Gazeti pendwa la Ijumaa linakuwa la kwanza kufichua siri kwamba wanawake waliokamatwa ndani ya kituo hicho kama wahudumu wa massage na ngono kwa mlango wa nyuma, ni wake za watu.
Funua funua ya wadaku wetu imebainisha kuwa wanawake hao wamekuwa wakijishughulisha na biashara hiyo bila waume zao kujua.
Gazeti la Risasi Mchanganyiko katika toleo lake la juzi (Jumatano) lilikuwa la kwanza kuandika habari ya kituo hicho chini ya kichwa: Aibu ya mwaka ambacho kilisindikizwa na maneno, Kituo cha vigogo kujivinjari kwa ngono chafumuliwa.
Katika habari hiyo, ilielezwa kuwa kulikuwa na biashara haramu ya ngono ndani ya Kituo cha Massage, kilichopo Kijitonyama, Dar es Salaam ambapo vigogo wa serikali, watumishi kwenye taasisi zinazolipa mishahara mikubwa na wafanyabiashara wenyenazo walifika mara kwa mara kupata huduma.
Liliandika kuwa baada ya kukamilisha uchunguzi wake, askari polisi wa Kituo cha Oysterbay kwa kushirikiana na waandishi wa habari, walikivamia kituo hicho na kuwafumania wahudumu wawili wakiwa uchi kama walivyozaliwa pamoja na wateja wawili, hivyo kutoa picha kuwa walikuwa kwenye harakati za kutenda ngono.
Baada ya kutoka kwa habari hiyo juzi, Ijumaa lilivujishiwa nyeti kuwa wanawake wawili waliokamatwa kituoni hapo ni wake za watu ambao wamekuwa wakijishughulisha kwa siri na kazi hiyo.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, wanawake hao (pichani), mmoja alikutwa uchi, mwingine akiwa amevaa, wote ni wake za watu ambapo wamekuwa wakijishughulisha na kazi hiyo pasipo waume zao kujua.
Katika unyetishaji huo, gazeti hili liliwekwa kweupe kwamba mwanamke mwingine aliyenaswa akiwa uchi na mteja chumbani, ni mchumba wa mtu na kwamba alimweleza mpenzi wake kuwa anafanyakazi saluni ya kike.
Ijumaa lilielezwa kuwa mwanamke anayeonekana kulia ukurasa wa kwanza anaitwa Lulu George na kwamba yupo kwenye ndoa na anaishi na mumewe Mbezi Tangibovu, Dar es Salaam kwa mwaka wa pili sasa.
Lilielezwa kuwa mwanamke anayeonekana kushoto ukurasa wa kwanza, yeye alikutwa uchi na kwamba jina lake ni Aisha, anaishi Tandika Mwembe Yanga, asili yake ni Mkoa wa Tanga na ana mchumba wake (jina tunaliminya).
Inaelezwa kuwa Aisha alijieleza kuwa anafanyakazi saluni ya kike wakati Lulu yeye alikuwa akimweleza mumewe kwamba ameajiriwa hotelini kama msimamizi wa wahudumu.
Mwanamke mwingine aliyenaswa kituoni hapo, anaonekana katika picha ndogo iliyozungushiwa duara ukurasa wa kwanza, naye imebainika kwamba ni mke wa mtu, ingawa hakukutwa uchi.
Gazeti hili lilimtuma paparazi Oysterbay Polisi kufuatilia maendeleo ya waliokamatwa katika ambushi hiyo ambapo alielezwa kwamba watuhumiwa wamepelekwa Mahakama ya Jiji kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Habari zaidi kutoka kwa chanzo chetu zinasema kuwa, waume wa akina dada hao walipopata taarifa za uchafu huo waliangua vilio kama watoto wadogo na kushindwa kufika polisi.
Ijumaa linalaani vikali biashara hiyo haramu na linaahidi kufuatilia sakata hilo katika Mahakama ya Jiji na kutoa maendeleo yake.
Chanzo: Global Publishers
My take: Hivi inawezekanaje ukaishi na mke wako na usifaham anapofanyiakazi, au akawa anakueleza nafanyakazi mahali flani na haujawahi fika?