MasterCard ya CRDB usumbufu mtupu

Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,204
626
Nimekua nikitumia card ya CRDB kufanya shopping online, wakati ule ilikua VISA card na nilikua nimeilink na Paypal, ilipoisha muda wake hawa jamaa wakanipa card ingine lakini hii card mpya ni MasterCard, sasa kila nikijaribu ku-link inakataa inasema maneno haya

This credit card has been denied by the bank that issued your credit card. For details on why your card was denied, please contact your credit card issuer's customer service department. Or, you may want to try adding a different credit card.

nimewapigia CRDB wanasema hakuna tatizo na card imesharuhusiwa kutransact online, tafadhali msaada kama kuna mtu anajua nini nifanye
 
Tafadhali tembelea tawi la crdb lilokaribu nawe au ulilochukulia hiyo card coz hii mastercard wanaifanyia apdated kila mara hivyo kuwapigia simu si sulihisho, dawa nikuwaendea tawini kwa msaada na uhakika zaidi. Mimi niko na account saba crdb na zote natumia kulipia mizigo inje ya nchi. Na kuna wakati zinagomaga na kunikasirisha ila nikiwaendea tawini tatizo linatatuliwa mara moja tofauti na kupiga 0714197700 halishugulikiwi haraka.
 
hilo ndio tatizo, hizi kadi zinatakiwa zipunguze usumbufu lakini badala yake hizi zinaongeza usumbufu
 
hilo ndio tatizo, hizi kadi zinatakiwa zipunguze usumbufu lakini badala yake hizi zinaongeza usumbufu

Wewe mwenye knowledge hiyo ndo unaona usumbufu ila angalia umma wa kitanzania na huu wizi wa internet. Assume umeibiwa hela zote kwenye credit card sijui ungewalalamikiaje crdb

Hizo card zinafungwa makusudi na crdb ili kuzuia zisiweze kufanya transaction ovyo na kusababisha wateja wao kuibiwa

Nafkiri kaongee nao waambie waifungue maisha wasiifunge
 
hivi karibuni nilikwenda crdb kuomba wanitengenezee mastercard waliniambia wamesitisha kuzitoa kwasababu zimekuwa zikiwasumbua watu wengi.
 
Ckia ww mkuu Master Card navyofahamu Hawajaanza Kuzi activate Master Card zao kwa hiyo ni kama pambo. Maybe cku hizi. Hiyo message ina maana Card namba yako ipo ila Benki haijakuunganisha kwenye huduma.
 
ckia ww mkuu master card navyofahamu hawajaanza kuzi activate master card zao kwa hiyo ni kama pambo. Maybe cku hizi. Hiyo message ina maana card namba yako ipo ila benki haijakuunganisha kwenye huduma.

duh......... Wapi tutapata hii huduma sasa?
 
walipotaka kunibadilishia wanipe Mastercard nikagoma, nademand ka-visa kangu ambako mpaka sasa sijaona usumbufu wowote!
 
Wakuu namimi naomba nitoe mchango wangu kuhusu MasterCard toka CRDB Bank. Nina watu wa karibu kabisa ambao ni staffs wa crdb. Kwa ujumla performance ya master card ya crdb ukilinganisha na visa card ya crdb kwa kipindi cha miezi kadha iliyopita imekua na matatizo ya hapa na pale. Kwa ufupi transaction failure cases kwa master card ni nyingi ukilinganisha na visa card, lakini tuzingatie kwamba hawana muda mrefu toka wameanza kutoa master card ukilinganisha na visa card, kwahiyo inawezekana baada ya muda fulani matatizo haya yakapungua kwa kiasi kikubwa. Suala la kufanya manunuzi online kupitia master card ya crdb limekuwa enabled si zaidi ya miezi miwili iliyopita. Hii inamaanisha miezi hiyo ya nyuma toka walipoanza kutoa hii master card, ulikua huwezi kufanya online purchases hata ungeenda kuwaona wangekujibu kwa sasa master card hazina hiyo facility.

Kwa upande mwingine, crdb wanatoa kadi zote mbili yaani visa au master, kwahiyo chaguo ni lako.
 
yep unasema kweli,ili kuondoa matatizo yote ni bora m2 uombe VISA card.
 
Mimi natumia Master card yangu kama kitambulisho kuchukua na kuweka pesa CRDB mambo ya transaction kwingine napeleka kwa mkono...acha niwe mshamba ila sitaki kuwa chakula ya ITs
 
Samahanini kwa kuingilia thread katikati..hivi nitatumia njia gani kurecover pesa yangu paypal (ambayo imekuwa linked na VISA card ya CRDB) baada ya cancelation ya transaction? maana nikienda kwa paypal account yangu salio ni 0 wakati pesa ilishakatwa ila kurudi kwa account haijarudishwa?. Sasa hii mambo inakueje? hiyo ela ipo wapi maana kwenye account ya paypal haipo wala CRDB haipo!
 
Nilikuwa napata the same message badae nikaenda CRDB

Paxman: nikawaambia naomba ku-activate account yangu iwe inafanya online transactions.
CRDB: Online transactions ndo nini?

Paxman: hahahah! ni huduma za kunua bidhaa au kufanya malipo kwa njia ya mtandao
CRDB: ok unatumia Visa card au Master Card?

Paxman: Ninatumia ile inanoyonipa fursa ya kuoa
CRDB: We mteja kiboko, tuone kadi yako!

Paxman: lol... hii hapa.
CRDB: Tanzania wateja wa huduma hizi ni wachache sana, ili upate huduma tunahitaji ujaze fomu hii na ujue kila
utakatwa TZS: 1000

Paxman: Sawa nipe fomu
CRDB: OK. Jaza iache hapa

Paxman: hakuna neno.
CRDB: Una tatizo lingine?

Paxman: Labda hapo badae kwa sasa nina ratiba tofauti baada ya kushughulikia hili...
CRDB: Heee! Kijana nenda Asante kwa kutumia huduma zetu.

Baada ya siku moja nikarudi paypal na kukuta ile message haipo tena badala yake kuna PIN wanazi genarate baada ya kukutaka USD: 1.9' hivi unatakiwa ukaombe bank statement ili uipate hiyo PIN then utaijaza hapo paypal after all Card yako inakuwa tayali linked.

Hitimisho: Card ya Master haina tatizo as you stated instead you have to go and ask the service to the Bank. Kwa usalama na ubora wa huduma imekaa njema ili mtu wa mwingine au mwizi asije link kadi yako.

mi nimeenda tawini jana tu, hawakuniambia kulipia wala nini...wamenipa form wakasema kesho yaani leo itakuwa tayari...ila mpaka sasa nimejaribu naona hamna kitu...
 
Samahanini kwa kuingilia thread katikati..hivi nitatumia njia gani kurecover pesa yangu paypal (ambayo imekuwa linked na VISA card ya CRDB) baada ya cancelation ya transaction? maana nikienda kwa paypal account yangu salio ni 0 wakati pesa ilishakatwa ila kurudi kwa account haijarudishwa?. Sasa hii mambo inakueje? hiyo ela ipo wapi maana kwenye account ya paypal haipo wala CRDB haipo!

pesa inatakiwa irudishwe kwenye account yako, kama haijarudi bado, print ile reversal transaction afu andika barua crdb attach hiyo kitu, address kwa reconciliation unit ya crdb, baada ya siku mbili tatu itakua imerudi
 
Nimekua nikitumia card ya CRDB kufanya shopping online, wakati ule ilikua VISA card na nilikua nimeilink na Paypal, ilipoisha muda wake hawa jamaa wakanipa card ingine lakini hii card mpya ni MasterCard, sasa kila nikijaribu ku-link inakataa inasema maneno haya

This credit card has been denied by the bank that issued your credit card. For details on why your card was denied, please contact your credit card issuer's customer service department. Or, you may want to try adding a different credit card.

nimewapigia CRDB wanasema hakuna tatizo na card imesharuhusiwa kutransact online, tafadhali msaada kama kuna mtu anajua nini nifanye

Hapa kwenye red, kama hukujaza form ya kuomba iruhusiwe ku-transact online ni kwamba pamoja na maelezo yao bado nakushauri urudi tawini ulikochukulia hiyo kadi, ujaze hiyo form na wakisha-activate basi utapata
huduma kwenye paypal yako bila shida. Sidhani kama kadi inakuwa tayari ku-transact online bila consent yako wewe unayeitumia.

Mimi natumia MasterCard yangu kwenye account yangu ya PayPal bila shida na kwa kweni ninaifurahia
 
Back
Top Bottom