Master J na Shaa wamwagana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Master J na Shaa wamwagana

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Binti Magufuli, Jun 5, 2012.

 1. Binti Magufuli

  Binti Magufuli JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 7,455
  Likes Received: 755
  Trophy Points: 280
  source global publishers

  WAPENZI masupastaa ambao iliwahi kuelezwa kwamba wanapendana sana, Joachim Kimaryo ‘Master Jay’ na Sarah Kaisi ‘Shaa’, wanadaiwa kumwagana rasmi.
  Chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa tofauti za kimapenzi kati ya Jay na Shaa, zimesababisha mpaka kuyumba kwa uhusiano wao wa kikazi ambao walikuwa nao kwa muda mrefu.
  Tangu Shaa alipoibuka kimuziki na baadaye alipojitenga na Kundi la Coca Cola Pop Star, alikuwa akisimamiwa kimuziki na Jay kwenye lebo yake ya MJ Records.
  Habari kutoka kwa chanzo chetu, zimedai kuwa baada ya kugombana na Jay, sasa hivi Shaa amehamia kwenye menejimenti mpya chini ya Meneja wa Kundi la Tip Top Connection, Hamis Taletale ‘Babu Tale’.
  “Hivi sasa kazi zote za muziki, Shaa anafanya chini ya Babu Tale. Kweli mapenzi ni mchezo wa ajabu, wapendanao wanaweza kuwa maadui,” kilisema chanzo chetu.
  Shaa hakupatikana kufafanua hilo, lakini Jay alisema: “Sina tofauti yoyote na Shaa na sijagombana naye. Uhusiano wetu upo vizuri ila nimemruhusu asimamiwe na Tale kwa sababu nahitaji apate usimamizi na uangalizi wa karibu zaidi.
  “Mambo mengine nitaendelea kumfanyia, ila umeneja ndiyo nimeamua kumuachia Tale, nikiamini sasa Shaa atakuwa vizuri sokoni. Tale anaweza kumsimamia vizuri.”
  Babu Tale alipopatikana kuzungumzia kuhusu kuanza kumsimamia Shaa, alikiri na kuongeza: “Hapa ieleweke kuwa Shaa hatakuwa Tip Top, nitamsimamia kimuziki kama msanii wa kujitegemea.”
  Alipoulizwa kuhusu yeye kuwa chanzo cha ugomvi kati ya Shaa na Jay, Tale alijibu: “Hapana, hiyo haipo kabisa. Mimi namsimamia kimuziki tu, nachojua kuhusu Shaa na Master Jay bado ni wapenzi na wanapendana sana lakini siwezi kuzungumza kiundani kwa sababu hayo ni mambo yao binafsi.”
   
 2. k

  kiparah JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2012
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,176
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Si kweli!
   
 3. The_Emperor

  The_Emperor JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 884
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Master J si ana mke jamani?Ina maana Shaa ameingilia ndoa ya watu!
   
 4. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,721
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Hv mj si ana mke na harusi yake si nasikia pfunk ndo alikuwa best man au? Huy mj atakuwa amezuzuliwa na machokumchuzi a.k..a makengeza ya shaa au ni nini tena mwana wane. We kimario njoo utupe ukweli chalii angu aisee.
  Sent from Siemens C25 using Jamiiforum
   
 5. aye

  aye JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,987
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 160
  uyu jamaa wife wake yupo south afrika na ana watoto wakubwa sasa kabisa
   
 6. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #6
  Jun 5, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,740
  Trophy Points: 280
  hii ndio imekuwa staili humu jf kutaja aina za simu mnazo tumia, hii tabia kaileta pepizo.
   
 7. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,721
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  mkuu sio sisi ni mobile application ya jf
  Sent from my Siemens C25 using JamiiForums
   
 8. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #8
  Jun 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Acha chai wewe Siemens C25 hata GPRS haina!!!
  Sent from Nokia 3210 using Jamiiforums
   
 9. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  hahahaaaaa!!!! ase umemshtukia anatufunga kamba eeehhh!!!
   
 10. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,286
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  haaah haya siku hz siemens mwanga wa njano kumbe zina net?


  --->>>sent from nokia torch using the bluetooth
   
 11. mojoki

  mojoki JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 1,333
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  hahaaaa hatari lakini salama, Kamba ndefuuu nimeistukia  sent from my blackbeli not mine ofcoz nimegongea kwa mshikaji
  [
   
 12. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #12
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,286
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Wewe mojoki ndio yule wa MIG33..???  ---->>> sent from nokia torch using the bluetooth
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. m

  mbezibeach 2 Senior Member

  #13
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 166
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nadhani mleta thread ameilisha maneno thread yake...

  MJ:mambo mengine nitaendelea kumfanyia..
  BT:back wanapendana.
   
 14. ney kush

  ney kush JF-Expert Member

  #14
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 1,195
  Likes Received: 377
  Trophy Points: 180
  teh teh ngoja niprove
   
 15. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,069
  Likes Received: 7,281
  Trophy Points: 280
  Master J hamli Shaa
  ---->>> sent from Nokia Ringo (mshindi) using the infrared
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Jun 8, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  ha ha ha aaahah!! Mwelekeo wa thread umehamia kwenye simu....
   
 17. Jeji

  Jeji JF-Expert Member

  #17
  Jun 8, 2012
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  hiyo ya C25 imenichekesha sana.
   
 18. ummu kulthum

  ummu kulthum JF-Expert Member

  #18
  Jun 9, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 2,791
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  du c25 hata bibi angu hatumii
   
 19. gbrother

  gbrother JF-Expert Member

  #19
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hii sasa ni noma,
  ki2 cha tochi?

   
 20. c

  chante Senior Member

  #20
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  chante and two others like this.
   
Loading...