Mastaa wa bongo: JK amwita Diamond ikulu

Status
Not open for further replies.
Mkuu Zomba kweli wewe ni wa ajabu saana, kazi alizozifanya Nyerere unaweza kuzifananisha na huu mdundiko unaoendelea hivi sasa???? Kama hujui au labda una issue ya kumchafua Marehemu Mzee wetu Nyerere basi huna sera kalale!!!


Kazi zipi za maana za kuuwa nchi na kupeleka wacheza ngoma Japan?
La Mzee Morris ni sifa la Diamond sifa mbaya. What a way of thinking.

Niambie ni kipi hapo nilichokisema kwenye nyuzi ambacho si kweli?
 
Bora useme wewe kuliko tukisema sisi tutaambiwa hao cdm kawaida yao, pole sana kwa kuwa na mwenyekiti promoter!

Asante sana kwa taarifa muhimu ngoja tufanye kazi ya kumshauri mwenye kiti wako.
 
Rais aliyezoea kula bata hata kabla ya kuingia ikulu.huyu si alikuwa anapiga modal za jeans tangu akiwa waziri? Nakumbuka mwaka 2000 aliwahi kuja Pugu sec amepiga modal na shati la kisharobeeeng

bushjeans-2.jpg


nyerere13bc.jpg


article-2005728-0CA3F65100000578-317_634x809.jpg


jk2.jpg
 
Kazi zipi za maana za kuuwa nchi na kupeleka wacheza ngoma Japan?
La Mzee Morris ni sifa la Diamond sifa mbaya. What a way of thinking.

Niambie ni kipi hapo nilichokisema kwenye nyuzi ambacho si kweli?
Priii! Priii!!!! Prii!!! Promota anabeep!!!!!
 
Wote mnazunguka porini tu kutaka kulaumu na kutafuta mchawi, maraisi wetu wote wa Tanzania ndio kioo chetu sisi Watanzania kama jamii jinsi tulivyo, hayo aliyofanya Kikwete au sijui Mwinyi au Mkapa hayana tofauti na yale tunayoyapa kipaumbele kila siku katika jamii zetu kama michango ya harusi badala ya kujenga shule, kushinda baa badala kuwa na familia nyumbani, sehemu kubwa ya posti za JF ni kuhusu mambo ya ngono tu hakuna jingine!

Kila mtu anategemea fulani ndio amfanyie yeye kitu fulani bila ya yeye kutaka kujitolea kwanza, Madaktari wako tayari kuacha watu wafe ili kuikomoa/kuishinikiza Serikali, wakati jamii nyingine hata madaktari wanagoma lakini kuna wanaojitolea kutibu watu wasio na hatia hata mitaani tu bila malipo,

Walimu hivyo hivyo wako tayari kuwasusa wanafunzi kushinikiza Serikali wakati jamii nyingine hata kama wakigoma kuna wanaojitolea kufundisha hata bila malipo ili tu wamsaidie mtoto wa maskini, watu wanafurahia na wanashinikiza sensa isifanikiwe wakifikri wanamkomoa Kikwete na CCM kumbe pesa inayopotea ni ya kwake yeye anayefanya kazi masaa 10 / siku na kukatwa kodi na si Kikwete, na ukitaka kuamini hicho hapa tunakutana kila siku kujadili matatizo ya Serikali lakini sio suluhisho,

Leo hii hapa ukisema tunaanzisha mfuko wa kutaka kununua madawati kwa watoto na wadogo zetu walewale wanaolialia kulaumu serikali ndio watakuwa wa kwanza kufanya kila kitu ili tu mfuko usifanikiwe kwa kuja na propaganda kibao, lakini anzisha kitu kama party ya JF kila weekend cocobeach uone thread itakavyo jaa watu kutaka kupata info zaidi kuhusu hiyo party!

Mifano ipo mingi sana na majibu ya kwa nini tuko hapa tulipo na wala hatuna wa kulaumu si cha Kikwete wala CCM isipokuwa ni sisi na jamii yetu, ni mpaka hapo tutakapo tambua hilo na kuamua kubadilika kama jamii ndipo tutakapoweza kuungana na jamii zingine Duniani kama "equal partners" kinyume cha hapo tutabaki tu kama alivyosema mchangiaji mmoja kutuma watu wakacheze sindimba Ulaya wakati wao wanatuletea mavitu kutuuzia kutafuta mchawi mara Kikwete mara Mkapa n.k
 
HonorableMP

Hoja yako imejaa itikadi, Diamond ni msanii maarufu nchini, na umaarufu wake unaweza kutumika kimataifa kuitangaza nchi kiutalii ni rasilimali zilizopo na hatimae kukuza sekta ya utalii na uwekezaji, pia Ikulu sio ya mtu binafasi, kila mwananchi anaweza kwenda kuonana na rais wake kwa issue binafsi, hata za nchi, sasa mnachoona cha ajabu kipi? Mheshimiwa Rais wapotezee hao ni wivu tu wa kwenda ikulu unawawasha na hawapagusi milele.
 
Last edited by a moderator:
Ndio uzuri wa kuwa na Rais limbukeni akiwa amezungukwa na limbukeni wenzake. Ulimbukeni haumaliziki kwa shule au masomo ya darasani. When you are one, you stay one and no amount of education can change you. He gets paralyzed in-front of a white man and feels all Tanzanians are too stupid to see this.

Waliompigia kura wajifunze sasa. Miaka mitano ya kipindi cha kwanza tuliona jinsi ambavyo alitunza ahadi zake na tukamzawadia mingine mitano ili aweze kutumalizia raslimali zilizosalia. Learn from it.
Hapo kwenye RED hiyo mitano ya sasa alizawadiwa na tume sio watanzania kwani uchaguzi wa 2010 hakushinda.
 
aah JK lini utabadilika? Au ndo you cant teach old dog new tricks! Kweli umekuja kutuumiza wa tz.
 
Mimi sioni tatizo lolote kwa Rais kumuita huyo msanii ikulu. kwasababu wote wako kwenye chama kimoja cha ma FM
wote wanajuana hao. ila tuiombee nchi yetu tupate hekima yakumchagua Raisi atakae livusha taifa kutoka katika hali mbaya ya umasikini nakutuweka kwenye hali Bora. hapo tunamuhitaji Mungu sana
 
HonorableMP

Umelipwa shiling ngapi? maana bandiko lako la leo mtaa wa UFIPA lazma utemeee teh teh haya changanya miguu mtaa wa UFIPA kachukue chako
 
Last edited by a moderator:
Honorable MP, kweli umekomaa si kisiasa tu, bali hata kijamii na inaonekana umekerwa sana na tabia za "mwenyekiti". Kwa habari hii uliyoiandika imenichefua zaidi,,,,nahisi kutapika hata hii breakfast yangu....

Anyway, Rais ni dhaifu kuliko chama anachokiongoza.
 
Kwa hiyo Rais anatakiwa kudeal na maprofesa tu? Wanamuziki hawatakiwi Ikulu!!! Nimeona watu mnalalamika hata kitendo cha Rais kushirikia mazishi ya Kanumba. Kumbukeni kuwa Urais haumfanyi mtu aache kuwa binadamu wa kawaida. Mmenikumbusha wafanyakazi wa White house ya Marekani wanavyomlalamikia Michelle Obama kuwa tangu ameingia Ikulu kuna wageni wa hali ya chini wengi wanakuja, wakati wamezoea kuona White hause wanaalikwa "watu bora".

Huyo Loveness kama kila kitu alichowaambia mmemwamini hamuwezi kuweka lawama kwa JK. Ni jukumu lenu wenyewe kutafuta ukweli.

Ili kufahamu zaidi tamaduni za kualika watu mbalimbali Ikulu za nchi mbalimbali tazama hapa:
Barack Obama Invites Damian Lewis, Idris Elba To White House Dinner For David Cameron (VIDEO, PHOTOS)

Michelle Obama invites TV host Jimmy Fallon in for a White House gym session | Mail Online

Carla Bruni welcomes Russian president to state dinner in a daringly tight dress ~ Beauty Care

Angela Merkel would like to dine with Vicente del Bosque


Naongopa kulinganisha uwezo wa kiuongozi na kitawala kati ya JK Na Obama. JK=Obama=sio serious. Bush hajawahi kufanya kitu hicho. Angalia Jk anafanya appointment kukutana na Bekham Airport ili wa-shake hands. Is he serious?. Haya ndo Mluo anafanya huko US. Je anamuono wa mbali au anaangalia aliposimama tu. Je amekosa washauri katika chama na serikali yake. Hii ilitokea katika nchi moja Asia ambapo rais alihusishwa katka filamu katika TV na alifukuzwa. Hii inakuja kwa Tz kama hatuna umakini katika yale tunayofanya. Sijui nani anayemshauri katika masuala ya SOCIAL? ANAMPOTOSHA!!!!!

Kama ameshindwa ni heri aseme ili nchi iongozwe na wenye uchungu na nchi. Mimi niko tayari kumsaidia katika kufanya maamuzi ya kweli.

Kikubwa ahusishe ma-profs. katika vyuo vyetu maana wengi hawajahusishwa sana na vyama na wana akili chanya sana ukilinganisha watu wa siasa au aliokua nao huko Kimbiji au Kibondo.

Acha jazba.
 
Mkuu jmushi1 pole sana. Wengine toka jina lake linapendekezwa mwaka 2005, tuliwatahadharisha Watanzania juu ya hatari ya kufungua milango ya jehanum...mimi kwa mfano nilikosana na ndugu na marafiki kwa msimamo wangu huo. Namshukuru Mungu kwa kuwawezesha wengi kufunguka macho na kumwona huyu msanii katika rangi yake halisi na idadi yao yaongezeka siku hadi siku. Kupitia wizi, kwa mfano EPA, aliingia madarakani na tangu hapo mkono wake upo katika kila tendo la kihalifu nchini linalolindwa na serikali kuanzia wizi wa rasilimali za taifa hadi sasa wizi wa roho za Watanzania wasio na hatia. Of course wapo akina ZeMarcopolo! Watakosaje? Wanafiki, wajinga na walafi ndio mtaji wa CCM, ndio mtaji wa Kikwete na ndio mtaji wa Mafisadi.
554627_10151028077040825_1456805117_n.jpg

Apple = CHADEMA
Samsung = CCM
Nokia = CUF
 
Kwa hiyo Rais wa Tanzania kumtafutia mtanzania deal ni tatizo?!
Rais anavyoongozana na wawakilishi wa makampuni mbalimbali kwenye DICOTA na kwengineko hamuoni inafaa? au NSSF na Exim bank peke yao ndio wana haki ya kutafutiwa deal na Kikwete?

Tatizo deal lenyewe kamtafutia ndani ya CCM na pesa za walala hoi ndizo atakazo tumia huyo msanii ndo tatizo lilipo we mwenzetu huoni tatizo kwa sababu upo kwenye system ya ulafi ndani ya CCM
 
Hata Andry Rajoelina, yule dogo wa Madagascar aliyekuwa Disco Joker (DJ) kwenye kumbi mbalimbali za starehe hawezi fanya kitu kama hiki kwani CV yake imepanda................."Inabidi Mwenyekiti ajitambue"
 
Kikwete na CCM wanaliaibisha Taifa. Anatumia ikulu vibaya.

Iweje Rais atumwe na Mwanamke, ambaye siye mkewe kumuita msanii kwenda Marekani?....Ikulu ni taasisi takatifu katika nchi. Ni taasisi inayostahili heshima zote. Ikulu yetu imegeuka kuwa pango la walanguzi, wanyang'anyi, wauaji wa Mabwepande, mapromoter, na wapokea suti. Ikulu imegeuka kuwa sehemu ya kuuzia rasilimali zetu n.k. Mbona taasisi ya Rais imeshuka hadhi kiasi hiki?


Hon: Member of Parliament (CCM)

Mh Mbunge;
Sijakusoma vizuri;
Katumwa kaombwa? Mwanamke siyo binadamu? Au siyo Mtanzania? Ingekuwa mwamnamme je, ingekuwa sawa kulingana na hoja yako? Kisa hapa ni kwa sababu huyu ni mwanamke?

Diamond anaangukaje kwenye hayo makundi uliyoyataja? Nadhani huyu kijana hujamtendea haki kulalamikia mwaliko wake. After all ni kijana ambaye anajitafutia kipato chake halali na amejizolea sifa kimataifa kiasi kwamba anailetea sifa nchi yetu ndani na nje, kuna kosa gani akaenda akafanya hilo tumbuizo kwenye ufunguzi wa hilo tawi?

Hoja yako ingekuwa kwamba unalalamikia issue ya delegation perce hapo afadhali ningekuelewa kidogo.

Kwa nini wa-Tanzania tunachukiana na kujichukija hivi jamani? Shetani gani huyu?


 
Naomba kuchukua nafasi hii kumpongeza dr. dr. dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kazi yake ya u-promoter ni muda mrefu nimekuwa nikijiuliza kwanini raisi wangu anapenda sana kupiga picha na wasani mbalimbali pengine kuliko raisi yoyote duniani achilia mbali hapa kwetu Tanzania maana wengine mpaka wana maliza muda wa uongozi wao hatukuwahi kuwaona viwanjani, Ndipo jana nikiwa napitia pitia mtandao wa JF nikakuta ameamua kuiweka wazi kazi yake hiyo ambayo watanzania wengi pengine walikuwa hawaijui yaani ya u-promoter baada ya kuchukua jukumu hilo kumpeleka msanii Diamond huko majuu huku mkuu huyu akiingia gharama za safari hiyo ili akatoe burudani kwa wabongo waliko huko USA, Nikagundua kikwete kuna baadhi ya vitu hufanya kwa vitendo zaidi kuliko kuongea ongea sana kama hili la kusafiri iko siku nalo ataliweka wazi.
Kuna tetesi kuwa wewe ndiyo uliwezesha wasanii wakubwa kama akina 50cent, shaggy na wengine wengi walio wahi kuja hapa Tanzania kwa siku za karibuni ingawa huwa hupendi kujitangaza pia umeonyesha nia ya kuleta timu kubwa kabisa kutoka Hispania naikumbukwe ulifankisha kuileta timu ya Brazil..well done Kikwete
Ushauri wangu: Usijisumbue kuleta timu kubwa kutoka Hispania bali peleka vijana wetu wenye umri wa chini ya miaka 20 angalao 10 ukawaombee wakaa kwenye timu hizo hata kama ni kwa miaka 2 kuliko kutumia mabilioni matokeo yake faida ni dogo sana au hakuna kabisa.
 
Mkuu Ritz
Hawa mods ni wanazi wakiona vijana wao wamebanwa wanakimbilia kuiondoa topic; hili suala tumeliongelea jana mods wamekimbila kuifunga topic baada ya kuona vijana wao pro Chadema wamezidiwa sasa wanaurudisha upuuzi ule ule, wote tunajua mods ni pro Chadema ila tunawaomba kabla ya kuifunga topic ongeeni nyie pro Chadema mmkubaliane ili tusiwe tunarudi jambo moja kila siku. Mkuu Ritz waambie jamaa zako mods wanachemsha; hawa jamaa wananipa raha sana uwanja wao, refa wao lakini bado wanakimbilia kuzima taa mpira uishe!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom