Maskini wa Mungu mimi sijui nifanyeje!

chukua magadi kilo tano changanya na pilipili kichaa nusu kilo,weka maharage yaliyo kwisha pikwa chini ya mvungu wa kitanda kwa muda wa wiki kisha changanya vyote uoge.......hiyo ni dawa ya kuvuta nyota ya kwako iko mbali sana.

Kudadeki..hata kombe la babu mwasapile cha mtoto katika hii...chonde usije ukawa Albino tu...!!
 
Unatafuta watoto au ndoa? Kama ni swala la watoto zaa watoto wako wawili, wanaume wa kukuzalisha ni wengi ni kuchagua tu, rangi, urefu, IQ etc!

Kama ni ndoa mradi ndoa nazo zipo tu, usiwe mvivu kwenye love connect!

Lkn kama mapenzi ya dhati, hayatafutwi na huyo better half wako anaweza akaja hata ukiwa in ur late 40s! Na hata akikuta na hao watoto wako 2! N believe me u r never lonely ukiwa na mtoto!

So ushauri wangu; zaa at least mtoto mmoja wakati bado una nguvu na mpaka anamaliza chuo bado utakuwa na nguvu wewe kama wewe wa kumsupport!
Kwakweli itabidi nizae tuu kwanza kuolewa baadae, nashukuru kwa mawazo yako mazuri umenitia moyo
 
Pole dada angu binafsi ntakuweka kwenye Maombi yangu usiku huu,lakn jaribu ku review tabia zako nafikiri unaweza pata jibu,pole Mungu atakupatia mume mwema
 
Wanawake wengi kuna kipindi huwa wanaringa sana wanapofuatiwa na wanaume inapofikia kipindi unahitaji sasa unakosa hata wakukuongelesha nadhani na wewe ulikuwa hivyo so endelea kusubiri banaa.
 
Nafikiri ni busara kama ukijiangalia wewe mwenyewe na zaidi the way unvyoji-position ukiwa na hao wenzi wako ambao hawajaonyesha interest za kukuoa. Inawezekana kuna tabia unazozionyesha kwao au pengine namna ya maongez1 ambayo huwafanya wahisi kuwa huenda ukawa siyo mke mwema kwao.
Jaribu kureview tabia yako, mwenendo, maongezi, mavazi, uhusiano wako na watu wengine etc. lakini nikupe moyo kwamba kwa umri huo, wewe bado kabisa, usikate tamaa.
Katika kuyafanya hayo, pia endelea kumuomba Mungu na kusubiri siyo kujiachia hivyo kwa wanaume kwa sababu ya kutaka kuolewa mwishowe utaonekana malaya ha hautaolewa kamwe.
Kila la kheri, na endelea kuvuta subira ipo siko mambo yatakunyookea.
Yaani sijui nianzie wapi hata, kaka mie ni mstarabu sana, sina tabia za ajabu hata tone, mavazi yangu ni ya heshima
nakubalika kwenye jamii sana yaani kila mtu huwa anajiuliza kwanini huyu dada
haolewi yaani nikimwambia mtu bado sijaolewa haamini mimi ninaheshima na nizamu za kila aina atakaenioa atakuwa amepata mke mwema. Sema tuu ni mkosi
 
Pole dada angu binafsi ntakuweka kwenye Maombi yangu usiku huu,lakn jaribu ku review tabia zako nafikiri unaweza pata jibu,pole Mungu atakupatia mume mwema
ahsante sana kaka nashukuru
sana kwakunifariji na kwakuniombea mungu akubariki sana na familia yako
 
Wanawake wengi kuna kipindi huwa wanaringa sana wanapofuatiwa na wanaume inapofikia kipindi unahitaji sasa unakosa hata wakukuongelesha nadhani na wewe ulikuwa hivyo so endelea kusubiri banaa.
Nooo sikua style hiyo mimi toka nikiwa na 23yrs nilikua nalilia kuolewa mimi, sema tatizo ndio kumpaata huyo mwenzi
 
We bado kijana sana 32 unalalamika? By the way kwani lazima kuolewa? Nani aliyekuambia kuolewa ndio kila kitu. Ni mambo ya muda tu subiri, endelea kuomba mungu atakujibu kwa wakati wake, huo umri wako bado unaruhusu bado kuolewa, tena ukampata mwenye mapenzi ya dhati kwako. Kuwa mvumilivu kwani kuna dada mmoja ni jirani yangu aliolewa akiwa na 37, tena she was hiv+ na aliwahi kupata matatizo akatolewa kizazi sembuse wewe mzima?
 
yaani sijui nianzie wapi hata, kaka mie ni mstarabu sana, sina tabia za ajabu hata tone, mavazi yangu ni ya heshima
nakubalika kwenye jamii sana yaani kila mtu huwa anajiuliza kwanini huyu dada
haolewi yaani nikimwambia mtu bado sijaolewa haamini mimi ninaheshima na nizamu za kila aina atakaenioa atakuwa amepata mke mwema. Sema tuu ni mkosi
hizi sifa unazojipa hapa uko sirious au ndio unajipa promo?
 
Pole sana, lakini tambua kuwa Mungu atakupatia mume mwema kuwa na subira maana furaha yako ya milele inakuja.
 
We bado kijana sana 32 unalalamika? By the way kwani lazima kuolewa? Nani aliyekuambia kuolewa ndio kila kitu. Ni mambo ya muda tu subiri, endelea kuomba mungu atakujibu kwa wakati wake, huo umri wako bado unaruhusu bado kuolewa, tena ukampata mwenye mapenzi ya dhati kwako. Kuwa mvumilivu kwani kuna dada mmoja ni jirani yangu aliolewa akiwa na 37, tena she was hiv+ na aliwahi kupata matatizo akatolewa kizazi sembuse wewe mzima?
duuuh hiyo ni story yakweli au ni style yakunipa moyo kiaina? Maana mbona ni balaa lingine hilo.
 
Endelea kumumba Mungu dadangu. usikate tamaa. Kuwa makini usije kupata bora mume, upate mume bora. sababu ukipata bora mume utatamani mara 100 ubaki hivyo ulivyo. Watoto ni baraka za Mungu tu, wapo ambao wapo kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 10 sasa na hawajapata watoto.Those who walk with God reach their destination.
 
Umenisikitisha sana, kujilaumu kiasi hicho?? We wajuaje kama hilo lisingekuwa jaribu? Piga magoti na umshukuru Muumba wako, muombe mapenzi yake yatimizwe kama atakavyo yeye na si kama utakavyo wewe! 32yrs sio age ya kulalamika na kujikatia tamaa kiasi hicho, kujiita una mkosi ina maana unavikubali vikwazo vya ibilisi na usipokuwa makini atakuharakisha kwa mume mbovu! Suala la ndoa ni nyeti wala halihitaji kupapatikiwa kwa kigezo cha umri kwani unawezajikuta umeangukia pasipofaa! Tuliza akili na uwe makini sana katika uchaguzi wako ila usisahau kufanya kazi ili kuongeza kipato chako!
 
Hiyo ni kweli kabisa; wanaume wengi ambao ni husband material hawana mapesa na magari ila wana love.

Tafuta kijana ambaye ana elimu mambo mengine yatakuja baadae;

Have seen many walioolewa na watu wa kawaida sana; lakini ndoa zimewapa baraka na sasa wana maisha mazuri sana kiuchumi within a very short time. Waoaji wapo lakini si hao mapedeshee.

Kwanza nakupa pole mdada.nna rafiki yangu anatatizo km lako.kila mvulana aliekuwa anamuapproach.alikuwa anachek mfuko wake.anasema kwao maskni nae hatak mtu maskn.umri umeenda sasa.rafiki zake sote tumeolewa na tuna watoto.yeye yupo analilia ndoa sasa.cha kujifunza bora uolewe na umpendae.pesa mtatafuta mkiwa pamoja.pesa ni matokeo. wasichana wengi huwa wanachagua watu wa kuwaoa.wanataka mtu awe na nyumba na gari.na hela juu.matokeo yake wanachezewa na kuachwa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Huna haja ya kukata tamaa,wa kwako yupo anakusubiri na huwezi kukutana naye mpaka wakati mungu aliokupangien ufike,usiangalie binadamu wanasema nn juu yako mwombe mungu akukutanishe na atakayekupa furaha ya ndoa na sio karaha,umri sio ishu kbs, na hao wanaume wakikujua tu uko desperati kuolewa wata take advantage na watakuchezea na kukuacha unalia,zidisha maombi ikiwezekana na kufunga na siku zote mjaribu mungu kwa kumtolea uone namna atakavyokujibu!toa hofu subiri wakati wa mungu.

Hiyo ni kweli kabisa.
 
Hiyo ni kweli kabisa.

Na pia kuwa na mwanaume yule uliyemkubali moyoni mwako na mwenye tabia njema, usikubali kuolewa na mwanaume wa aina yeyote, hata kama atakuambia humtaki kwa sababu unaringa na kujiona muache aongee anavyotaka, mdomo mali yake!, we endelea kumtafuta yule utakaye kufanya uwe na furaha.
 
Acha utani kwanza hebu tueleze kwanza tabia yako ya asili ni ipi maana nionavyo mimi hizi tabia unazotuorodheshea sasa hivi ni za kutengeneza na hizi zinakuja baada ya kuona mbona jua linakaribia machweo pasipo kufanikisha lolote mawindoni? Rejea tabia zako za awali kwanza utapata jibu tu hakika naamini wanaume sii wajinga au hawakuoni wakakuvutia upepo kiasi hicho.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom