Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Ni katika kuitafuta haki, kuondoa fitina, majungu au habari zisizo na mshiko na za kusadikikasadikika.
1. Ufisadi wa Richmond ukoje? Je tunaupembua kama rushwa, kukiukwa sheria & taratibu za uzabuni au ni matumizi Mabaya ya mamlaka & madaraka?
2. Kama Richmond ni Rushwa, ilitolewa namna gani, kwa nani na kwa nini mpaka leo hakuna ushahidi kamili ili suala lifuate mkondo kisheria[DN1] ?
3. Kama Richmond ulikuwa ni wizi, ni fedha gani ziliibiwa? Ni nani aliiziba au khidhinisha wizi? Ni nini hasa kilichoibiwa?
4. Kama Richmond ulikuwa ni Mkataba hewa, mkopo uliotolewa na CRDB umerudishwa? Mitambo iliyoletwa na mkataba kwanini vilihanishiwa Dowans?
5. Kama Richmond ni ukiukwaji wa kanuni, kuvunja sheria, kutumia madaraka vibaya, vipi wahusika hawajapelekwa mahakamani kama Mramba ?
6. Kama kwenye Richmomd, kamati ya bunge ilisema PCCB walifanya udhaifu na ujanjaujanja kufunika kweli, kwa nini Hosea bado yu madarakani?
7. Kama mkataba wa Richmond ulikuwa na walakini, hata kukiukwa na Richmond, kwanini uliuzwa kwa Dowans kisha Symbion badala ya kufutwa?
8. Kama Serikali kupitia CRDB waliweza kuikopesha Richmond, walete turbines, kwanini hatukuipa Tanesco huo mkopo wanunue mtambo uwe wao?
9. Je ni hasara ya kiasi gani iliingia Taifa kwa ujumla kwa Richmond kushindwa kuwa makini na imara kuzalisha umeme Kama ilivyotakikana?
10. Kama Richmond walishindwa na kuchelewa kuanza uzalishaji kwa mujibu wa mkataba, kwanini mkataba huu haukusitishwa mara moja?
11. Baada ya kashfa ya Richmond, ripoti ya Mwakyembe, kujiuzulu Lowassa, Serikali (PCCB, DPP, AG) walifanya nini kuendeleza uchunguzi?
12. Kwenye hili la Richmond, kwanini limeendelea kuwa jambo la utata na minong'ono ya tuhuma za ufisadi mpaka sasa? Rais kwanini yu kimya?
13. Kama CCM kweli ilitaka kuondokana na zimwi la Richmond, ufisadi wake na hata Lowassa, kwanini hadi leo tope na doa hili halijaondolewa?
14. Haki na ukweli lazima vifahamike na ukiri wa udhaifu na aibu uIshike CCM. Hatiwezi kuwa waadilifu na wawajibikaji tusipotatua Richmond!
15. Ili tuendele, kashfa, tuhuma na tetesi za IPTL, RAdar, Meremeta, Richmond, Loliondo nk, lazima zitatuliwe, sheria na haki zifanye kazi !
16. Tanzania Mpya, yenye matumaini na mabadiliko ni ndoto tuu, kama jinamizi la ufisadi na hizo kashfa zitazikwa bila ukweli kufahamika!