Maskini wa Mungu mimi sijui nifanyeje!

chukua magadi kilo tano changanya na pilipili kichaa nusu kilo,weka maharage yaliyo kwisha pikwa chini ya mvungu wa kitanda kwa muda wa wiki kisha changanya vyote uoge.......hiyo ni dawa ya kuvuta nyota ya kwako iko mbali sana.

Hashycool....!
 
Wajameni wapendwa wa mmu nisaidieni kimawazo mie mwenzenu nimechanganyikiwa sasa.

Tatizo langu ni kwamba nimemuomba mungu kwa muda mrefu nahitaji kuolewa bila mafanikio wadogo zangu
wote wameolewa marafiki zangu wakaribu wote najisikia vibaya sana najiona sina maisha sina furaha ya ma
isha mimi.

Navyojua mimi kila mwanadamu anahaki ya kuoa/kulewa ili awe na familia sasa mimi maisha gani haya nayoishi raha ya maisha nikuona uko na watoto wako na mume wako kwakweli kuna utamu wake kuliko kuishi kwa wazazi mtu mzima sivutiwi na maisha ya kuishi pekeyangu wala sitamani tamaa yangu nikuwa na familia, kiukweli umri wangu umeenda sana mwezi ujao naanza mwaka wa 32 sasa najiuliza sijui nizae bila kuolewa? Japokuwa naona hali hiyo itanitesa baadae.

Sina lakufanya nalia kila kukicha najiona sina thamani wenzangu wana watoto mimi sina hata wa dawa basi nimechanganyikiwa nasikia uchungu mimi.

Nisaidieni nipeni moyo nifanyeje nimeshaomba mungu saana bila mafanikio.

Wanaume wako wengi Duniani, usijali, utampata anayekufaa.
 
Mbona ni mke wa mtu tayari? Unataka aolewe mara ngapi?

ndo huolewi.yaani wewe husninyo siku ukiolewa paka ataota pembe.tatizo lako huna heshima kwa wanaume.nani atakuoa wakati humheshimu?wewe husninyo wanaume unawaona kama wasichana wenzio.na mwaka huu utajuta kuzaliwa.mwaka jana umesema ooh! naolewa sijui nna mchumba kakutosa.safari hii unamganda uporoto01.unafikiri uporoto ataoa bibi kizee ka wewe?
 
never give up! utaolewa tu. Mungu atatukuzwa kupitia wewe so js hv faith my dia. usiangalie nan kaolewa jst enjoy ur time alon kwanza, ndoa ipo 2, 32yrs sio ming sana.
 
Acha utani kwanza hebu tueleze kwanza tabia yako ya asili ni ipi maana nionavyo mimi hizi tabia unazotuorodheshea sasa hivi ni za kutengeneza na hizi zinakuja baada ya kuona mbona jua linakaribia machweo pasipo kufanikisha lolote mawindoni? Rejea tabia zako za awali kwanza utapata jibu tu hakika naamini wanaume sii wajinga au hawakuoni wakakuvutia upepo kiasi hicho.
Tabia yangu ya asili ni upole
na nilichelewa sana kuanza mambo ya mausiano na wanaume labda ndio tatizo
 
Nooo sikua style hiyo mimi toka nikiwa na 23yrs nilikua nalilia kuolewa mimi, sema tatizo ndio kumpaata huyo mwenzi

Hapo ndio tatizo kwani kwa sabab umeweka kuolewa kipaumbele utawakubali hata wasiokustaili.Relax na ujaribu kujichanganya kwenye social events mbalimbali.Ila fanya haya yote huku ukimshirikisha Mungu kwa kumdai ule mstari aliposema si vema mtu aishi peke yake.Mwanzo 2:18.kila la heri
 
Nashukuru sana kwa mstari
umenijenga, ila kwenye social event ndio kama wapi?
 
chukua magadi kilo tano changanya na pilipili kichaa nusu kilo,weka maharage yaliyo kwisha pikwa chini ya mvungu wa kitanda kwa muda wa wiki kisha changanya vyote uoge.......hiyo ni dawa ya kuvuta nyota ya kwako iko mbali sana.

Ahahahaaah!! Hii kali we ni mganga wa kienyeji?
 
Tabia yangu ya asili ni upole
na nilichelewa sana kuanza mambo ya mausiano na wanaume labda ndio tatizo
Yawezekana ulichoandika hapa ni kweli... Ila najiuliza sana wazo la hiyo id yako lilitoka wapi. Waweza sema si kitu na haina umuhimu sana... Lakini....
 
mimi nafikiri waweza pata watu wanataka kuwa na uhusiano na wewe, wewe ukawa unakataa kwa kutegemea yupo atakayekuja tangaza ndoa kabisa ndo umkubali. watu wanaanza kwa mahusiano ingawa si lazima m'do', then utakapojiridhisha na tabia zake mna'do' maana wengi ndo tunaanza hivyo kuogopa uziwa mbuzi kwenye gunia. so usibane sana eti mpaka ndoa, hao wapo wachache.
kama unapenda kuolewa, ukizaa unapunguza chance ya kuolewa so kwa nini huyo unayemfikiria kuzaa naye ndo umchague atakaye'qualify' kukuoa kabisa? jambo la kuolewa ni rahisi sana tena una kazi, punguza kushinda ndani kwani watu wa umri wako inawawia vigumu kukufuatilia nyumbani kwa wazazi, ivyo kama mkristo jiunge na kwaya, sometimes kutoka na marafiki out wengine wanaweza kuogopa kama unakuwa na misimamo mikali sana ya dini ile ndani full time. play effectively your part the rest God will do.
 
chukua magadi kilo tano changanya na pilipili kichaa nusu kilo,weka maharage yaliyo kwisha pikwa chini ya mvungu wa kitanda kwa muda wa wiki kisha changanya vyote uoge.......hiyo ni dawa ya kuvuta nyota ya kwako iko mbali sana.

mh wakati wengine tunawaza tutapata wapi, wengine wanalia kutoolewa.
 
Mimi nilikuwa nafikiria kutangaza kutafuta mke,maadam wewe umetoa kilio chako hapa ngoja nikufanyie feva kwa kujitolea mimi mwenyewe.,ni PM pls maana mengine ni yetu binafsi.
 
Wajameni wapendwa wa mmu nisaidieni kimawazo mie mwenzenu nimechanganyikiwa sasa.

Tatizo langu ni kwamba nimemuomba mungu kwa muda mrefu nahitaji kuolewa bila mafanikio wadogo zangu
wote wameolewa marafiki zangu wakaribu wote najisikia vibaya sana najiona sina maisha sina furaha ya ma
isha mimi.

Navyojua mimi kila mwanadamu anahaki ya kuoa/kulewa ili awe na familia sasa mimi maisha gani haya nayoishi raha ya maisha nikuona uko na watoto wako na mume wako kwakweli kuna utamu wake kuliko kuishi kwa wazazi mtu mzima sivutiwi na maisha ya kuishi pekeyangu wala sitamani tamaa yangu nikuwa na familia, kiukweli umri wangu umeenda sana mwezi ujao naanza mwaka wa 32 sasa najiuliza sijui nizae bila kuolewa? Japokuwa naona hali hiyo itanitesa baadae.

Sina lakufanya nalia kila kukicha najiona sina thamani wenzangu wana watoto mimi sina hata wa dawa basi nimechanganyikiwa nasikia uchungu mimi.

Nisaidieni nipeni moyo nifanyeje nimeshaomba mungu saana bila mafanikio.
kumbe kuna watu bado,watu tunasaka wife kumbe mpo duuh.!Ndugu yangu God is gr8 endelea ku pray..onyo:usiende kwa waganga wa kienyeji.
 
siko hivyo kaka mie wa kawaida kabisa sina mashauzi , siringi wala sijisikii, siendagi kwenye starehe wala pombe sio mnywaji, nakubalika sana kwenye jamii tatizo ni hilo tuu siolewi sijui nimemkosea nini mwenyezi mungu najuuta

nyavu haikamati pweza dadaangu, wala mshipi hauwezi dawa ni kuzama ndani ya bahari na mkuki. Chamuhimu ni kutongoza mwenyewe mwanaume unaempenda acha kulaza damu shauri yako. Utaja olewa wakati menstruation cycle yako imeshazima..
 
Usichoke wala usikate tamaa kumuomba Mungu,
kwani kila jambo yeye ndio anapanga. Muda ukifika utafanikiwa tu.
Muda gani huo unaouzungumzia? Mungu anaamua anavyopenda anaweza kuamua
aishi bila kuolewa. Muhimu ni kufanya ibada na kujiandaa na yanayokuja mbele ya
safari!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom