Mastaa 10 waliolipwa fedha nyingi zadi duniani mwaka uliopita kwa mujibu wa jarida la Forbes

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Kwa miezi 12 iliyopita, mastaa 100 wanaolipwa fedha nyingi zaidi dunia waliingiza jumla ya Tsh trilioni 11 ikiwa ni fedha nyingi kuliko pato la taifa la nchi tatu za Belize, Liberia na Gambia zikichanganywa kwa pamoja.

Katika orodha hiyo ya mastaa 100 walioingiza fedha nyingi zaidi, inaongozwa na mwanamuziki kutoka nchini Marekani, Diddy ambaye pekee aliingiza jumla ya Tsh 291 bilioni ambapo anafuatiwa na Beyonce na J.K. Rowling ambao wanahitimisha tatu bora ya wenye mkwanja mrefu.

Orodha hiyo ya mastaa 100 imejumuisha watu kutoka tasnia mbalimbali kama vile utangazaji, uanamuziki, michezo mbalimbali lakini wanamuziki hasa kutokea Marekani wanaonekana kutawala katika mastaa 10 wa mwanzo.

Orodha hii imejumuisha kipato kilichoingizwa na staa husika kutokea Juni 1, 2016 hadi Juni 1, 2017. Fedha hizo ni kabla makato ya wanasheria, mameneja na mawakala wa mastaa hao.

Hapa chini tutaorodhesha mastaa 10 walioingiza mkwanja mrefu zaidi ikifuatiwa na fedha aliyoingiza na tasnia anayofanyia kazi pamoja na nchi atokayo staa huyo.

1. Diddy- $130 milioni (Tsh bilioni 291), Mwanamuziki nchini Marekani
2. Beyoncé- $105 milioni (Tsh bilioni 235), Mwanamuziki nchini Marekani
3. J.K. Rowling- $95 milioni (Tsh bilioni 213), Mwandishi nchini Uingereza
4. Drake- $94 milioni (Tsh bilioni 210), Mwanamuziki nchini Marekani
5. Cristiano Ronaldo- $93 milioni (Tsh bilioni 208), Mchezajii nchini Ureno
6. The Weeknd- $92 milioni (Tsh bilioni 206), Mwanamuziki nchini Canada
7. Howard Stern- $90 milioni (Tsh bilioni 203), Mtangazaji nchini Marekani
8. Coldplay- $88 miliioni (Tsh bilioni 196), Mwanamuziki nchini Uingereza
9. James Patterson- $87 milioni (Tsh bilioni 195), Mwanamuziki nchini Marekani
10. LeBron James- $86 milioni (Tsh bilioni 192), Mchezaji nchini Marekani.

Unaweza kuiona orodha yote kwa kutembelea tovuti ya Forbes ambayo ni www.forbes.com

forbes-highest-paid-celebrities.jpg

beyonce-1.jpg


498775218.jpg
 
Nimeona hiyo report baada ya Forbes kunitumia news alert kwenye email yangu.

Nimeangalia hiyo ripoti baada ya kukosa jina langu nikajua tu hii ripoti imepikwa na forbes ili kutafta kiki.

Najaribu kuwasiliana na mtaalam wa sheria za kimataifa ze nyoka mwenye makengeza nione kama naweza kuwashtaki forbes au kuwataka waniombe radhi kwa kutokujumuisha jina langu kwenye hiyo top ten yao.
 
Nadhani kwa Diddy ingekuwa mfanyabiashara na sio mwanamuziki, japo inawezekana hela zake nyingi zimetoka kwenye muziki.
 
80% of the world's wealth is earned by 20% of its people, the rest tutabaki watazamaji tu unless tuamue sasa kufanya kazi kama watumwa.
 
Daaaaah mamaeeee mnyama cr7 kashika tano boraaaa!

Niangalizieni yule dwarf mwenye ndevu kama mchicha pori yupo namba ngapi???

Cc PNC 1
 
daaaahhh vipaji vikisimamiwa vizur vinaingiza hela ndefu kuliko kazi yoyote hapa duniani......sema wazaz wa kiafrica hawajui hilo yn
 
Back
Top Bottom