Maswali 7 ya Jaji Joseph Sinde Warioba

Maswali 7 ya Jaji Joseph Sinde Warioba

Wewe ndo unajiita unafikiri?? kwani hayo maswali si aliyajenga katika kujibu hoja? aliyaulizia wapi hayo maswali? chooni? ni kwamba hana majibu ya hoja na maswali yanayoulizwa kuhusu rasimu ya tume yake. Hawa Ghasia ana haki ya kumuambia afunge mdomo wake kwa kuwa anachokifanya ni kupigia debe serikali 3 badala ya kujibu hoja za msingi. Kwa hiyo wewe umemuona Hawa Ghasia kakosea kwa kumuambia Jaji Warioba afunge mdomo wake kisa ni former PM? na sio Tundu Lissu aliyemuambia Mwl Nyerere muasisi wa taifa letu kuwa alikuwa akiishi kwa uwongo na kuwalaghai watanzania?
Hawa Ghasia kwa hadhi gani aliyonayo ya kumwambia Mzee wetu Warioba afunge mdomo? Yeye asubiri 2015 inakuja arudi kuwa bibi shamba ,maana shemeji hatakuwepo tena Magogoni.
 
Moja ya kosa ililofanya tume ni kuacha mapendekezo mengine muhimu katika Rasimu hii, mfano mmoja mpaka sasa kuna serikali 2 sasa kwanini nayo isiingizwe ili wajumbe wachambue mapungufu yake na mazuri yake wananchi tupambanue, huwezi kungo,oa mfumo uliopo kwa Rasimu tuu bila ya kuwepo majadiliano, huo ni uhunu mkubwa kbs ambao tume imefanya na ndio nasema chanzo cha mgogoro huo ni tume. Sasa kwa kuwa jambo laenyewe limeenda kwa wadau wenyewe unategemea litapita kimya kimya? Haiwezekani.

Sijui hata kama unajua ilichoandika. Samahani lakini.
 
Siri: UVCCM Inampango Wakuchoma tena Makanisa kama Ukawa watafanya mikutano Zanzibar.

Ndugu Wazalendo wa Zanzibar na Wale wa Tanganyika/Tanzania Bara ambao wanaipendelea Nchi yetu hii impya ya Tanzania kuwa na Umoja, amani, Utulivu na Muungano wenye Muundo wa Serikali 3 ambao utaondoa kero na manunguniko. Napenda kuwajuilisha kwamba nimepata habari kutoka kwa Sheha mmoja wa CCM ambae mimi ni jamaa yangu wa damu.
Amesema UVCCM wameanshaandaa Kufanya fujo visiwani ili Wa Wadis-rupt (wawaharibie) UKAWA pindipo kama watafanya Mikutano Zanzibar. Hoja hiyo inaaminika kuwa ni mpango mwengine kabamba wakutaka Kumshinikiza Maalim Seif na Ugaidi katika Chama chake CUF. HIvo Ile hoja ya LUKUVI kusema kwamba wanaogopa Serikali ya Kiislamu inaweza kujengwa zaidi hapo pindipo Makanisa mengine yatachomwa Visiwani..
Tunatakiwa tuichukue habari hii in a Serious matter niko mbioni kuipata barua waliojiandaa CCM na nitaiweka hapa kama itawezekana..
Nawasilisha Ujumbe.
 
Ondoa hoja uchwara hapa, watu ujibu hoja kwa hoja na si tabo na taarabu. Kwanza nani alikwambia Warioba ndiye aliyeandika Rasimu ya Katiba. Hii Rasimu imeandikwa na watu wanaoheshimika, mbona hamtaji Jaji Mkuu mstaafu Agustino Ramadhan ambaye alikuwa makamu Mwenyekiti, ni mtu mashauru sana hapa nchini, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi huru za Afrika hivi sasa Umoja Afrika AU Dk. Salim Ahmed Salim si mtu wa kubeza mataifa yanamheshimu sana, wako waadhili wa sheria, mhadhiri wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Paramagamba Kabudi na marehemu Dk. Sengodo Mvungi si watu wa kuokoteza. Kwa hiyo unapokuwa unabeza husiangalia kwa kukaririshwa na kuwa kasuku. Hapa ulipo sidhani hata siku moja utawahi kuwafikia watu hawa kwa sifa hata upande mlima Kilimanjaro

Warioba amevurugwa kwa kiasi kikubwa sana anashindwa afanye lipi kwenye maisha yake alivyodanganya alijua kuwa kazi imeisha kumbe alikuwa anajaribu kina cha maji kwa miguu yote miwili.
 
Tume ya jaji warioba upande wa mfumo wa muungano wamekosea mh mbunge, alafu si wananchi wote walopropose serikali 3,
Hiyo kitu italigawa taifa in the longrun it is obvious.

hivi wewe umeshawahi kufanya utafiti wa kitakwimu?

halafu kweli kwa akili yako kweli ulitaka wananchi wote wahojiwe km wanataka serikali ngapi?

au ulitegemea wananchi wote waliohojiwa watake serikali tatu ndiyo ingekuwa halali kwa tume ya warioba kupendekeza muundo wa serikali tatu?
 
Ondoa hoja uchwara hapa, watu ujibu hoja kwa hoja na si tabo na taarabu. Kwanza nani alikwambia Warioba ndiye aliyeandika Rasimu ya Katiba. Hii Rasimu imeandikwa na watu wanaoheshimika, mbona hamtaji Jaji Mkuu mstaafu Agustino Ramadhan ambaye alikuwa makamu Mwenyekiti, ni mtu mashauru sana hapa nchini, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi huru za Afrika hivi sasa Umoja Afrika AU Dk. Salim Ahmed Salim si mtu wa kubeza mataifa yanamheshimu sana, wako waadhili wa sheria, mhadhiri wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Paramagamba Kabudi na marehemu Dk. Sengodo Mvungi si watu wa kuokoteza. Kwa hiyo unapokuwa unabeza husiangalia kwa kukaririshwa na kuwa kasuku. Hapa ulipo sidhani hata siku moja utawahi kuwafikia watu hawa kwa sifa hata upande mlima Kilimanjaro

Umesema vema kuwa hawa ni watu wenye taaluma, weledi na heshima zao. Lakini tusiwe watumwa wa fikra kwa kujaji mtu kwa weledi na sifa zake, kumbuka hapa hatujaji mtu isipokuwa kazi yao, hivyo tutaijaji rasimu kwa maudhui na mantiki yake badala ya kumuangalia mtu usoni. Tuanze hoja kama ifuatavyo;.....

Kumbuka rasimu ya kwanza ilibeba maoni ya wananchi waliyoyatoa kwenye mikutano ya tume.
Rasimu ya pili ilitakiwa ibebe maoni ya wananchi kwenye mabaraza ya katiba. Lakini cha kushangaza, kwa makusudi kabisa tume iliyarudia maoni yaleyale ya wananchi kwenye mikutano yake kutengeneza rasimu ya pili na maoni ya mabaraza ya katiba yakawekwa kando.
Kumbuka maoni ya wananchi kwenye mikutano ya tume haikuwa na utaratibu maalum kiuwiano katika uwakilishi na pia mikutano hiyo ya tume haikuweza kufanyika katika maeneo yote ya Tanzania, ndio maana hata matokeo yake yanatiliwa shaka kitakwimu.
Maoni ya mabaraza ya katiba yalikuwa na utaratibu maalum kiuwiano katika uwakilishi na pia yalifanyika katika wilaya zote za Tanzania, hivyo basi maoni haya ndiyo yangetoa matokeo sahihi yanayoakisi utashi wa wananchi.

Kuna swali muhimu sana ambalo Jaji Warioba na wenzake wameshindwa kulijibu, sitokaa katu kuiamini rasimu ya tume kuwa ni maoni ya wananchi mpaka wajibu swali lifuatalo;

SWALI: "Kwanini tume haikuyaingiza wala kuzingatia maoni ya mabaraza ya katiba katika rasimu ya pili? hali ya kuwa ndiyo maoni pekee ambayo yamezingatia kwa usahihi uwiano wa uwakilishi kwa Tanzania nzima, na badala yake wametumia maoni yaleyale yaliyotumika kutengeneza rasimu ya kwanza ambayo yametokana na mikutano ya tume"

Maoni mengi ya mabaraza ya katiba yamependekeza serikali 2, kutoingizwa kwake kwenye rasimu inaniaminisha kuwa tume ilikuwa inachagua kipi cha kuingiza na kipi cha kuacha ili kuakisi utashi wao binafsi.
Kilichofanywa na tume ni kiini macho kwa kutuaminisha kuwa rasimu ya katiba imetokana na wananchi hali ya kuwa ni maoni yao binafsi.
 
Huwa najiuliza ulinzi anaoutegemea Warioba ni wa Mungu ama ni wa hao hao anao pambana nao???

Au kuna nini kinachoendelea??? Maana dunia ya sasa kuondoana maisha ni sekunde tu.

Hao wauaji nao saa nyingine wanachoka, una habari huwa wanapambana na maruweruwe ya roho ngapi walizozipoteza? Ndio maana wakati mwingine utashangaa kama kweli mtu ana akili timamu au la kwa maneno wanayoongeana matendo wanayofanya, kuua mtu si kitu rahisi sana, damu ya mtu ina nguvu sana, unaweza rukwa na akili, hujawahi kuona au kusikia mtu kaua halafu akawehuka moja kwa moja? Wanajua hakuna siri iwapo wataondoa figure nyeti
 
Fuatilia Dk 45 ITV LEO UMUONE MZEE WARIOBA AKIWACHOMA WATU KWA SINDANO YA MAJI YA MOTO
 
Nishawahi 'kusikia'-ukiwapa SMZ wawe na serikali yao, Tz bara itakosa mapato mengi ya wahisani, zenji itakuwa tishio kijeshi, na itatumia effective rasilimali zao za baharini, mafuta na gesi.
Hii kitu Kikwete and his team hawataruhusu kamwe wajitenge. Lakini ukweli ni kwamba unapokuwa na nchi mbili huru...huwezi kukwepa serikali tatu.
Na hayo maswali ya Jaji Warioba hakuna mwana CCM atayeweza kuyajibu pale Bungeni miaka 100. Mchakato ulikuwa wa wazi, ni wapi Sinde kaingiza wazo lake la serikali 3 ?

Halafu hao wabunge wa CCM mbona kama siwaelewi, ni kweli Rasimu inataka Muungaano uvunjwe? manake ndo wanachoshupalia. Serikali 3 haivunji Muungano bali inaboresha tu. Ujio wa Yesu si kutengua torati ni kuiboresha.
Tanganyika haikwepeki katu.
Mkuu, wanamsubiri mwenyekiti aokoteze majibu toka kwa 'intellectually dishonest' ndipo wacopy n paste.
 
Kwa taarifa yako Rasimu hii kwa sura ya kwanza na sita haitaji hata phd ya kuichambua inajionesha wazi mapungufu yake, Kwanza kwa takwimu za maoni hazijakidhi uwakilishi, pia muundo wenyewe na mambo ya msingi kuhusu Manufaa na hasara za kuwa na serikali tatu, kama katiba pia kuna hofu ambayo hata tume imekili juu Ya uhai wa serikali yenyewe sasa kwa nn msikubaliane na maoni ya wanaotaka serikali mbili? Ni ubishi ambao hauna maana yeyote na kutaka kuwabebesha mzigo watanzania kwa manufaa ya kisiasa, ni dhahili kbs msingi wa hoja ya serikali tatu ni hitaji la kisiasa, na tunaposema ki siasa nina maanisha kuwa kuna kundi linataka kutawala au kuwa sehemu ya utawala kwa kupitia katiba lakini cyo kwa manufaa ya wananchi ambao ndio wadau wa hiyo serikali yenyewe.. kuna hoja ya tume kuwa haya ni maoni ya wananchi , tujiulize ni mwananchi gani wa kawaida ambaye ana kero za maji, afya, elimu ,ajira ,malipo ya uzeeni , mishahara kwa watumishi kama wa elimu na kadhalika akaona Jibu la kuwa na serikali ya tatu atapata ufumbuzi?,, hii c kweli kbs, wakati wa mchakato tulimbiwa tupunguze madaraka ya Rais,halafu leo wajumbe wengine wanasema kuwa Rais wa jamhuri amepokonywa madaraka, na wakati huo huo tunaongeza serikali ingine,, jambo lingine tume inasema serikali washirika zitasimamia mambo yao ya maendeleo huku serikali.za mitaa ambazo ndizo karibu na wananchi mnaziondoa hii imekaaje? Ki uhalisia tunahitaji mjadala mpaka juu ya Huu muundo na mm naona kuna haja ya kurudi kwa wanachi juu ya hii sura ya kwanza na sita na cyo kuwaa hia wajumbe wa bunge maalumu sababu wengine wanakichukulia ki siasa zaidi.

Hayo uliyoandika nimeshayasikia mara nyingi kwenye hili kundi la serikali mbili. Nawe umeyadaka au nawe ni mmoja wao. Yote ni rubish. Rubish kabisa! Yaani kwa kuwa wananchi wana matatizo ya barabara, maji, elimu, afya, ajira, n.k. Yote uliyoyataja ndo tuache kujadili muundo wa serikali ktk katiba? Kwa nini CCM miaka 50 ya utawala wake haijaondoa matatizo hayo ndani ya serikali 2? Yaani tubaki tulivyo kwa uzembe wa CCM! Nonsense!

Matumizi makubwa hayatokani na idadi ya serikali. Sasa hivi zipo mbili, matumizi ni madogo? Ninyi munaamua kugawana pesa ya serikali na kujenga vituo vya mafuta na kununulia UDA halafu munasema serikali ni mzigo? Sitaki kabisa uzembe wa kufikiri.

Mtu anaitwa kiongozi halafu anatafuta vyanzo vya mapato ya serikali kwenye katiba. Katiba itaje vyanzo vya mapato? Halafu anasema ameisoma sana! Wapi bwana! Kaambiwa tu naye akadaka.

takwimu ziko ok! Uliza swali nikujibu kuhusu hizo takwimu. Kazi hiyo naijua kuliko mbunge yeyote wa CCM.
 
Warioba amezeeka,tena mbaya zaidi amezeeka ubongo! tofauti na Hayati Baba wa Taifa Julius K.Nyerere ambaye inasemekana kadri alivyokuwa anazeeka ndivyo akili yake ilivyokuwa inakuwa kali kama ''WEMBE"! Kama kweli maswali hayo yametoka kwa WARIOBA basi naomba apumzike! Ni maswali ya KITOTO kabisa! Swali lake la kwanza, katiba hiyo haijatokana na Wananchi wa Tanzania! Tunakubali ni wananchi kwa maana ya Warioba na wajumbe wake wa Tume basi! Yako wapi maoni ya Mabaraza ambayo ndiyo yalikuwa uwe msingi wa rasimu ya pili! WARIOBA JIBU HILO KWANZA!

Kwa nini munahangaika kutafuta maoni ya mabaraza ya katiba? Mabaraza ya katiba yalikuwa ni ya watu wa CCM! Ktk ukusanyaji wa takwimu hakuna haja ya kutumia takwimu ambazo ziko biased na ndiyo maan CCM WANATAFUTA TAKWIMU ZAO. Walipanga ili ionekane ni wengi. Kumbuka mabaraza yalitakiwa kujadili draft siyo kutoa maoni ya awali. Tunapoteza muda kutumia kigezo cha takwimu wakati kati yenu hakuna mtaalamu wa takwimu. Nonsense!
 
Alisema wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba ikikusanya maoni ya wananchi, wanajeshi na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini walijikita zaidi kutoa maoni ya kuimarishwa kwa ulinzi na usalama na siyo mambo mengine.


“Tatizo ambalo walitueleza ni kuchoshwa na kitendo cha kupiga mizinga 21 kwa Amri Jeshi Mkuu wakiwa Dar es Salaam na wakiwa Zanzibar. Walisema kwa nidhamu ya jeshi, Amri Jeshi Mkuu ni mmoja tu. Nadhani mngewaondolea kero hiyo na si mambo mengine,” alisisitiza.
 
Jibu ni NDIO.
Takwimu za tume ya Warioba zina makosa, tena makosa makubwa ambayo yanafanya kila hitimisho lililoegemea takwimu hizo kuwa na makosa. Tena mbaya zaidi ni kwamba makosa yao si ya kibahati mbaya ya kiubinadam, isipokuwa ni ya makusudi na yaliyopangwa ili tu yaakisi utashi wao binafsi kwa kutumia mwamvuli wa utashi wa wananchi. Huku ni kuwahadaa watanzania na kuwafanya ni mbumbumbu kwa kugeuza maoni yao binafsi kuwa ni ya wananchi kama wanavyotaka kutuaminisha.
Na hata kama takwimu zao zingekuwa ni sahihi, lakini bado hitimisho lao la serikali 3 halikubaliani na takwimu zao wao wenyewe japo ni za nadharia tu na si uhalisia.

sitaki urudi shuleni. Kwa nini unasema makosa makubwa bila kusema maana ya makubwa? Huonekani kuwa mtaalamu. Sema hasa. Kosa liko wapi? Takwimu ina kitu kinaitwa systematic error na kingine kinaitwa random error, Kwa CCM wanataka kusema kwamba Warioba amefanya mistake. Natumia maneno ya kiingereza ili kuonyesha upungufu wa CCM. kama unaweza nitajie mtu hata mmoja anayejua elimu ya takwimu kati ya hao wana CCM.
 
Jaji warioba yupo vizuri!watu hawajadili katiba, hawasikilizi maoni ya wananchi! Nchi inaendeshwa kidictator.
 
Hongera jaji walioba. Mungu yupo mbele yako na wanainchi tupo nyuma yako. Hamna mwingine anaweza dhubutu sema ukweli kama ambavyo unafanya na wengine wote wanafiki tu. Nchi hii itaingia kwenye machafuko sio kwaajili ya upinzani bali ni kwasababu ya chama tawala kung' ang'ania madalaka. Kila kitu kina mwisho wake kama sio leo basi kesho. Wananchi wa leo sio wa mwaka 1964 chonde jamani tukubali transition kwa amani.
 
Huyo Jaji Warioba ni miongoni mwa watu waliokuwa washauri wa Baba wa Taifa enzi za utawala wake, sasa inakuwaje watoto waliozaliwa miaka ya hivi karibuni waruhusiwe kusimama Bungeni na kumshambulia kuwa hana nia nzuri na taifa, ingekuwa hivyo si angeanza enzi hizo ? Ikumbukwe kuwa sio mfano mzuri mtu mzima kama yule kusemwa vibaya kiasi hicho, inatoa mafundisho mabaya kwa kizazi kijacho kwa maana kuwa hakitakuwa na heshima kwa watu wazima.

Sawabho;
Shetwan hawezi kumheshimu mtu yeyote. Umri wako weye hujawahi kumwona mtoto aliye laaniwa akiinuka na kumpiga babake au kumtusi au kumdharau? Hayo ndo yanayotokea BMK leo hii. Na hiyo ndo kazi ya shetwan.
Wote wameamua kumpendeza aliye watuma mle. Hujajiuliza, hiyo rasimu ya serekali 2 wanayo ijadili wameitoa wapi??? Kwani walipelekwa BMK kujadili rasimu mpya au kuiboresha rasimu ya pili ya Warioba ambayo iliyabeba maoni ya wananchi?
Kuhusu Jeshi kupindua, hilo sio jambo geni kwa ccm, kumbukeni kila mara uchaguzi ukianza tu, Picha na matangazo mengi TBCCM huwa ni kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya Rwanda kila siku. Kuleta hofu kwa wale wapenda mabadiliko. Tumewazoea.
Naamini hizi mbinu za ccm kugandamiza wananchi zitafunuliwa siku moja na kuwekwa wazi tu na Mungu yupo aliyesema; Amtukanaye babaye, kunguru wa kondeni watamla macho yake. We are just waiting for that day. Uovu haufunikwi kwa wingi wa uovu.
CCM wenzangu badilikeni. Turudi kwenye kilicho tupeleka BMK. Tujadiliane jinsi ya kuifanya iwe bora zaidi, kuulinda muungano wetu. Tujadili jinsi ya kuimarisha serekali ya Muungano baada ya kuivua koti serekali ya Tanganyika. Tumeshaona shida iko kwenye mapato sasa tujadili namna ya kuipatia mapato halali na ya kudumu.
Baba wa taifa aliwahi kusema; A corrupt Government will not collect Taxes from the big shots but only from the petty traders. Mzee wa Vijisenti akaona mahali pazuri pa kupata kodi ni kwenye line za simu. Oh! Holy cow! Sijui alikuwa anawaza nini. Huyo mwenye huo mtandao wa hiyo simu amepewa likizo ya kodi, mlaji ndiye alipe, sijui mlimwelewa??
This is my Tanzania.
Wabunge wa BMK, jadilini rasimu sio watu na vijimambo. Poleni zenu tu. Mmesema mtakuja kutueleza uongo wa UKAWA, sawa ila kwa lugha hiyo ya bungeni, sidhani kama kuna atakayewavumilia. Tuna njaa ya haki, msijetucheulia mitumbo yenu iliyo vimbirwa na kodi zetu.
 
Umesema vema kuwa hawa ni watu wenye taaluma, weledi na heshima zao. Lakini tusiwe watumwa wa fikra kwa kujaji mtu kwa weledi na sifa zake, kumbuka hapa hatujaji mtu isipokuwa kazi yao, hivyo tutaijaji rasimu kwa maudhui na mantiki yake badala ya kumuangalia mtu usoni. Tuanze hoja kama ifuatavyo;.....

Kumbuka rasimu ya kwanza ilibeba maoni ya wananchi waliyoyatoa kwenye mikutano ya tume.
Rasimu ya pili ilitakiwa ibebe maoni ya wananchi kwenye mabaraza ya katiba.
Lakini cha kushangaza, kwa makusudi kabisa tume iliyarudia maoni yaleyale ya wananchi kwenye mikutano yake kutengeneza rasimu ya pili na maoni ya mabaraza ya katiba yakawekwa kando.
Kumbuka maoni ya wananchi kwenye mikutano ya tume haikuwa na utaratibu maalum kiuwiano katika uwakilishi na pia mikutano hiyo ya tume haikuweza kufanyika katika maeneo yote ya Tanzania, ndio maana hata matokeo yake yanatiliwa shaka kitakwimu.
Maoni ya mabaraza ya katiba yalikuwa na utaratibu maalum kiuwiano katika uwakilishi na pia yalifanyika katika wilaya zote za Tanzania, hivyo basi maoni haya ndiyo yangetoa matokeo sahihi yanayoakisi utashi wa wananchi.

Kuna swali muhimu sana ambalo Jaji Warioba na wenzake wameshindwa kulijibu, sitokaa katu kuiamini rasimu ya tume kuwa ni maoni ya wananchi mpaka wajibu swali lifuatalo;

SWALI: "Kwanini tume haikuyaingiza wala kuzingatia maoni ya mabaraza ya katiba katika rasimu ya pili? hali ya kuwa ndiyo maoni pekee ambayo yamezingatia kwa usahihi uwiano wa uwakilishi kwa Tanzania nzima, na badala yake wametumia maoni yaleyale yaliyotumika kutengeneza rasimu ya kwanza ambayo yametokana na mikutano ya tume"

Maoni mengi ya mabaraza ya katiba yamependekeza serikali 2, kutoingizwa kwake kwenye rasimu inaniaminisha kuwa tume ilikuwa inachagua kipi cha kuingiza na kipi cha kuacha ili kuakisi utashi wao binafsi.
Kilichofanywa na tume ni kiini macho kwa kutuaminisha kuwa rasimu ya katiba imetokana na wananchi hali ya kuwa ni maoni yao binafsi.

Umetumia akili ndogo sana kufikiri na kutoa hoja yako. Unafikiri mabaraza ya katiba yaliwekwa ili kutoa maoni ya kutengeneza Rasimu nyingine ambayo ni tofauti na ya kwanza au yaliwekwa kwaajili ya kuboresha Rasimu ya Kwanza? Lakini ninavyokuona unahasira kwasababu unaona kama vile maoni ya mabaraza ya CCM yamewekwa kando. Mabaraza yalikuwa mengi tena mengine yakiwakilisha makundi makubwa ya wafuasi wake. Kwataarifa yako BAKWATA, TEC, PCT,TCC, haya ni baadhi tu ya mabaraza ambayo yanawakilisha wafuasi wengi lakini yalipendekeza serikali 3. Hatutungi katiba ya CCM wala CHADEMA au CUF, tunatunga katiba ya wananchi wa Tanzania wenye itikadi tofauti za kidini na kisiasa. Leo CCM wakilazimisha katiba yenye mtazamo wa itikadi yake, kesho CUF wakiwa madarakani nao wataifumua katiba ili iendane na matakwa yao, namna hii hatuwezi kufika. Lazima pawepo maridhiano na utashi wa kutosha kuhakikisha kwamba katiba inayotungwa itatufaa Watanzania kwa miongo mingi ijayo.
 
Ni kweli kodi zetu zinaliwa, sisi kitaa tumechoka balaa, wabunge wanajadili uozo. Mimi namshangaa mwenyekiti wa bunge la katiba amekua weak sana. Ama kwa sababu waliobakia wote ccm! Watu wanatoka nje ya hoja yeye yupo kimya tu! Wabunge wanasutana yupo kimya! Hawajadili kilichowapeleka!sikutegemea mwenyekiti angekua Hana nguvu.
 
" Katika kero ambazo wamekuwa wanatueleza wanajeshi ni kupiga mizinga 21 kwa amiri jeshi huko dar.....na amiri jeshi mwingine huko Zanzibar.....amiri jeshi kwa kawaida huwa mmoja ...mjitahidi kuwaondolea wanajeshi kero hii" - Warioba

nimejifunza jambo jipya hapa, kuwa nchi moja ina marais wawili na 'Amiri Jeshi Wakuu' wawili.
 
Huyo mpenda Fujo(Ghasia) alitakiwa kamamsomi wakweli kuwashauri wenzie waji kitezaidi katika kujadili Rasmi badala ya kumjadili Warioba, kwani hawa kuitwaBungeni kumjadili mtu.
 
Back
Top Bottom