Mastaa wamchana vibaya diamond kisa misiba

Mastaa wamchana vibaya diamond kisa misiba

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
19,899
Reaction score
37,699
IMEKULA kwake!

Wasanii wa sinema na Bongo Fleva wamemchana vibaya staa wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond' kwamba si mtokaji kwenye misiba ya wenzake.Wakizungumza na Amani kwenye maziko ya baba mzazi wa Mbongo Fleva, Abdul Sykes ‘Dully Sykes', Ebby Sykes,

Jumatatu iliyopita, wasanii hao walioomba majina yao yalindwe walisema kumbukumbu za vichwani mwao zinaonesha kuwa, Diamond amekuwa akichagua misiba ya kujitokeza hasa ile ambayo itampa ‘kavareji' kwenye vyombo vya habari.

"Mimi nakumbuka wakati wa kifo cha Kanumba (Steven), Diamond alitokea kwa sababu ulikuwa msiba mkubwa sana na kweli alipata kavareji ya kutosha kwenye media.


"Halafu akaonekana tena kwenye msiba wa baba yake Wema Sepetu, nadhani kwa vile alikuwa mtu wake Wema wakati huo asingeacha kwenda. Lakini baada ya hapo sikumbuki," alisema msanii mmoja.


Msanii mwingine aliongeza: "Halafu Diamond na Dully ni washikaji, sasa jamaa tunasikia yuko Zenji tu hapo anakula bata na Zari (Zarina Hassan) lakini ameshindwa kuja Dar kumzika baba mzazi wa mshikaji wake."

Blogu ya Wananchi
 
Wabongo Waajabu, nilisha wahis ema Misibani watu huenda kuchunguzana kwamba nani kaja na nani hakuja, Misibani wenye uchungu ni wale wafiwa tena wa karibu sana wengine hakuna kitu, that is why mimi napendsana misiba ya wazungu, ni ishu ya kifamilia na si ishu ya jumuia.

Na msibani si lazima mtu aende na unae enda kama kweli umeguswa na msiba huo muda wa kuuliza fulani mbona simuoni unatoka wapi? Misibani kwa Bongo ndo sehemu ya kwenda kubishana kuhusu mpiria, siasa,
 
Tuanze utaratibu wa wenzetu.. Msiba hadi mualiko.. Haukuhusu uendelee na mía zako...
 
Hata mimi napenda sana misiba ya wazungu, eeeh!!! Wafe tu!!
 
kila mtu anaratiba zake mjini,sio kila mtu anaweza fika kwenye msiba wa mwenzake.
 
Watu wote waliofika hawana maana bila Diamond kufika? Yaani mtu yupo Zanzibar aache shughuli zake aje Dar kwenye msiba ambao hata sio wa ndugu yake. Kwani msiba unaisha siku moja? Watu si wanaruhusiwa kwenda kutoa pole/kuhani msiba hata baada ya maziko?
 
Hoja Zao Hazina Mashiko Na WAMEFILISIKA KIAKILI na KIFIKRA.

Hivi Kwenda Msibani Kuna Kulazimishana au Kupangiana? Waulize Hata Wao Wenyewe Tu Kuwa Je Ni Misiba Mingapi Ya Ndugu Zao Wa Damu Hawajahudhuria? Watanzania Hebu Tuacheni UNAFIKI Na Kupoteza Muda Kwa Mambo Ya Kipuuzi Namna Hii. Mimi Siyo Mshabiki Wa Diamond ILA Ktk Hili Namtetea Kwa 100%.

Hivi Kama Kipindi Hiki Cha Msiba Labda Hakuwa Nchini Na Hata Kama Alikuwa Nchini Je Wewe Unajua Ratiba Za Watu Na Mipangilio Yao Kimaisha?

Hata Hao Hao Waliotoa Malalamiko Hayo Na Wao Wameenda Ktk Huo Msiba Wa Baba Yake Dully Kuwakilisha Tu Kwa Kujionyesha Mavazi, Cheni Zao Na Vijigari Vyao Uchwara. Kama Kweli Nyie Ni Watu Wa Misiba Mbona Sisi Wapenda Soka Hatujawaoneni Katika Ule Msiba Wa Mafisango Na Hata Tu Huu Wa Juzi Wa Mdogo Wake Julio Hapo Kigogo?

Lakini Sisi Mashabiki Wa Soka Ni Kama Chumvi Vile Kote Kote Tupo Na Hatubagui Na Wengi Wetu Ndiyo Huwa Tunajaza Sana Shazi Misiba Yenu Huku Tukilia Kiuchungu Japo Misosi Huwa Mnatutolea Mbavuni Na Kula Wenyewe Ki Bongo Movie Na Ki Bongo Flavor.
 
Huu ni ujinga.

Mbona rais alikwenda wa kanumba lakini huo hakwenda/

Mbona mimi hamjanianzishia thredi, na si kwenda?

Kama mnamwombea apate msiba ili msiende, imekula kwenu, kwani rais atahudhuria, sasa nyie na rais wa nchi nani ni takataka?
 
Hii ni dalili mojawapo ya kuwa kazi inaelekea kuwashinda
 
Back
Top Bottom