WanaJF
Nilikuwa mmojawapo wa viongozi tulioandamana na Mhe Rais katika ziara yake ya majuzi nchini Singapore. Ninawaletea sehemu ya Master Plan ya mji wao mpya unaojengwa kutokana na kuokoa ardhi baharini (reclamation). Unaona kila kipande cha ardhi mpya kimeshapangiwa matumizi yake na kuwekewa malengo ya majengo yanayotakiwa.
Kupanga ni kuchagua. Kunahitaji nidhamu na hakuna mchezo wala utani. Huwezi kuwa na mji uliopangwa kama unapenda na kuendekeza uholela na vurugu (chaos). Kinachotakiwa ni kushirikisha wadau wote kupanga malengo na viwango baada ya kupata maoni ya wataalam. Wanaoarithirika na kulazimisha kuhama kupisha maendelezo mapya wanalipw fidia stahiki na endelevu.
Anayedai vinginevyo si msema kweli. WaSingapore wamehaidi kutusaidia katika ujenzi wa Mji Mpya wa Kigamboni. Ninakaribisha maoni yenu hasa nyie mlio nje na mnaishi katika miji iliyopangwa? Je uholela unavumiliwa au kuendekezwa? Tupe habari.
View attachment 97055
Mama Tibaijuka
mkuu soma vizuri nadhani hujaelewa hapa "WaSingapore wamehaidi kutusaidia katika ujenzi wa Mji Mpya wa Kigamboni"
siyo kuchora master plan, sasa ni kuanza ujenzi
Ndio maana nashangaa, why land reclamation in Tanzania ambapo tuna ardhi ambayo wala hatujai-utilise kabisa?
Kama hii ilitokea kama 'by the way', kwa nini aripoti by 'the ways' aache ya msingi yaliyowapeleka?
Ageleta taarifa ya kilichowapeleka na walicho-achieve ningeona mantiki labda.
Land reclamation inafanyika kwenye Maji (Bahari/Ziwa), that obviously kwa DSM inaweza ikawa Posta to Osterbay labda mpaka Kunduchi au Ununio. Nina uhakika hapa wame-target zaidi Posta, na ni kulekule kuendekeza ulimbukeni kwamba majengo marefu lazima yakae Posta.
Kama ndivyo basi tumekwisha maana kama kwa majengo yaliyopo Posta sasa, watu wanaamka saa 10 alfajiri na kufika ofisini Saa 3 asubuhi basi wakifanya hiyo reclamation yao watu watakua wanafika saa tano ofisini.
E mungu tunusuru!!
Mama kwanza shikamoo
Pili nimefarijika sana kwamba nawewe ni mwanachama mwenzetu wa JF
Tatu ni kwa wewe kutambua kwamba ndani ya JF utapata elimu, maarifa, maoni na mengi mengineyo
Nne na mwisho ni masikitiko yangu kwamba umeitupa hii post yako, nimesoma ukurasa kwa ukurasa, post kwa post lakini sijaona majibu yako. Au pengine nia yako hasa ilikuwa ni kupata maoni tuu?
Nikutakie siku njema mama yetu
Respect !!!
zomba kama huyu mama yupo serious ahakikishe NHC wanauza hisa DSE
wakusanye mtaji wa kufa mtu wajenge nyumba za kuuza na kupangisha tele
...Tukishindwa kuwaondoa 2015 hivi hatuwezi kumuazima Kagame kwa miaka michache tu? mbona makocha tunawanunua kwa gharama yoyote wakati tatizo letu kubwa nchini ni uongozi wa juu - Rais na mawaziri?Mama Tibaijuka, hongera kwa kujianika jamvini. Kwa uzoefu wako, ukiwa chuoni, WAMATA, Habitat na sasa Waziri, nilitegemea kabla ya kuwakilisha hoja yako basi ungewatumia wasaidizi wako na kujiridhisha kwa sana kabla ya kupost. Hiyo post yako ni sawa sawa na kuweka chumvi kwenye kidonda. Nikuambie kati ya wizara mbovu kiutendaji, kukosa weledi, uzalendo, kujawa na ubinafsi, na kuchangia kuiangusha kwa kila hali nchi yetu ni wizara yako. Sikutegemea kweli ungeweza kuibuka na kusingle out ka issue kadogo kwa taifa ukitegemea sympathy. Forget. Nikuambie, mimi ni mtumishi wa serikali ambaye karibu naelekea kustaafu maeneo ya Arusha. Nikuambie sasa nimeanza kuomba kupata kiwanja ili nijenge makazi yangu tangia 1996. Sijawahi kupata. Utasikia vimepimwa tena kidogo, lakini unakuja ona majina au kuambiwa wakubwa wamegawana or zoezi la upimaji limesimamishwa. Ni migogoro juu ya migogoro or ulipie mara mia. Huwezi kuniletea hadithi zako leo nikusifie wakati vitu vidogo na vya msingi kabisa katika mipango miji ni kugawa surveyed lands vinawashinda. Siwezi.
Sasa niseme, unaweza kuwa unania njema, lakini haitatekelezeka kwa sababu UWEZO HUNA. Serikali yako inayoongozwa na chama chako hawana uwezo huo kwa sababu. 1. Nyie nyote hamna vipa umbele. 2, Hamsimamii sheria zilizopo ambazo ni nzuri tuu. 3. Hamna mipango endelevu. 4. Suala lote la ardhi limezingirwa na Rushwa, Ubinafsi, Kujuana na akili ndogo isiyo na uzalendo kusimamia. Aliingiaga Magufuli wakati Fulani. Kulikuwa na impact japo naye hakukaaa. Sijui aligusa pabaya! Angalau alijaribu kutaka kurudisha nidhamu, kusimamia taratibu zilizopo, uwajibikaji nk.
Matatizo yote haya yamefanya serikali na nyie kina Tibaijuka kufikia mahali mnakuwa na narrow vision badala ya kuwa pana, mnafocus kwenye vitu vidogo, badala ya kitaifa, Waziri huwezi kujitapa na Kigamboni, wakati kila dakika li-squatter linazaliwa kwenye miji yetu. Mmegota, ni kama engine inayosumbua kila mara. Ukienda kwa fundi atakushauri very simple kuwa inahitaji overhaul. Ndicho kilichobaki. Muondoke waje wengine, or nchi ipate RAIS DIKTETA MZALENDO ambaye atakuwa anauliza maswali kama UTARATIBU UNASEMAJE? KWA NINI HAUKUFUATWA? BASI UFUATWE NA NIPEWE RIPORT YA UTEKELEZAJI BAADA YA SIKU SABA.
Mmetuharibia sana nchi yetu.
...Mkuu Zomba kumbe na ninyi huwa mnafikiria kama sisi wa CHADEMA? yaani nimeshangaa!NHC hawatoweza kusimamia, ingekuwa ni shirika binafsi, hizo kodi wanazokusanya na assets za majumba waliokuwa nayo hawana hata sababu ya kukusanya mtaji, wana mtaji tosha kabisa. Lakini wamekalia pale kujineemesha wao tu.