Maswali 7 ya Jaji Joseph Sinde Warioba

Maswali 7 ya Jaji Joseph Sinde Warioba

Warioba asipoangalia atazeeka mara mbili yeye akae (kimywa) dawa iweze kuingia alipotosha sana sasa moto unamwakia anajuta na mikono kichwani.

Angalia ulicho kiandika hapo juu nilipo kuwekea mabano.umbumbumbu ume kujaa.
 
Kwa taarifa yako Rasimu hii kwa sura ya kwanza na sita haitaji hata phd ya kuichambua inajionesha wazi mapungufu yake, Kwanza kwa takwimu za maoni hazijakidhi uwakilishi, pia muundo wenyewe na mambo ya msingi kuhusu Manufaa na hasara za kuwa na serikali tatu, kama katiba pia kuna hofu ambayo hata tume imekili juu Ya uhai wa serikali yenyewe sasa kwa nn msikubaliane na maoni ya wanaotaka serikali mbili? Ni ubishi ambao hauna maana yeyote na kutaka kuwabebesha mzigo watanzania kwa manufaa ya kisiasa, ni dhahili kbs msingi wa hoja ya serikali tatu ni hitaji la kisiasa, na tunaposema ki siasa nina maanisha kuwa kuna kundi linataka kutawala au kuwa sehemu ya utawala kwa kupitia katiba lakini cyo kwa manufaa ya wananchi ambao ndio wadau wa hiyo serikali yenyewe.. kuna hoja ya tume kuwa haya ni maoni ya wananchi , tujiulize ni mwananchi gani wa kawaida ambaye ana kero za maji, afya, elimu ,ajira ,malipo ya uzeeni , mishahara kwa watumishi kama wa elimu na kadhalika akaona Jibu la kuwa na serikali ya tatu atapata ufumbuzi?,, hii c kweli kbs, wakati wa mchakato tulimbiwa tupunguze madaraka ya Rais,halafu leo wajumbe wengine wanasema kuwa Rais wa jamhuri amepokonywa madaraka, na wakati huo huo tunaongeza serikali ingine,, jambo lingine tume inasema serikali washirika zitasimamia mambo yao ya maendeleo huku serikali.za mitaa ambazo ndizo karibu na wananchi mnaziondoa hii imekaaje? Ki uhalisia tunahitaji mjadala mpaka juu ya Huu muundo na mm naona kuna haja ya kurudi kwa wanachi juu ya hii sura ya kwanza na sita na cyo kuwaa hia wajumbe wa bunge maalumu sababu wengine wanakichukulia ki siasa zaidi.

Mkuu naomba tusaidie wengine 'tuliochanganywa' na majadiliano hayo ya mfumo, hivi kwa nini serikali mmoja haizungumziwi kama option? Manake tunavyosikia (nakiri sijaisoma) rasimu ina pendekezo la serikali 3, na kuna wajumbe wanadai ziwe 2 (ambayo hii haipo kwenye rasimu), au moja ni 'baba mkwe' kabisa?
 
Warioba amezeeka,tena mbaya zaidi amezeeka ubongo! tofauti na Hayati Baba wa Taifa Julius K.Nyerere ambaye inasemekana kadri alivyokuwa anazeeka ndivyo akili yake ilivyokuwa inakuwa kali kama ''WEMBE"! Kama kweli maswali hayo yametoka kwa WARIOBA basi naomba apumzike! Ni maswali ya KITOTO kabisa! Swali lake la kwanza, katiba hiyo haijatokana na Wananchi wa Tanzania! Tunakubali ni wananchi kwa maana ya Warioba na wajumbe wake wa Tume basi! Yako wapi maoni ya Mabaraza ambayo ndiyo yalikuwa uwe msingi wa rasimu ya pili! WARIOBA JIBU HILO KWANZA!
 
Warioba amevurugwa kwa kiasi kikubwa sana anashindwa afanye lipi kwenye maisha yake alivyodanganya alijua kuwa kazi imeisha kumbe alikuwa anajaribu kina cha maji kwa miguu yote miwili.

Unauhakika amedanganya?Je,kwa sasa kweli kuna muungano?Je,kiukweli hawa wajumbe toka Zanzibar wanasema ukweli au wanasema hayo kwa ajili ya kutafuta ulaji tu?Nafuu aliyesema ukweli maana umemwacha huru.

Nampongeza Judge Warioba na Team yake kwa kusema ukweli,na daima kumbuka ukweli unauma.Kilichotakiwa wala si kumtukana Judge Warioba bali kwenda ndani zaidi na kujua kwa nini Tume ilipaswa kusema waliyoyasema.Wangejaribu kutafiti zaidi kujua undani wa tatizo la Muungano na kuja na muafaka na marithiano na upande wa pili wa Zanzibar,kinachoendelea bungeni kwa sasa wala siyo kujadili Rasimu ya Katiba bali muendelezo wa uwongo na mbaya zaidi wanatumia matusi,kebehi na dharau kwa watu waliowatuma.

Haituingii akilini hata siye tunaosupport serikali mbili bali tunapata aibu tu maana malumbano ni ya watu na si kilichowapeleka.

Usitukane mtu aliyesema kweli na sote tunajua alichosema ni ukweli,tunachohitaji kutatua tatizo katika kweli.
 
" Katika kero ambazo wamekuwa wanatueleza wanajeshi ni kupiga mizinga 21 kwa amiri jeshi huko dar.....na amiri jeshi mwingine huko Zanzibar.....amiri jeshi kwa kawaida huwa mmoja ...mjitahidi kuwaondolea wanajeshi kero hii" - Warioba

Nikiangalia hili BMK na kusikiliza hoja za wengi napata na kichefuchefu. Nini wanakijadili pale.
 
Mkuu naomba tusaidie wengine 'tuliochanganywa' na majadiliano hayo ya mfumo, hivi kwa nini serikali mmoja haizungumziwi kama option? Manake tunavyosikia (nakiri sijaisoma) rasimu ina pendekezo la serikali 3, na kuna wajumbe wanadai ziwe 2 (ambayo hii haipo kwenye rasimu), au moja ni 'baba mkwe' kabisa?

Moja ya kosa ililofanya tume ni kuacha mapendekezo mengine muhimu katika Rasimu hii, mfano mmoja mpaka sasa kuna serikali 2 sasa kwanini nayo isiingizwe ili wajumbe wachambue mapungufu yake na mazuri yake wananchi tupambanue, huwezi kungo,oa mfumo uliopo kwa Rasimu tuu bila ya kuwepo majadiliano, huo ni uhunu mkubwa kbs ambao tume imefanya na ndio nasema chanzo cha mgogoro huo ni tume. Sasa kwa kuwa jambo laenyewe limeenda kwa wadau wenyewe unategemea litapita kimya kimya? Haiwezekani.
 
Huwa najiuliza ulinzi anaoutegemea Warioba ni wa Mungu ama ni wa hao hao anao pambana nao???

Au kuna nini kinachoendelea??? Maana dunia ya sasa kuondoana maisha ni sekunde tu.

Mkuu, kumbuka wote tutaonja mauti. Anayeua ataonja mauti pia. Jaji Warioba aendelee kutuelimisha. Watawala wetu wamekuwa walevi wa madaraka. Wanatengeneza mazingira ya kurisishana utawala. Mwenye akili haitaji kuambiwa.
Ili mbegu iote lazima ifukiwa ardhini.
 
Warioba ninge mwelewa kama ange toa hoja za msingi zaidi ya hizo mfano! Wajumbe wengi kila wanapo simama kuchangia utawasikia wana sema takwim zilizo pelekea kupatikana kwa rasim hiyo si sahihi, wengine si za kweli, wengine hazina mashiko na nk!

Kwa mtazamo huo kuna kiwango flani cha kitakwimu wajumbe wanadhani hicho kinge fikiwa basi maoni hayo yangekuwa valid! Sasa kwanini wanaendelea kijadili kitu ambacho hakina takwimu sahihi? Basi wavunje bunge watengeneze sample size inayo takiwa waipe tume nyingine irudi tena kwa wananchi ikusanye maoni kwa kiwango wanacho taka then wajadili upya!

Lakini pia hivi wao rasimu iliyo pendekeza serikali mbili wameitoa wapi? wanasema wanachi wanataka serikali mbili hiyo research waliifanya wapi saa ngapi na kwa nani na waka andika wapi ripoti yao kwa ajiri ya reference?

Lakini pia swali lingine la kujiuliza kama tume ya warioba iliyopewa kazi ya kukusanya maoni kisheria imefanya kazi mbovu kama wanavyo sema hawaoni ni tusi kwa aliye wateua pia? Kwamba hakuwa makini katika uteuzi wake kwa kuteua watu mizigo ambao wametumia gharama kubwa na kuleta kitu kisicho faaa?

Kwa mtazamo huu najenga picha kuwa kumbe hakukua na haja ya kuunda tume kwa kua wajumbe walio teuliwa walikuwa na maoni kabisa ya wanachi kwa nini wasinge enda tu moja kwa moja bungeni na kuyatoa huko wakatengeneza na rasimu yao waka ipitisha moja kwa moja?

Tusichezeane akili na hivi vyama vya siasa! Ifike mahala watu tuwe wakweli kama mnania ya kufanya kitu kifanyike sio kupindisha pindisha mambo mgekuwa wote mnataka umoja wakitaifa ninge waelewa kama mnataka serikali 1, mkawashawishi na wanachi lakini kwa kuwa kila chama kimeweka maslahi yake mbele ndio maana kila mtu anataka muundo wa serikali utako vutia maslahi yake!

Tanzania ya serikali moja kwanza!
 
Moja ya kosa ililofanya tume ni kuacha mapendekezo mengine muhimu katika Rasimu hii, mfano mmoja mpaka sasa kuna serikali 2 sasa kwanini nayo isiingizwe ili wajumbe wachambue mapungufu yake na mazuri yake wananchi tupambanue, huwezi kungo,oa mfumo uliopo kwa Rasimu tuu bila ya kuwepo majadiliano, huo ni uhunu mkubwa kbs ambao tume imefanya na ndio nasema chanzo cha mgogoro huo ni tume. Sasa kwa kuwa jambo laenyewe limeenda kwa wadau wenyewe unategemea litapita kimya kimya? Haiwezekani.

Kama ni hivyo, huoni kama hiyo rasimu isingepatikana kwa wakati huu kwa kutaka maoni yote, bila kuzingatia statistics, yaingizwe kwenye rasimu? Bado ingekuwa ni rasimu au mapendekezo/maoni ya walioulizwa? Kama ndivyo, ina maana tumeruka hatua moja ambayo maoni yote ndio yangeletwa kwenye mkusanyiko huu (badala ya tume) ili wachambue nini kiunde rasimu? Na kama ndivyo, basi nafikiri tumewahi sana kukimbilia kuunda bunge hili kwa sasa, na tulihitaji muda mrefu zaidi wa mchakato?
 
[h=1]Maswali saba ya Jaji Warioba[/h]
ico_plus.png
SHARE
ico_bookmark.png
BOOKMARK
ico_print.png
PRINTEMAILRATING
warioba.jpg
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.PICHA|MAKTABA Na Fidelis Butahe, Mwananchi

Posted Alhamisi,Aprili24 2014 saa 24:0 AM

KWA UFUPI
"Tume inapewa lawama kubwa, wajibuni wananchi hii tume ilitumwa na nani kukusanya maoni ya wananchi? Waambieni ilikusanya maoni hayo kwa kutumia sheria ipi zaidi ya ile ya Mabadiliko ya Katiba?" alisema Jaji Warioba katika swali lake la nne.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ameuliza maswali saba ya msingi kwa wajumbe wa Bunge la Katiba wanaopinga Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume yake akitaka wawajibu wananchi ili kutuliza kiu yao.
[COLOR=#333333 !important]​

[/COLOR]
Jaji Warioba ambaye tangu awasilishe Rasimu ya Katiba Desemba 30, mwaka jana amegeuka kuwa adui kwa watu wanaotaka muundo wa serikali mbili, aliuliza maswali hayo jana katika uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa Taasisi ya Twaweza kuhusu mchakato wa Katiba.

Akizungumza kwa ukali, Jaji Warioba alisema: "Kwanza, jibuni kwa nini mnapinga muundo wa Muungano wakati walioupendekeza ni wananchi?

"Sheria inasema uwepo wa Muungano na mapendekezo katika rasimu hayasemi Muungano usiwepo. Kumbukeni kuwa wananchi walitakiwa kutoa mapendekezo ya namna ya kuboresha Muungano."

Katika swali lake la pili, Warioba alisema kwa nini Tanganyika imevaa koti la Muungano? Kwa kuwa katika ukusanyaji wa maoni wananchi walieleza kuwa Serikali ya Muungano ya sasa siyo ya Muungano, ni ya Tanganyika.

Katika swali la tatu alisema wajumbe hao wanatakiwa kujibu maelezo ya wananchi ambao waliieleza tume hiyo kuwa Katiba imevunjwa na madaraka ya rais yamechukuliwa na sasa kuna marais wawili katika nchi moja.

"Tume inapewa lawama kubwa, wajibuni wananchi hii tume ilitumwa na nani kukusanya maoni ya wananchi? Waambieni ilikusanya maoni hayo kwa kutumia sheria ipi zaidi ya ile ya Mabadiliko ya Katiba?" alisema Jaji Warioba katika swali lake la nne.

Katika swali lake la tano, Warioba aliwataka wajumbe hao kutoa sababu za kumtuhumu kuwa amependekeza muundo wa serikali tatu kwa sababu yeye pamoja na (Joseph Butiku) walikuwa wajumbe wa Tume ya Jaji Kisanga na Jaji Nyalali ambazo nazo zilipendekeza muundo wa serikali tatu, kitu ambacho alisema si kweli na hawakuwahi kuwa mjumbe wa tume hizo.

Pia, aliwataka wajumbe hao kujibu swali la sita, kwa nini hawataki kuzungumzia yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na badala yake wanageuza rasimu hiyo kuwa imeandikwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Katika swali lake la saba, aliwataka wajumbe kujibu kwa nini wanaishutumu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa imeingiza maoni yake, wakati ilikusanya maoni hayo kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba?

Alisema badala ya kujadili hoja za msingi, wajumbe wa Bunge hilo wamekuwa wakitoa lugha za kejeli na matusi kwa baadhi ya watu (akiwamo na yeye), kitendo ambacho alisema si sahihi na kinaweza kuligawa taifa kwa sababu yaliyomo katika Rasimu ya Katiba yametokana na maoni ya wananchi.

Katika uzinduzi huo walikuwepo baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo ambao ni Dk Hamisi Kigwangalla aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Julius Mtatiro, Maria Sarungi na aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole.

uelewa wangu ni kwamba suala la sample size lilikua na utashii wa kisiasa kwa kuangalia bajeti badala ya uhalisia (nadhani umenielewa)
Warioba ninge mwelewa kama ange toa hoja za msingi zaidi ya hizo mfano! Wajumbe wengi kila wanapo simama kuchangia utawasikia wana sema takwim zilizo pelekea kupatikana kwa rasim hiyo si sahihi, wengine si za kweli, wengine hazina mashiko na nk!

Kwa mtazamo huo kuna kiwango flani cha kitakwimu wajumbe wanadhani hicho kinge fikiwa basi maoni hayo yangekuwa valid! Sasa kwanini wanaendelea kijadili kitu ambacho hakina takwimu sahihi? Basi wavunje bunge watengeneze sample size inayo takiwa waipe tume nyingine irudi tena kwa wananchi ikusanye maoni kwa kiwango wanacho taka then wajadili upya!

Lakini pia hivi wao rasimu iliyo pendekeza serikali mbili wameitoa wapi? wanasema wanachi wanataka serikali mbili hiyo research waliifanya wapi saa ngapi na kwa nani na waka andika wapi ripoti yao kwa ajiri ya reference?

Lakini pia swali lingine la kujiuliza kama tume ya warioba iliyopewa kazi ya kukusanya maoni kisheria imefanya kazi mbovu kama wanavyo sema hawaoni ni tusi kwa aliye wateua pia? Kwamba hakuwa makini katika uteuzi wake kwa kuteua watu mizigo ambao wametumia gharama kubwa na kuleta kitu kisicho faaa?

Kwa mtazamo huu najenga picha kuwa kumbe hakukua na haja ya kuunda tume kwa kua wajumbe walio teuliwa walikuwa na maoni kabisa ya wanachi kwa nini wasinge enda tu moja kwa moja bungeni na kuyatoa huko wakatengeneza na rasimu yao waka ipitisha moja kwa moja?

Tusichezeane akili na hivi vyama vya siasa! Ifike mahala watu tuwe wakweli kama mnania ya kufanya kitu kifanyike sio kupindisha pindisha mambo mgekuwa wote mnataka umoja wakitaifa ninge waelewa kama mnataka serikali 1, mkawashawishi na wanachi lakini kwa kuwa kila chama kimeweka maslahi yake mbele ndio maana kila mtu anataka muundo wa serikali utako vutia maslahi yake!

Tanzania ya serikali moja kwanza!
 
Hao ndiyo Watanzania hawawezi hata kutambua mambo ya kawaida kabisa.Warioba sasa anaonekana kama ndiyo aliyependekeza yote yaliyomo kwenye rasimu ya Katiba ili hali yeye alikuwa miongoni mwa Wajumbe wa tume tofauti yake ikiwa ni kuwa yeye ndiyeliu mwenyekiti wa tume tu.Katika hali ya kawaida pale Dodoma wajumbe wale wanapaswa kuwa watambuzi wa mambo lakini tofauti hiyo haipo kabisa.Sasa tujiulize katika jamii yetu ya Kitanzania wajumbe wale ndiyo weledi kiasi cha kutambuliwa na Mamlaka za uteuzi kuwateua.Swali ni je kweli wanao uwezo wa kushughulikia suala nyeti kama hili la kutengeneza katiba ya nchi?.
 
Kinywa hutamka yaujazayo moyo! Waliobaki mjengoni ukiwaangalia kwa makini wanapotoa michango yao (kama ina hadhi ya kuitwa michango at all) utabaini hawako settled, even their vocal tones are hollow, their inner fears are vivid and you can even feel their pounding heartbeats though they pretend to be poised. The inner silent voice is haunting them, they are afraid!
 
Jaji Warioba amejibu propaganda zilizoanzishwa na JK baadae kupokewa na Lukuvi kuwa BLK likipitisha Serikali 3 nchi itatawaliwa na Jeshi kwa sababu Serikali itashindwa kulipa mishahara! Jaji Warioba ameonya wanasiasa Hawa uchwara kutumia taasisi nyeti ya Jeshi vibaya. Amehoji kwa nini lizungumziwe Jeshi na si polisi au Mawaziri ndio watashindwa kulipwa? Jaji ameongeza kuwa kwa nini ufisadi na rushwa visiwe ndio vichocheo vya kushawishi Jeshi kuasi? Na pia amehoji fedha za sasa za kulipa Jeshi zinatoka wapi? . Huyu mzee anastahili Ujaji

He is The judge and that i why he managed the CRC very effectively beside CCM intense pressure.
 
Najionea wazi wazi maadili ya wanaojiita viongozi yakishuka kwa kiwango kikubwa. Kwa nini kumjadili mtu tena kwa kejeli badala ya kilicholetwa?
Kwa nini kama hukubaliani na data au sample size iliyotumika usilete ulizofanyia kazi wewe?
Inakera sana mtu kuishia kutoa maneno ya kejeli wakati yeye hana data zozote.
 
Kinywa hutamka yaujazayo moyo! Waliobaki mjengoni ukiwaangalia kwa makini wanapotoa michango yao (kama ina hadhi ya kuitwa michango at all) utabaini hawako settled, even their vocal tones are hollow, their inner fears are vivid and you can even feel their pounding heartbeats though they pretend to be poised. The inner silent voice is haunting them, they are afraid!

You are right.
"Cowards die more times before their deaths" Shakespere
 
Warioba ninge mwelewa kama ange toa hoja za msingi zaidi ya hizo mfano! Wajumbe wengi kila wanapo simama kuchangia utawasikia wana sema takwim zilizo pelekea kupatikana kwa rasim hiyo si sahihi, wengine si za kweli, wengine hazina mashiko na nk!

Kwa mtazamo huo kuna kiwango flani cha kitakwimu wajumbe wanadhani hicho kinge fikiwa basi maoni hayo yangekuwa valid! Sasa kwanini wanaendelea kijadili kitu ambacho hakina takwimu sahihi? Basi wavunje bunge watengeneze sample size inayo takiwa waipe tume nyingine irudi tena kwa wananchi ikusanye maoni kwa kiwango wanacho taka then wajadili upya!

Lakini pia hivi wao rasimu iliyo pendekeza serikali mbili wameitoa wapi? wanasema wanachi wanataka serikali mbili hiyo research waliifanya wapi saa ngapi na kwa nani na waka andika wapi ripoti yao kwa ajiri ya reference?

Lakini pia swali lingine la kujiuliza kama tume ya warioba iliyopewa kazi ya kukusanya maoni kisheria imefanya kazi mbovu kama wanavyo sema hawaoni ni tusi kwa aliye wateua pia? Kwamba hakuwa makini katika uteuzi wake kwa kuteua watu mizigo ambao wametumia gharama kubwa na kuleta kitu kisicho faaa?

Kwa mtazamo huu najenga picha kuwa kumbe hakukua na haja ya kuunda tume kwa kua wajumbe walio teuliwa walikuwa na maoni kabisa ya wanachi kwa nini wasinge enda tu moja kwa moja bungeni na kuyatoa huko wakatengeneza na rasimu yao waka ipitisha moja kwa moja?

Tusichezeane akili na hivi vyama vya siasa! Ifike mahala watu tuwe wakweli kama mnania ya kufanya kitu kifanyike sio kupindisha pindisha mambo mgekuwa wote mnataka umoja wakitaifa ninge waelewa kama mnataka serikali 1, mkawashawishi na wanachi lakini kwa kuwa kila chama kimeweka maslahi yake mbele ndio maana kila mtu anataka muundo wa serikali utako vutia maslahi yake!

Tanzania ya serikali moja kwanza!

Yoga, ujue hizo ni tuhuma tu ambazo zinatolewa na wajumbe kutoka CCM. Kwa busara ya kawaida kabisa, kama wajumbe hao wana mashaka na TAKWIMU za Judge Warioba. Basi walitakiwa kumuita tena ndani ya BMK kuzitolea ufafanuzi takwimu zake. Kama angeshindwa kuwaondolea mashaka wajumbe, basi ndiyo wangekuwa na HAKI ya kumutuhuma kwamba AMEPIKA takwimu. Lakini CCM hawawezi kamwe kumuruhusu Warioba kurudi tena kwenye BMK kutoa ufafanuzi wa takwimu zake. Guess why? CCM wao ndiyo wana TORTURE hizo Statistics zikubaliane na matakwa yao ya S2. BTW, mtu(?) aliyeteua watu wabovu kumkusanyia maoni nafikiri mtu(?) huyo ndiyo MBOVU zaidi. Kama kweli mtu(?) huyo ni makini atawezaje kuteua watu wabovu wamkusanyie maoni? With all due respect hivi kweli watu kama akina Warioba, Salimu Ahmed Salimu wanaweza kuwa WABOVU kama unavyotaka kutuaminisha leo. If my memory still serves me correctly nakumbuka kama hawa watu "wabovu" Jugde Warioba alishawahi kuwa PM of URT na Salimu alishawahi kuwa Secretary General of OAU, PM of URT na pia mwafrika wa kwanza kabisa kugombea kiti cha Secretary general of UN! Hata kama watu hawa "wabovu" wameleta maoni ambayo haya kwenda na matakwa yetu i.e S2, sidhani kama ni haki to call them names. Give a dog a bad name and kill her.
 
-Warioba amebariki Serikali ya tatu kwa kigezo cha maoni ya wananchi kwa kutumia takwimu
-Wanaompinga nao wanasema takwimu alizotumia siyo za kweli.
-Mfumo aliotumia wa "sampling" haukufuata kanuni za mfumo huo
-Hakuweka takwmu za mabaraza ya katiba
Hivyo kusema kuwa maoni ya Serikali tatu ni maoni ya wananchi siyo. Kwa maana hiyo Warioba alitakiwa kujibu hoja hizi na siyo kutuletea tena maswali.
 
Usiite watu mbumbumbu mkuu, si ustaarabu.
Sijawai fanya takwimu,
Sijafuata maelekezo ya yeyote yule, nimewaza mwenyewe nikachanganya na wanosema ukawa na walio against ukawa nimeconclude serikali 3 italeta matatizo, nitapigia kura mbili,
Ni maoni tu

Ulichoandika umejidhihirisha unavyofuata Maelekezo! Uliona wapi muungano wenye SERIKALI mbili km ckukaririshwa,,,,!!!!???
 
Huwa najiuliza ulinzi anaoutegemea Warioba ni wa Mungu ama ni wa hao hao anao pambana nao???

Au kuna nini kinachoendelea??? Maana dunia ya sasa kuondoana maisha ni sekunde tu.

.
Kakutuma Mwigulu?
.
 
Back
Top Bottom