john jrr
Member
- Feb 23, 2014
- 7
- 0
Warioba ninge mwelewa kama ange toa hoja za msingi zaidi ya hizo mfano! Wajumbe wengi kila wanapo simama kuchangia utawasikia wana sema takwim zilizo pelekea kupatikana kwa rasim hiyo si sahihi, wengine si za kweli, wengine hazina mashiko na nk!
Kwa mtazamo huo kuna kiwango flani cha kitakwimu wajumbe wanadhani hicho kinge fikiwa basi maoni hayo yangekuwa valid! Sasa kwanini wanaendelea kijadili kitu ambacho hakina takwimu sahihi? Basi wavunje bunge watengeneze sample size inayo takiwa waipe tume nyingine irudi tena kwa wananchi ikusanye maoni kwa kiwango wanacho taka then wajadili upya!
Lakini pia hivi wao rasimu iliyo pendekeza serikali mbili wameitoa wapi? wanasema wanachi wanataka serikali mbili hiyo research waliifanya wapi saa ngapi na kwa nani na waka andika wapi ripoti yao kwa ajiri ya reference?
Lakini pia swali lingine la kujiuliza kama tume ya warioba iliyopewa kazi ya kukusanya maoni kisheria imefanya kazi mbovu kama wanavyo sema hawaoni ni tusi kwa aliye wateua pia? Kwamba hakuwa makini katika uteuzi wake kwa kuteua watu mizigo ambao wametumia gharama kubwa na kuleta kitu kisicho faaa?
Kwa mtazamo huu najenga picha kuwa kumbe hakukua na haja ya kuunda tume kwa kua wajumbe walio teuliwa walikuwa na maoni kabisa ya wanachi kwa nini wasinge enda tu moja kwa moja bungeni na kuyatoa huko wakatengeneza na rasimu yao waka ipitisha moja kwa moja?
Tusichezeane akili na hivi vyama vya siasa! Ifike mahala watu tuwe wakweli kama mnania ya kufanya kitu kifanyike sio kupindisha pindisha mambo mgekuwa wote mnataka umoja wakitaifa ninge waelewa kama mnataka serikali 1, mkawashawishi na wanachi lakini kwa kuwa kila chama kimeweka maslahi yake mbele ndio maana kila mtu anataka muundo wa serikali utako vutia maslahi yake!
Tanzania ya serikali moja kwanza!
Mm nimekuelewa ukwel cna hata mda wa kusikiliza mbili Wala tatu moja ndo mpango cuzz zote mbili na tatu ukitizama kiundan zina matatizo au zitaleta matatizo baadae