Maswali 7 ya Jaji Joseph Sinde Warioba

Maswali 7 ya Jaji Joseph Sinde Warioba

Warioba amevurugwa kwa kiasi kikubwa sana anashindwa afanye lipi kwenye maisha yake alivyodanganya alijua kuwa kazi imeisha kumbe alikuwa anajaribu kina cha maji kwa miguu yote miwili.

Wewe nawe kila kitu lazima udandie na kuandika upuu.zi huoni aibu? Unalipwa shilingi ngapi kwa kujivua kwako akili? Naomba nikuambie, wewe umejidhihirisha kuwa ni binadamu asiye na hoja ya msingi na anayeweza kutumika vyovyote vile kwa furaha ya wengine. Hata kama uko nyuma ya keyboard na hakuna akujuaye jaribu kuona aibu kidogo. Mbona ukiwa peke yako MSALANI huwezi fanya mambo ya ajabu kwa vile tuu watu hawakuoni?
Mzee Warioba amejidhihirisha kuwa sio saizi yenu.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Warioba nafasi yake ilishakwisha kwenye tume, now he is just senior citizen kama wengine
 
Warioba asipoangalia atazeeka mara mbili yeye akae kimywa dawa iweze kuingia alipotosha sana sasa moto unamwakia anajuta na mikono kichwani.

utazeeka wewe utamuacha, unadhani yule mzee ni wa kawaida yule ni deep sea bana ana watu mamilioni nyuma yake gusa uone
 
Laana ni mbaya, imewakumba ccm sasa wanavaa cp kichwani sasa na kuwashambulia wazee wao wenye busara ati wao ndo wakali zaidi. Ukimsikia nepi naiwe unapata kinyaa kabisa! Mimi nafungaga TV kila kijani kinapoanza maana baada ya kijani unaona sura hiyo na matusi pamoja na mapovu yakitoka midomoni utadhani kanywa sumu. Bora hata Kinana anaongelea masuala.
 
Usiite watu mbumbumbu mkuu, si ustaarabu.
Sijawai fanya takwimu,
Sijafuata maelekezo ya yeyote yule, nimewaza mwenyewe nikachanganya na wanosema ukawa na walio against ukawa nimeconclude serikali 3 italeta matatizo, nitapigia kura mbili,
Ni maoni tu
 
Wangapi walipendekeza serikali mbili?

Hiyo safi!

Kina mjumbe mmoja eti anajiita profesa naye alitaka aelezwe maoni ya mabaraza yaliwekwa wapi. Niliamua kumuita ----- wa utafiti maana hajui kwamba kila takwimu zinahitaji kusafishwa. Mabaraza ya katiba yote yalipangwa na ccm na hayakutoa haki sawa. Wote tulisikia watu wakipigiwa simu kuulizwa misimamo yao kabla tume haijawatembelea. Kwa nini uchukuwe takwimu ambazo ni biased?
 
Wewe umewahi kukusanya takwimu au nawe unafuata maelezo ya hao mbumbumbu wa Dodoma? Ukiwa na maswali kwenye dodoso, lini watu wote wameshawahi kujibu maswali yote?

naomba ujieleze wewe mwenyewe kama kweli umewahi kufanya uchambuzi wa takwimu za kitafiti na hasa wa aina hii yaani maswali ya kisosholojia maana hapo hatukuwa na sayansi? Hatukutegemea jibu sahihi.

nenda shule bana mbona zipo nyingi tu kasomee statistical analysis utabain kama warioba alikuwa sahihi au la wewe unamsikiliza komba na sendeka walokimbia shule.
 
Nishawahi 'kusikia'-ukiwapa SMZ wawe na serikali yao, Tz bara itakosa mapato mengi ya wahisani, zenji itakuwa tishio kijeshi, na itatumia effective rasilimali zao za baharini, mafuta na gesi.
Hii kitu Kikwete and his team hawataruhusu kamwe wajitenge. Lakini ukweli ni kwamba unapokuwa na nchi mbili huru...huwezi kukwepa serikali tatu.
Na hayo maswali ya Jaji Warioba hakuna mwana CCM atayeweza kuyajibu pale Bungeni miaka 100. Mchakato ulikuwa wa wazi, ni wapi Sinde kaingiza wazo lake la serikali 3 ?

Halafu hao wabunge wa CCM mbona kama siwaelewi, ni kweli Rasimu inataka Muungaano uvunjwe? manake ndo wanachoshupalia. Serikali 3 haivunji Muungano bali inaboresha tu. Ujio wa Yesu si kutengua torati ni kuiboresha.
Tanganyika haikwepeki katu.
 
Bunge la katiba kwa sasa ni kama ukakasi usioweza kuustahimili, inatisha lakini inasikitisha sana jinsi mtu anajipambanua msomi, mwelewa, sijui nini, huku akitoa hoja za kukashfu na kukejeli tume ya kukusanya maoni, mbaya zaidi anajadili watu badala ya kujadili kilichomo kwenye rasmu,kutoa vitisho na uchafu mwingine mwingi. Ila tukubali tusikubali, waTZ wa sasa siyo wa enzi za zidumu fikira bila kujali kama zina tija au hazina
 
Aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya mabadaliko ya katiba jaji JOSEPH S WARIOBA ametoa maswali saba kwa wale wa wanao mkejeli na kumpiga vijembe likiwezo, la kutaka majibu ya kwanini Tanganyika imevaa koti la muungano kwa miaka miaka mingi?.

Maswali mengine ni:
-kwanini wajumbe wanakataa muundo wa serikali uliopendekezwa na wananchi?

-kwanini wanasema tume ilipendekeza maoni ya tume na sio wananchi?

-kwanini wanasema warioba alikua mjumbe wa akina Nyarari iliyokua ikitaka serikali 3?
We unazungumziaje suala hili?
 
!
!
jeshi linaweza kuasi. Wako sahihi kwani jeshi lenyewe ni la ovyo ovyo tu. Badala ya kukomaa na tafiti mbalimbali jeshi letu lipo busy na gesi mtwara

Hahaaa wenyewe wakiisoma hii utatafutwa ka Usama...!! Lol sidhani kama Jeshi lina habari na takwimu za katiba.
 
Warioba nafasi yake ilishakwisha kwenye tume, now he is just senior citizen kama wengine

Sasa iweje maandiko yake mnataka kuyachakachua? Si ashasema sheria ya rasimu ndo ilitumika kuandika rasimu...so mnakimbia kivuli chenu nyie.
 
Wacha liasi tuone. Kwa dunia ya sasa hamnaga hayo mambo coz hawatawala kwa amani zaidi ya kutengwa na kuwekewa vikwazo lukuki vya uchumi kiufupi hali ndo itakua mbaya zaidi. Nasema tena haiwezekani.
 
Usiite watu mbumbumbu mkuu, si ustaarabu.
Sijawai fanya takwimu,
Sijafuata maelekezo ya yeyote yule, nimewaza mwenyewe nikachanganya na wanosema ukawa na walio against ukawa nimeconclude serikali 3 italeta matatizo, nitapigia kura mbili,
Ni maoni tu

Huo ni uamuzi mzito. Kabla hujaamua kusema serikali mbili let yourself be informed! Usiwafuate CCM au UKAWA wote hao wanaweza kuwa nje ya ukweli. Ndani ya JF tunaelimishana na ndo maana nikakuuliza kama ulishafanya utafiti au hata kuchambua Takwimu. Ungependa kufahamu undani wantakwimu hizi, ningekueleza jinsi Warioba alivyo sahihi.

Tume iliyumia SPSS ambayo hata hao wajumbe walio wengi hawajui hata maana yake, uwezo wake na hata udhaifu wake. Wameamua kurukia au kufuata wanayoyasikia na kuyaona kwenye majedwali.

Hawa bado ni mbumbumbu!

Angalia, wanaombwa wabaki kwenye katiba na siyo watu lakini mtu anamaliza kuwaomba hivyo, anayefuata anaendelea na hayohayo! Wa kwanza anazungumzia jambo fulani, anayefuata naye anasema hilohilo bila hata kugundua kwamba limeshasemwa. Unajua maana yake? Ni ufahamu mdogo. Wanakuja na maneno na hawawezi kubadili hata kidogo.
 
Warioba asipoangalia atazeeka mara mbili yeye akae kimywa dawa iweze kuingia alipotosha sana sasa moto unamwakia anajuta na mikono kichwani.
anadai eti wanajeshi wamechoka kupiga mizinga 21 mara mbili,pointless.
 
Warioba amevurugwa kwa kiasi kikubwa sana anashindwa afanye lipi kwenye maisha yake alivyodanganya alijua kuwa kazi imeisha kumbe alikuwa anajaribu kina cha maji kwa miguu yote miwili.


We tangu usikiye neno kuvurugwa unajiona na wewe mjanja!

Kubwa jinga ata ungeishi miaka 1000 bado utakuwa kubwa jinga we
Una ubongo wa kuku huwezi ongelea mambo ya binadam wenye akili na busara kama mzee warioba
 
nenda shule bana mbona zipo nyingi tu kasomee statistical analysis utabain kama warioba alikuwa sahihi au la wewe unamsikiliza komba na sendeka walokimbia shule.

Unasema nini wewe? Uko Jf au kundi la wanywa lubisi? Shule ziko nyingi wapi? Nenda chuo cha maana, siyo useme vyuo vingi, hata vya CCM. Soma unamjinu nani na kasema nini!
 
Back
Top Bottom