswali saba ya msingi kwa wajumbe wa Bunge la Katiba wanaopinga Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume yake akitaka wawajibu wananchi ili kutuliza kiu yao.
Jaji Warioba ambaye tangu awasilishe Rasimu ya Katiba Desemba 30, mwaka jana amegeuka kuwa adui kwa watu wanaotaka muundo wa serikali mbili, aliuliza maswali hayo jana katika uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa Taasisi ya Twaweza kuhusu mchakato wa Katiba.

Akizungumza kwa ukali, Jaji Warioba alisema: "Kwanza, jibuni kwa nini mnapinga muundo wa Muungano wakati walioupendekeza ni wananchi?

"Sheria inasema uwepo wa Muungano na mapendekezo katika rasimu hayasemi Muungano usiwepo. Kumbukeni kuwa wananchi walitakiwa kutoa mapendekezo ya namna ya kuboresha Muungano."
Katika swali lake la pili, Warioba alisema kwa nini Tanganyika imevaa koti la Muungano? Kwa kuwa katika ukusanyaji wa maoni wananchi walieleza kuwa Serikali ya Muungano ya sasa siyo ya Muungano, ni ya Tanganyika.
Katika swali la tatu alisema wajumbe hao wanatakiwa kujibu maelezo ya wananchi ambao waliieleza tume hiyo kuwa Katiba imevunjwa na madaraka ya rais yamechukuliwa na sasa kuna marais wawili katika nchi moja.
"Tume inapewa lawama kubwa, wajibuni wananchi hii tume ilitumwa na nani kukusanya maoni ya wananchi? Waambieni ilikusanya maoni hayo kwa kutumia sheria ipi zaidi ya ile ya Mabadiliko ya Katiba?" alisema Jaji Warioba katika swali lake la nne.
Katika swali lake la tano, Warioba aliwataka wajumbe hao kutoa sababu za kumtuhumu kuwa amependekeza muundo wa serikali tatu kwa sababu yeye pamoja na (Joseph Butiku) walikuwa wajumbe wa Tume ya Jaji Kisanga na Jaji Nyalali ambazo nazo zilipendekeza muundo wa serikali tatu, kitu ambacho alisema si kweli na hawakuwahi kuwa mjumbe wa tume hizo.
Pia, aliwataka wajumbe hao kujibu swali la sita, kwa nini hawataki kuzungumzia yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na badala yake wanageuza rasimu hiyo kuwa imeandikwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Katika swali lake la saba, aliwataka wajumbe kujibu kwa nini wanaishutumu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa imeingiza maoni yake, wakati ilikusanya maoni hayo kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba?
Alisema badala ya kujadili hoja za msingi, wajumbe wa Bunge hilo wamekuwa wakitoa lugha za kejeli na matusi kwa baadhi ya watu (akiwamo na yeye), kitendo ambacho alisema si sahihi na kinaweza kuligawa taifa kwa sababu yaliyomo katika Rasimu ya Katiba yametokana na maoni ya wananchi.
Katika uzinduzi huo walikuwepo baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo ambao ni Dk Hamisi Kigwangalla aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Julius Mtatiro, Maria Sarungi na aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole
 
Sasa Mr. Dr. inakuwaje unashindwa kuandika vizuri? Utaunganishaje jina la mtu na neno lingine? nimeshindwa kusoma kwakweli.

usijifanye hujui kusoma mwenzio kaandika kiswahili na ndio lugha yako. maandishi huyaelewi na picha nayo huitambui??? acha umburula wee bwe..ge
 
Tume ya jaji warioba upande wa mfumo wa muungano wamekosea mh mbunge, alafu si wananchi wote walopropose serikali 3,
Hiyo kitu italigawa taifa in the longrun it is obvious.

Me nina shindwa kuwaelewa kwani visiwani wakigoma kuungana na sisi tutawalazimisha?
Na je ni lazima kuungana ?
Kwanini tusiungane na burundi au kenya kwa mfumo huo wa zanzibar coz nirahisi zaidi amana maji ya kuvuka ata kwa miguu tu mtu unaingia kenya na kutoka kwanini zanzibar ?
 
Tume ya jaji warioba upande wa mfumo wa muungano wamekosea mh mbunge, alafu si wananchi wote walopropose serikali 3,
Hiyo kitu italigawa taifa in the longrun it is obvious.

Hata iliyopo hakupEndekezwa na wato wote na ukweli ni kuwa hata hii ilishaligawa Taifa.
 
Warioba ni kichwa muhimu baada ya baba wa Taifa kuondoka. Ataendelea kupuzwa na ccm mpaka atakapomfuata mjomba wake. Watakaosifiwa na ccm ni yale madodoki tu ambayo hayajui kuchuja, porojo zao ndo heshima yao lakini mafisadi waliokubuhu. Wanajua mkate wa wizi utadhurika endapo rasimu hii ya 2 itapita na kuwa katiba. Wanajua kwamba wananchi wanaogopa vichapo vya jeshi na kwa hiyo wanaitumia kama fimbo ya kupitishia uharamia wao. Bado nashangaa mpaka sasa, Mwamunyange na au msemaji wa Jeshi kwa nini wanaogopa kukanusha machafuzi ya bosi wao? Ni jeshi la wananchi na sio la JK wasiogope wataungwa mkono na wenye jeshi ambao ni wananchi wenyewe. Mkorofi na mhalifu ndiye anayeogopa jeshi siku zote, mtu safi na makini ni rafiki wa jeshi daima kwa sababu jeshi lipo kwa ajili ya kumhakikishia usalama.

Hakika umenena vyema kiongozi. Hawa ndio ccm itakayowakumbuka kwa ufanisi wao lukuvi wassira komba kigwangalah mwingulu serkukamba nkamia.
 
Majibu yote aliyouliza Warioba anayo majibu yake. Yeye alipaswa kuungama na kuwaomba radhi Watanzania kwa jaribio lake la uhaini
 
Warioba amejidhalilisha kweli. Ni bora akatafuta pa kujificha kuliko anavyoendelea kuongea kwenye media. Vinginevyo watanzania wataamini kuwa serikali tatu ulikuwa ni mpango wake na si mawazo ya wananchi
 
majibu hawana.wamebakia kuongelea mtu-warioba na sio issues-rasimu.
 
Huwa najiuliza ulinzi anaoutegemea Warioba ni wa Mungu ama ni wa hao hao anao pambana nao???

Au kuna nini kinachoendelea??? Maana dunia ya sasa kuondoana maisha ni sekunde tu.

Ulinzi mkubwa kuliko wote ni wa MUNGU na ndio warioba anautegemea. MUNGU asipokulinda hata ukatumia wanajeshi wote tanzania na duniani kukulinda ni bure.
 
warioba.jpg

Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ameuliza maswali saba ya msingi kwa wajumbe wa Bunge la Katiba wanaopinga Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume yake akitaka wawajibu wananchi ili kutuliza kiu yao.

Jaji Warioba ambaye tangu awasilishe Rasimu ya Katiba Desemba 30, mwaka jana amegeuka kuwa adui kwa watu wanaotaka muundo wa serikali mbili, aliuliza maswali hayo jana katika uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa Taasisi ya Twaweza kuhusu mchakato wa Katiba.

Akizungumza kwa ukali, Jaji Warioba alisema: "Kwanza, jibuni kwa nini mnapinga muundo wa Muungano wakati walioupendekeza ni wananchi?

"Sheria inasema uwepo wa Muungano na mapendekezo katika rasimu hayasemi Muungano usiwepo. Kumbukeni kuwa wananchi walitakiwa kutoa mapendekezo ya namna ya kuboresha Muungano."

Katika swali lake la pili, Warioba alisema kwa nini Tanganyika imevaa koti la Muungano? Kwa kuwa katika ukusanyaji wa maoni wananchi walieleza kuwa Serikali ya Muungano ya sasa siyo ya Muungano, ni ya Tanganyika.

Katika swali la tatu alisema wajumbe hao wanatakiwa kujibu maelezo ya wananchi ambao waliieleza tume hiyo kuwa Katiba imevunjwa na madaraka ya rais yamechukuliwa na sasa kuna marais wawili katika nchi moja.

"Tume inapewa lawama kubwa, wajibuni wananchi hii tume ilitumwa na nani kukusanya maoni ya wananchi? Waambieni ilikusanya maoni hayo kwa kutumia sheria ipi zaidi ya ile ya Mabadiliko ya Katiba?" alisema Jaji Warioba katika swali lake la nne.

Katika swali lake la tano, Warioba aliwataka wajumbe hao kutoa sababu za kumtuhumu kuwa amependekeza muundo wa serikali tatu kwa sababu yeye pamoja na (Joseph Butiku) walikuwa wajumbe wa Tume ya Jaji Kisanga na Jaji Nyalali ambazo nazo zilipendekeza muundo wa serikali tatu, kitu ambacho alisema si kweli na hawakuwahi kuwa mjumbe wa tume hizo.

Pia, aliwataka wajumbe hao kujibu swali la sita, kwa nini hawataki kuzungumzia yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na badala yake wanageuza rasimu hiyo kuwa imeandikwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Katika swali lake la saba, aliwataka wajumbe kujibu kwa nini wanaishutumu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa imeingiza maoni yake, wakati ilikusanya maoni hayo kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba?

Alisema badala ya kujadili hoja za msingi, wajumbe wa Bunge hilo wamekuwa wakitoa lugha za kejeli na matusi kwa baadhi ya watu (akiwamo na yeye), kitendo ambacho alisema si sahihi na kinaweza kuligawa taifa kwa sababu yaliyomo katika Rasimu ya Katiba yametokana na maoni ya wananchi.

Katika uzinduzi huo walikuwepo baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo ambao ni Dk Hamisi Kigwangalla aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Julius Mtatiro, Maria Sarungi na aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole.

Amshukia Lukuvi

Katika maelezo yake, Jaji Warioba alieleza kushangazwa kwake na wajumbe kulitumia Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kama mfano wa kuwashawishi Watanzania kukubaliana na matakwa yao ya kutaka kupinga mfumo wa serikali tatu.

"Nchi hii imekuwa na matatizo ya rushwa na ufisadi, lakini hakuna hata siku moja mtu amesema jeshi linaweza kushika madaraka. Leo kwa sababu ya madaraka mnaingiza jeshi na mchakato wa Katiba katika makundi."

Licha ya kutomtaja mlengwa, kauli hiyo ilionekana kumlenga Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge), William Lukuvi ambaye Aprili 13, mwaka huu aliwataka wananchi kupinga muundo wa serikali tatu, akisema la sivyo jeshi linaweza kuchukua madaraka.

Akiwa katika Kanisa la Methodist, Jimbo la Dodoma alipokuwa mgeni rasmi akimwakilisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Lukuvi alisema muundo huo ukipita, nchi itatawaliwa na jeshi kwa kuwa Serikali ya Muungano itashindwa kuwalipa mishahara wanajeshi.

Kauli kama hiyo pia iliwahi kutolewa na Rais Jakaya Kikwete wakati akizindua Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma.

"Msiliingize jeshi katika siasa za makundi na inakuwa mbaya zaidi kama mkienda katika makanisa na kutoa kauli za namna hii," alisema Warioba na kuongeza:

"Umoja wetu, amani na utulivu kwa kiwango kikubwa mhimili wake ni viongozi wa dini. Wamekuwa wakihubiri umoja, amani na mshikamano, hivyo tusiingize siasa za makundi kwenye makanisa na misikiti."

Jaji Warioba aliwataka wajumbe wa Bunge hilo kukumbuka wajibu wao wa kuwaunganisha wananchi na kuwataka waachane na kauli za kejeli, kuudhi na matusi kwani zinaweza kuleta mgawanyiko na mpasuko nchini.

"Nimekuwa mtumishi wa umma kwa muda mrefu lakini sijawahi kuona taasisi yenye uzalendo wa hali ya juu kama JWTZ," alisema Warioba.

Warioba ambaye amewahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania, kuanzia mwaka 1985 hadi 1990, alisema: "Katika ziara zangu mikoani nilikuwa nikikutana na wanajeshi na kunieleza matatizo yao. Licha ya wakati huo serikali za mataifa mengine zilikuwa zikipinduliwa na jeshi, hapa kwetu ilikuwa tofauti, walikuwa na uzalendo wa hali ya juu licha ya kuwa hali yetu kiuchumi ilikuwa mbaya," alisema.

Alisema wakati huo wanajeshi walikuwa wakivaa sare zilizochakaa na viatu vilivyopasuka, lakini hawakufikiria kuipindua Serikali.

Alisema hata katika vita dhidi ya Uganda, wanajeshi wa Tanzania walishinda kwa sababu ya uzalendo na siyo vifaa vya kisasa vya kivita... "Inashangaza kuona watu wanatolea mfano mmoja tu wa kama wanajeshi wasipolipwa; kwa nini wasiseme mawaziri au watumishi wa serikali wasipolipwa?"

Alisema kauli hiyo ni sawa na kuwaeleza wananchi kuwa jeshi ni baya na kama ikipita Katiba isiyoendana na matakwa ya walio wengi jeshi litachukua nchi.

Alisema wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba ikikusanya maoni ya wananchi, wanajeshi na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini walijikita zaidi kutoa maoni ya kuimarishwa kwa ulinzi na usalama na siyo mambo mengine.

"Tatizo ambalo walitueleza ni kuchoshwa na kitendo cha kupiga mizinga 21 kwa Amri Jeshi Mkuu wakiwa Dar es Salaam na wakiwa Zanzibar. Walisema kwa nidhamu ya jeshi, Amri Jeshi Mkuu ni mmoja tu. Nadhani mngewaondolea kero hiyo na si mambo mengine," alisisitiza.

Kigwangalla

Kwa upande wake, Dk Kigwangalla alisema kama tatizo ni Muungano ni vyema suala hilo likarejeshwa upya kwa wananchi ili watoe maoni yao kwa sababu mchakato huo sasa umehamia katika muundo wa Muungano pekee.

"Mchakato huu si wa kuifufua Tanganyika na kuvunja mkataba wa Muungano na siyo wa kubadili muundo wa utawala. Mambo haya yalihitaji mchakato unaojitegemea," alisema.

Alisema tume zote zilizotoa mapendekezo ya Serikali tatu zilikuwa na asilimia ndogo ya watu waliounga mkono kama ilivyo kwa Tume ya Jaji Warioba.

Chanzo:Mwananchi
 
Warioba amejidhalilisha
kweli. Ni bora akatafuta pa kujificha kuliko anavyoendelea kuongea
kwenye media. Vinginevyo watanzania wataamini kuwa serikali tatu ulikuwa
ni mpango wake na si mawazo ya wananchi
Mkimaliza huo u simba na yanga mtamkumbuka Warioba na tume yake. Swali? Umewahi kuiona serikali inayojipinga yenyewe? HII NI MARA YA KWANZA KWA BUNGE KUPINGA TUME YAKE TENA YA RAIS..AJABU! Kidogo nikubaliane na Mtikila kuwa hii ni laana ya Taifa kumkataa Mungu.
 
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ameuliza maswali saba yamsingi kwa wajumbe wa Bunge la Katiba wanaopinga Rasimu ya Katiba iliyotolewa naTume yake akitaka wawajibu wananchi ili kutuliza kiu yao.
Jaji Wariobaa mbaye tangu awasilishe Rasimu ya Katiba Desemba 30, mwaka jana amegeuka kuwa adui kwa watu wanaotaka muundo wa serikali mbili, aliuliza maswali hayo jana katika uzinduzi wa ripoti ya utafiti waTaasisi yaTwaweza kuhusu mchakato waKatiba.
Akizungumza kwaukali, Jaji Warioba alisema: “Kwanza, jibuni kwanini mnapinga muundo wa Muungano wakati walioupendekeza ni wananchi?
“Sheria inasema uwepo wa Muungano na mapendekezo katika rasimu hayasemi Muungano usiwepo. Kumbukeni kuwa wananchiwalitakiwakutoa mapendekezo ya namna yakuboresha Muungano.”
Katika swalilake la pili,Wariobaalisema kwa niniTanganyika imevaakoti la Muungano? Kwakuwa katika ukusanyaji wamaoni wananchiwalielezakuwa Serikaliya Muungano yasasasiyoyaMuungano, ni ya Tanganyika.
Katika swalila tatu alisema wajumbe hao wanatakiwakujibu maelezo yawananchi ambao waliielezatume hiyo kuwa Katiba imevunjwa namadarakayarais yamechukuliwa nasasakuna maraiswawili katika nchi moja.
“Tume inapewa lawamakubwa, wajibuni wananchihii tume ilitumwananani kukusanya maoni yawananchi?Waambieni ilikusanyamaoni hayo kwakutumia sheria ipi zaidiyaile yaMabadiliko yaKatiba?” alisema JajiWariobakatika swalilake la nne.
Katika swalilake la tano, Wariobaaliwataka wajumbe hao kutoa sababuza kumtuhumu kuwa amependekeza muundo waserikalitatu kwasababuyeye pamoja na(Joseph Butiku) walikuwa wajumbe waTume yaJajiKisanga naJajiNyalaliambazo nazo zilipendekeza muundo waserikalitatu, kitu ambacho alisema si kwelinahawakuwahikuwa mjumbe watume hizo.
Pia, aliwatakawajumbe hao kujibu swalila sita, kwaninihawatakikuzungumzia yaliyomo katika Rasimu yaKatibanabadalayake wanageuzarasimu hiyo kuwa imeandikwana Tume yaMabadiliko yaKatiba.
Katika swalilake la saba, aliwatakawajumbe kujibu kwaniniwanaishutumu Tume ya Mabadiliko yaKatibakuwa imeingiza maoni yake, wakatiilikusanyamaoni hayo kwa mujibu waSheria yaMabadiliko yaKatiba?
Alisemabadalayakujadilihoja za msingi, wajumbe waBunge hilo wamekuwa wakitoa lugha za kejeli namatusi kwabaadhiyawatu (akiwamo nayeye), kitendo ambacho alisema si sahihinakinaweza kuligawa taifakwa sababuyaliyomokatika Rasimu yaKatiba yametokana namaoni yawananchi.
Katika uzinduzi huo walikuwepo baadhiya wajumbe waBunge hilo ambao ni Dk Hamisi KigwangallaaliyemwakilishaKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, JuliusMtatiro, MariaSarunginaaliyekuwamjumbe waTume yaMabadiliko yaKatiba, Humphrey Polepole.

Du...huu uandishi huu!

Kweli wewe ni daktari (I mean medical doctor)....
 
Tume ya jaji warioba upande wa mfumo wa muungano wamekosea mh mbunge, alafu si wananchi wote walopropose serikali 3,
Hiyo kitu italigawa taifa in the longrun it is obvious.

Unaposema si wote kwani wote wana mawazo sawa? Au je wote wanaujua muungano? Je kuna kitu walichosema wote?
 
Warioba kama binadamu ni halali kujibu au kuwauliza maswali wajumbe hawa, lakini nahisi tofauti yake na wajumbe hawa ni kubwa sana. Uchambuzi wote unaosikika bungeni ni wa kuelekezwa kabisa. Waliowengi hawana uwezo wa kusoma document kubwa kama hii ya katiba. Siamini kabisa kwamba watu kama Nchemba, Hawa Ghasia, Sendeka, Komba, n.k. wana uwezo wa kusoma kwa makini na kuweza kukumbuka yaliyoandikwa na baadaye eti wachambue.

Hawa ni watu ambao hawana hata ufahamu wa Dunia inavyokwenda. Pale Bungeni mtu kama Sendeka kapangwa kukaa na mtu anayemsaidia kupanga ya kuzungumza, msaidizi mwenyewe naye ni hoi! Kwa ujumla hatuna wabunge na bunge lilihalibiwa na uteuzi. Aina ya wajumbe na ubora wao uko chini sana.

unachoweza kuona ni kwamba baadhi ya watu walio na uwezo mkubwa wanashindwa kuzungumza. Wengine tuliotegemea waonyeshe ufahamu mkubwa wameamua kujikomba na kujidai eti ni wasomi wazoefu, wanajua kuchambua takwimu, n.k. Lakini wako hoi na hata ukiwatafuta google hawajawahi kuhangaika na takwimu wengine kwa miaka 10 iliyopita. Mtafute Tibaijuka, mtafute yule wa UD anaitwa Francis, mtafute yule wa SU anaitwa Asei, mtafute Magembe, mtafute Msola, wote hawana kabisa zile basics za takwimu. Ni aibu kwamba hata wanaofundisha vyuo vikuu wamaekuwa ni chini ya mwanafunzi wa sekondari anayejua haki yake ya kupikiwa chakula kiive.

Kwa taarifa yako Rasimu hii kwa sura ya kwanza na sita haitaji hata phd ya kuichambua inajionesha wazi mapungufu yake, Kwanza kwa takwimu za maoni hazijakidhi uwakilishi, pia muundo wenyewe na mambo ya msingi kuhusu Manufaa na hasara za kuwa na serikali tatu, kama katiba pia kuna hofu ambayo hata tume imekili juu Ya uhai wa serikali yenyewe sasa kwa nn msikubaliane na maoni ya wanaotaka serikali mbili? Ni ubishi ambao hauna maana yeyote na kutaka kuwabebesha mzigo watanzania kwa manufaa ya kisiasa, ni dhahili kbs msingi wa hoja ya serikali tatu ni hitaji la kisiasa, na tunaposema ki siasa nina maanisha kuwa kuna kundi linataka kutawala au kuwa sehemu ya utawala kwa kupitia katiba lakini cyo kwa manufaa ya wananchi ambao ndio wadau wa hiyo serikali yenyewe.. kuna hoja ya tume kuwa haya ni maoni ya wananchi , tujiulize ni mwananchi gani wa kawaida ambaye ana kero za maji, afya, elimu ,ajira ,malipo ya uzeeni , mishahara kwa watumishi kama wa elimu na kadhalika akaona Jibu la kuwa na serikali ya tatu atapata ufumbuzi?,, hii c kweli kbs, wakati wa mchakato tulimbiwa tupunguze madaraka ya Rais,halafu leo wajumbe wengine wanasema kuwa Rais wa jamhuri amepokonywa madaraka, na wakati huo huo tunaongeza serikali ingine,, jambo lingine tume inasema serikali washirika zitasimamia mambo yao ya maendeleo huku serikali.za mitaa ambazo ndizo karibu na wananchi mnaziondoa hii imekaaje? Ki uhalisia tunahitaji mjadala mpaka juu ya Huu muundo na mm naona kuna haja ya kurudi kwa wanachi juu ya hii sura ya kwanza na sita na cyo kuwaa hia wajumbe wa bunge maalumu sababu wengine wanakichukulia ki siasa zaidi.
 
Usiite watu mbumbumbu mkuu, si ustaarabu.
Sijawai fanya takwimu,
Sijafuata maelekezo ya yeyote yule, nimewaza mwenyewe nikachanganya na wanosema ukawa na walio against ukawa nimeconclude serikali 3 italeta matatizo, nitapigia kura mbili,
Ni maoni tu

mbwiga mburulaaaaa................
 
Nawaza kwa sauti...
1. HIVI KUNA JAMBO LOLOTE LA MUUNGANO LINALOSHUGHURIKIWA NA SERIKALI ZA MAPINDUZI YA ZANZIBAR PEKEE..?

2. Kama mambo ya muungano yote yanashughurikiwa serikali moja, kuna muungano kweli hapo...?

3. Kwa nini katika muungano, Zanzibar idai mamlka kamili..?? Kuna muungano kweli hapo..??
 
" Katika kero ambazo wamekuwa wanatueleza wanajeshi ni kupiga mizinga 21 kwa amiri jeshi huko dar.....na amiri jeshi mwingine huko Zanzibar.....amiri jeshi kwa kawaida huwa mmoja ...mjitahidi kuwaondolea wanajeshi kero hii" - Warioba

ha ha ha! Huyu mzee kweli alifaa kuwa jaji mkuu.
 
Warioba kama binadamu ni halali kujibu au kuwauliza maswali wajumbe hawa, lakini nahisi tofauti yake na wajumbe hawa ni kubwa sana. Uchambuzi wote unaosikika bungeni ni wa kuelekezwa kabisa. Waliowengi hawana uwezo wa kusoma document kubwa kama hii ya katiba. Siamini kabisa kwamba watu kama Nchemba, Hawa Ghasia, Sendeka, Komba, n.k. wana uwezo wa kusoma kwa makini na kuweza kukumbuka yaliyoandikwa na baadaye eti wachambue.

Hawa ni watu ambao hawana hata ufahamu wa Dunia inavyokwenda. Pale Bungeni mtu kama Sendeka kapangwa kukaa na mtu anayemsaidia kupanga ya kuzungumza, msaidizi mwenyewe naye ni hoi! Kwa ujumla hatuna wabunge na bunge lilihalibiwa na uteuzi. Aina ya wajumbe na ubora wao uko chini sana.

unachoweza kuona ni kwamba baadhi ya watu walio na uwezo mkubwa wanashindwa kuzungumza. Wengine tuliotegemea waonyeshe ufahamu mkubwa wameamua kujikomba na kujidai eti ni wasomi wazoefu, wanajua kuchambua takwimu, n.k. Lakini wako hoi na hata ukiwatafuta google hawajawahi kuhangaika na takwimu wengine kwa miaka 10 iliyopita. Mtafute Tibaijuka, mtafute yule wa UD anaitwa Francis, mtafute yule wa SU anaitwa Asei, mtafute Magembe, mtafute Msola, wote hawana kabisa zile basics za takwimu. Ni aibu kwamba hata wanaofundisha vyuo vikuu wamaekuwa ni chini ya mwanafunzi wa sekondari anayejua haki yake ya kupikiwa chakula kiive.

Asante sana kwa hili jicho la 'nne', binafsi yangu naona hiki ndio kiini cha tatizo.....Ni afadhali bunge hili lingekuwa na watu hata 30 tu, wanojua wanafanya nini, labda tungepata katiba mpya recently...Lakini kwa waliopo, I doubt...
 
Back
Top Bottom