Pumzika kwa Amani Edward Ngoyai Lowassa

Tao

Member
Nov 10, 2018
95
157
Mhe Laigwanan. tumekupumzisha katika nyumba yako ya milele lakini kama mfuasi mwaminifu wa Bwana wetu Yesu Kristo tuna imani utafufuliwa mnamo marejeo ya Kristo parapanda itakapolia

Tanzania imempoteza kiongozi shujaa,mzalendo wa kweli,mchapa kazi ,mcha Mungu na kiongozi jasiri na asiyependa mzaha.

Ukiwa Waziri mkuu ndani ya muda mfupi tu ulianzisha sekondari za kata na wewe ndiye uliyeasisi ujenzi wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM)

Kabla ya hapo ulisimamia mradi wa maji ziwa Victoria ukiwa na maono kuwa maji hayo yafike Dodoma na wale wapuuzi walipokufanyia hila ukaamua kujiuzuru nafasi ya Uwaziri mkuu mwaka 2008 kila kitu kilisimama.

Mwaka 2011 nilipoajiriwa kama afisa wa Idara ya Siasa na uhusiano wa kimataifa CCM makao makuu sikuficha kuwa nakuunga mkono,Jambo ambalo limenitesa kisiasa mpaka leo lakini kwangu huu ni ushindi.

Kwakuwa Rais wa wakati huo na familia take walikuwa wakiunga mkono juhudi za Bernard Kamilius Membe kuwa Rais sisi tuliokuwa tukikuunga mkono tulikuwa tukipoteza kila kitu hata teuzi lakini hicho hakikutuzuia kukupigania kwani ndani ya CCM hakukuwa na kiongozi wa sampuli yako,naam tulipita kwenye moto mkali Sana na wakati fulani ilibidi tuishi Kwa tahadhari kubwa kwani tulikuwa kwenye blacklist.

Waliamua kukuchafua kupitia scandal ya Richmond ili mradi ujiuzuru Kwa kashfa ya ufisadi kwani ulikuwa tishio kwenye urais mwaka 2015.

Nilikuunga mkono katika mbio za urais mwaka 2015 na hata ulipohamia Chadema niliumia zaidi kwani nilijua huwezi kutangazwa mshindi kupitia upinzani.

Mungu aliyeumba Mbingu na Nchi anajua zaidi na akili zake hazichunguziki lakini naamini hakika kuwa wale waliokusaliti na watakumbwa na mabalaa na zahama kubwa.

Pumzika kwa Amani ENL.

Wakuu nimeikuta mahali
Ni Mimi Otieno Peter Baraka
 
Back
Top Bottom