Masoud Kipanya na Fina Mango wa Clouds FM

Status
Not open for further replies.
Yupo Gerald Hando na Paul James...wanaboa haooooooo!!!!! Afadhali kidogo Gerald ana kauzoefu ka kukaa na wale wawili lakini Paulo kama wanavyomuita! Mhhh! Safari pevu!

siyo kweli, mimi nimesikiliza power breakfast moja last week, it was fantastic, walikuwa wanaongelea mchungaji mtikila.

Jamani tusikimbilie kusema kwa kuwa moved na kitufulani, tuzungumze ukweli penye ukweli tutoe heko, pabaya kupige kelele. mimi nasema labda utaratibu wa kuwaachisha kazi haukuwa mzuri,otherwise, kipindi bado bomba. LAKINI pia jamini ukiwa kwenye kampuni ndogo za private unategemea kuachishwa vipi?????
 
Jamani msiumize vichwa, sehemu ya maelezo ya Kipanya haya hapa kama alivyoojiwa na Bongo Celebrity

"Mimi sikuacha kazi Clouds Fm kama inavyosemekana, mimi nimepewa barua ambayo inazungumzia ku-revoke (kutengua,kuahirisha) mkataba wangu na Clouds.Nitazungumzia sababu za kupewa barua hiyo, ila kabla sijaingia ndani zaidi, mwisho wa barua ile niliyopewa imesema, nainukuu, ‘we wish you all the best in your future endeavors’ mwisho wa kuinuukuu barua niliyopewa na HR Manager wa Clouds Media Group. kwa lugha rahisi ikimaanaisha tunakutakia kila la heri katika mahangaiko yako ya mbeleni.

Kwa mantiki hiyo labda wasomaji waniambie sijaielewa maana ya barua ile, lakini kwa kifupi nilichoelewa ni kwamba, kutokana na makosa niliyoyafanya, Clouds imeonelea kuwa sina sifa za kuendelea kuwa sehemu ya timu ya Clouds Fm. Sasa basi, hebu tuangalie makosa niliyoyafanya mimi pamoja na Fina.

Tarehe 29th May 2008, kwa pamoja, mimi na Fina tuliamua tusiingie kwenye kipindi kuonyesha kutoridhishwa na utendaji wa baadhi ya wenzetu. Kama kuna waliosikia, siku moja kabla yaani tarehe 28th May tulifanya mahojiano na Balozi wa Marekani nchini Tanzania.Bahati mbaya (kwa sababu ambazo zilikuwa ndani ya uwezo wa Technical Department) mahojiano yale hayakusikika vizuri, yalisikika vibaya mno!!! Na hata vifaa pia havikuwa timilifu, mfano mmoja mdogo tu ni kwamba tulikuwa tunatumia mic moja.Yaani watangazaji watatu na balozi, kwangu ilinipa wakati mgumu sana hasa ikizingatiwa taarifa za interview zilipatikana karibu wiki nzima.Nilitegemea wenzetu wangejiandaa kwa kila kitu. Kwa kifupi watu wa technical walikuwa na uwezo wa kusema kwamba interview isingewezekana kutokana na ufinyu wa signal na vifaa, TUNGEAHIRISHA.Makosa kama haya yamekuwa yakijirudiarudia mara kwa mara na ndio maana nasi tukaamua kuweka msisitizo kwa njia ile ya kugoma.

Najua kuna watakaojiuliza, hapa Gerald anaingia wapi, kwa sababu alisikika wakati wa mahojiano na balozi, akayapata madhira lakini hakugoma. Hilo sitolitolea maelezo nikiamini yeye mwenyewe ndiye mwenye nafasi nzuri ya kufafanua atakapotakiwa kufanya hivyo ingawa halazimiki. Ila ieleweke kwamba, kwenye mpango wa kugoma, ALIHUSISHWA NA AKAUKUBALI.

Kilichofuatia ni kutakiwa tujielezee kwa nini hatukwenda kwenye kipindi, tukajielezea, na hatimaye mimi nikapewa barua niliyoielezea hapo juu na tetesi za uhakika nilizo nazo ni kwamba mtu wa technical kapewa barua ya warning.

Kwa hiyo basi, kuondolewa kwangu hakuhusiani kabisa na suala la masilahi yaani mishahara. Kosa ni hilo hapo juu na tulilifanya kwa nia njema ya kujaribu kujenga zaidi kwa vile tunaamini Clouds inazidi kukua siku hadi siku.

Ni juu ya atakayesoma waraka huu kupima uzito wa kosa na uzito wa adhabu.Kwangu naona sawa kwa sababu si kila kinachotokea lazima kiwe na sababu za msingi. Bado mwenye mali ana mamlaka ya kuamua nani awe kwenye timu na nani asiwemo.Na ninaamini kila anayekosea lazima aadhibiwe,nami nimeadhibiwa na nimeheshimu. Maisha yanaendelea.

Namshukuru mungu na nawahakikishia wachache waliokuwa wakitusikiliza kwamba kamwe hatukuwahi kulewa sifa kwa sababu kama ni kulewa sifa tungeshagoma siku nyingi zilizopita kama suala lingekuwa ni mshahara. Kwa wenye kumbukumbu, Power Breakfast ilianza kama ‘wake up show’, enzi hizo kipindi kilikuwa kinaanza saa 11 alfajiri, maana yake ni kwamba mimi na Fina tulikuwa tunaamka saa 10 alfajiri, kwa mshahara wa kawaida kabisa na bado tuliweza kulibeba jahazi."

tembelea www.bongocelebrity.com
 
wanangu fina na kp i wish mngekuwa na uwezo wa kufungua recording studio yenu mkawa mnafanya talk show na kuuza kwenye tv stations,nyingine za kiswahili nyingine za kiingereza.you are so talented,msiache kipaji chenu kika go into waste.lakini yote ni majaliwa,one day yes!
 
msisifie ujinga.
wangekuwa na vipaji basi mara moja tungewasikia radio za kweli kama deutsche welle au BBC, kama wenzao kina aboubakar lyongo, sekione kitojo na wengine wengi wanaotangaza habari na vipindi vya ukweli na sio hayo makelele na majibizano yao kama kilabuni...
 
Inawezekana sijakuelewa mkulu kwani kwenda BBC au DW ndo maana ya mafanikio kwa waandishi wa habari? Inawezekana wasiende huko na wakafanya mambo ambayo dunia inaweza kuwakumbuka milele kwani sio waandishi wote mahili ulimwenguni wamepitia vyombo vikubwa kama hivyo.
 
kipanya alifukuzwa kazi baada ya kuchuuzwa na wenzao waliodanganyana kugoma baadaya kipindi cha chao kilichorushwa live kutoka American Embassy kutokuwa na ubora kutokana na Tecchnical department kuwafanyia 'ntima nyongo' Fina yeye hakufukuzwa ila aliamua kufuata "kampani yake". Walipewa barua wajieleze kwa nini wasichukuliwe hatua kwa kugoma kurusha kipindi, kipanya akajibu jeuri wakamuwasha!
 
msisifie ujinga.
wangekuwa na vipaji basi mara moja tungewasikia radio za kweli kama deutsche welle au BBC, kama wenzao kina aboubakar lyongo, sekione kitojo na wengine wengi wanaotangaza habari na vipindi vya ukweli na sio hayo makelele na majibizano yao kama kilabuni...

Hapa ndipo tunapokosea sisi wabongo,yaani kuwa na mafanikio mpaka ufike majuu.Na huko BBC na Deutsche welle wanaweza kuwaajili wafanyakazi wangapi kwa pamoja,uongo si kazi vijana kazi wanaiweza kwani kipindi walikuwa wanakimudu.MTAENDELEA KUOTA ULAYA MPAKA MNAINGIA KABURINI na bado mnajiita wazalendo.Yaani kama una uwezo basi utathibitika pale utakapo kwenda kuwatumikia wazungu sio,ila uwezi kufanya hivyo hapa kwenu.SAFARI BADO NI NDEFU
 
Labda nikuulize unakubali au hukubali kwamba DW na BBC wana viwango vya juu vya utangazaji? Kwenda kufanya kazi BBC hata nchi kama Uk ni heshima kubwa kutokana na kuwa inaheshimika kwa viwango vyake vya juu. Hii habari ya kufurahi mediocrity yetu na kuitukuza ni upuuzi!! Mi nawashauri Kp na Fina warudi shule wajifunze uandishi wa habari vyema na wakajenge a real carrieer siyo radio jockey who run off their mouths in the morning. Personally I think that they are very nice, lakini kama tunataka kuwapa ushauri mzuri tusiwatie ujinga!
 
Kuwa na kiwango cha juu cha utangaziji haichangiwi na vipaji peke yake bali mazingira na vitendea kazi ambavyo ndivyo wakina kipanya walichokuwa wanakililia.Hata uwe na kipaji vipi kama mazingira ni mabovu lazima utachemsha.Angalia katika soka,ni vipaji vingapi Africa tulivyonavyo lakini hata nusu fainali hatujawahi kunusa,as a continent.

Unatumia staili gani kufikisha ujumbe ni uamuzi wa mtu,kama watu wote tutasema tuwe tunafikisha ujumbe kwa njia ya kama tunasoma taarifa ya habari hatuwezi kufika rafiki yangu.Swala la kwenda shule silikatai,lakini hoja hapa ilikuwa ni vipaji,wanavyo hawana.Na wala mimi siwatii ujinga ila nyie ndo mnajaribu kuwapotosha,kuwa mafanikio ni mpaka kutangaza BBC,kwa hiyo ukishafika BBC ndo basi na sisi kama watanzania tutakuwa tumefaidika nini kwa kwenda kwake huko BBC?Said Kubenea angeenda kufanya kazi daily mail,angeyafanya aliyoyafanya kwa nchi yake mpaka sasa.Hebu tufikirie ni jinsi gani tutaiendeleza nchi yetu na si kwenda kuendeleza nchi za wenzetu.UZALENDO LINA MAANA PANA.
 
Umezungumzia mambo mazuri sana, umetoa mfano wa soka, kwamba vipaji vingi lakini Afrika hatufiki nusu fainali. Sasa ujiulize kwa nini hao akina Drogba wakirudi kuchezea nchi zao bado hawailetei faida?
Pili kuhusu kufaidisha nchi badala ya kufaidisha nchi za wengine, sawa, lakini nchi inatufaidisha vipi? Alafu uzalendo wa akina KP uko wapi? Walifanya kazi gani unayoweza kufananisha na Kubenea? Mi ndo maana nimewashauri warudi shuleni, wasione wamefika.
Mafanikio si kutangaza tu BBC na nimefurahi umetoa mfano wa Kubenea, kumbuka Kubenea amepata acknowledgment za kimataifa na amekubalika kama mwandishi hata na taasisi za kimataifa. Yeye ni mfano wa kuigwa, lakini KP na Fina hapana! They have brought nothing to the table. Safari bado ni ndefu sana kwao, wamepewa 2nd chance, mimi binafsi nadhani ni vyema wameondoka Clouds, waende kupanua mawazo (expand their horizons) maana walikuwa wanadumaa tu (stagnating) Clouds.
 
Labda nikuulize unakubali au hukubali kwamba DW na BBC wana viwango vya juu vya utangazaji? Kwenda kufanya kazi BBC hata nchi kama Uk ni heshima kubwa kutokana na kuwa inaheshimika kwa viwango vyake vya juu. Hii habari ya kufurahi mediocrity yetu na kuitukuza ni upuuzi!! Mi nawashauri Kp na Fina warudi shule wajifunze uandishi wa habari vyema na wakajenge a real carrieer siyo radio jockey who run off their mouths in the morning. Personally I think that they are very nice, lakini kama tunataka kuwapa ushauri mzuri tusiwatie ujinga!

thanx susuviri kwa maelezo yako mazuri ambayo naamini yamewaingia vijana ambao walikuwa wanafananisha chokaa na rangi.
ukweli ni kuwa radio kama BBC au DW kwanza zimesheheni watu makini, waliopitia darasani kuhakikisha wanaendeleza vipaji vyao.
na ni redio ambayo watangazaji wake wanafahamu kuwa wanasikilizwa na watu makini wakiwemo susuviri na gang chomba thats why kila kipindi chao kiko makini...so huwezi kumfananisha mtangazaji wa DW na mtangazaji wa clouds, na mtangazaji wa clouds ambaye anataka akatangaze radio zile basi anatakiwa aingie darasani kisha avue ujinga na utoto wooote auache clouds na avae ngozi mpya yenye busara na umakini wa kazi hapo atakubalika na jamii yenye hekima na si wasikiliza muziki na mabishano yasiyo na msingi
 
Kuwa na kiwango cha juu cha utangaziji haichangiwi na vipaji peke yake bali mazingira na vitendea kazi ambavyo ndivyo wakina kipanya walichokuwa wanakililia.Hata uwe na kipaji vipi kama mazingira ni mabovu lazima utachemsha.Angalia katika soka,ni vipaji vingapi Africa tulivyonavyo lakini hata nusu fainali hatujawahi kunusa,as a continent.

Unatumia staili gani kufikisha ujumbe ni uamuzi wa mtu,kama watu wote tutasema tuwe tunafikisha ujumbe kwa njia ya kama tunasoma taarifa ya habari hatuwezi kufika rafiki yangu.Swala la kwenda shule silikatai,lakini hoja hapa ilikuwa ni vipaji,wanavyo hawana.Na wala mimi siwatii ujinga ila nyie ndo mnajaribu kuwapotosha,kuwa mafanikio ni mpaka kutangaza BBC,kwa hiyo ukishafika BBC ndo basi na sisi kama watanzania tutakuwa tumefaidika nini kwa kwenda kwake huko BBC?Said Kubenea angeenda kufanya kazi daily mail,angeyafanya aliyoyafanya kwa nchi yake mpaka sasa.Hebu tufikirie ni jinsi gani tutaiendeleza nchi yetu na si kwenda kuendeleza nchi za wenzetu.UZALENDO LINA MAANA PANA.

dogo mi nakushauri ufute hiyo kauli yako ya uzalendo.
nyinyi watanzania mnataka uzalendo usimame kwenye vitu visivyokuwa na msingi.
kwa nini uzalendo huu usisimame kwenye sakata za EPA, richmond na mengine meengi yenye manufaa kwa taifa?
 
kipanya na masudy walikuwa ni wehu ni better kama wameacha maana itawasaidia hata wao wenyewe maana walipokuwa wanaelekea ni kupingwa risasi au kutafutiwa kes even kuambiwa wao sio raia wa bongo
kwanza walikuwa wanaboa na story zao za kujisifia sifia kama watoto wa form two na suala la fina na kp kudoana mi nilijua very long tym ago na niliambia watu kama hawa watu hakuna usalama
 
watu wasitake kutuletea uzalendo wa taifa staz hadi huku kwani we unadhani kuna uzalendo bongo?
 
Wakuu nimeona thread moja jamaa masoud kipanya ambae alikuwa clouds alifukuzwa
sasa sijajua sababu nimjuavyo kijana ametulia sijui nje!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom