Maskini wa Mungu mimi sijui nifanyeje!

Chokochoko

JF-Expert Member
Oct 15, 2011
438
183
Wajameni wapendwa wa mmu nisaidieni kimawazo mie mwenzenu nimechanganyikiwa sasa.

Tatizo langu ni kwamba nimemuomba mungu kwa muda mrefu nahitaji kuolewa bila mafanikio wadogo zangu
wote wameolewa marafiki zangu wakaribu wote najisikia vibaya sana najiona sina maisha sina furaha ya ma
isha mimi.

Navyojua mimi kila mwanadamu anahaki ya kuoa/kulewa ili awe na familia sasa mimi maisha gani haya nayoishi raha ya maisha nikuona uko na watoto wako na mume wako kwakweli kuna utamu wake kuliko kuishi kwa wazazi mtu mzima sivutiwi na maisha ya kuishi pekeyangu wala sitamani tamaa yangu nikuwa na familia, kiukweli umri wangu umeenda sana mwezi ujao naanza mwaka wa 32 sasa najiuliza sijui nizae bila kuolewa? Japokuwa naona hali hiyo itanitesa baadae.

Sina lakufanya nalia kila kukicha najiona sina thamani wenzangu wana watoto mimi sina hata wa dawa basi nimechanganyikiwa nasikia uchungu mimi.

Nisaidieni nipeni moyo nifanyeje nimeshaomba mungu saana bila mafanikio.
 
je wewe ni bikira????????
probably not...

je una sex?probably yes...

na akina nani??????......

how about uanze kuwaambia kila anaetaka ku sex na wewe kuwa 'unajiona huna thamani bila ya kuolewa'
na kwamba uko 'desperate ' kuolewa by 'any means' na hutajali 'lolote lingine' ili mradi akuoe????
 
Mungu hujibu kwa wakati wake usimpangie cha muhimu endelea kumwomba huku ukijithaminisha kwa wanadamu. Wengi wameolewa late wanaenjoy ilhali kuna walioolewa mapema wanajuta na kutamani kutoka. Kama umepangiwa utapata tu jipe moyo
 
Sijakuelewa uliposema sijui uzae tu,huyo unaepanga kuzaa nae si ndo muoane.32 bado kabisa watu wanaolewa na 40
 
Wajameni wapendwa wa mmu nisaidieni kimawazo mie mwenzenu nimechanganyikiwa sasa.

Tatizo langu ni kwamba nimemuomba mungu kwa muda mrefu nahitaji kuolewa bila mafanikio wadogo zangu
wote wameolewa marafiki zangu wakaribu wote najisikia vibaya sana najiona sina maisha sina furaha ya ma
isha mimi.

Navyojua mimi kila mwanadamu anahaki ya kuoa/kulewa ili awe na familia sasa mimi maisha gani haya nayoishi raha ya maisha nikuona uko na watoto wako na mume wako kwakweli kuna utamu wake kuliko kuishi kwa wazazi mtu mzima sivutiwi na maisha ya kuishi pekeyangu wala sitamani tamaa yangu nikuwa na familia, kiukweli umri wangu umeenda sana mwezi ujao naanza mwaka wa 32 sasa najiuliza sijui nizae bila kuolewa? Japokuwa naona hali hiyo itanitesa baadae.

Sina lakufanya nalia kila kukicha najiona sina thamani wenzangu wana watoto mimi sina hata wa dawa basi nimechanganyikiwa nasikia uchungu mimi.

Nisaidieni nipeni moyo nifanyeje nimeshaomba mungu saana bila mafanikio.

0s

0

binti sasa hivikuolewa nikama kugombea ubunge jimbo la igunga.waliomo watakatoka na wanje wataka ingia,na mlango ni mmoja.
 
Kwa sasa cha kufanya badilisha mfumo wa maisha, hilo linaweza kuwa ni tatizo kubwa sana!! Kwa mfano kama unapenda sana kujirusha, mlevi, na unapenda kuonekana expensive kila wakati!!

Wanaume wengi hawapendi wanawake wenye sifa hizo hapo juu

Kuwa karibu na Mungu wako, kuwa na maisha ya kawaida kabisa na jichanganye na watu wa aina zote!! Hakuna anayependa kuoa then atengwe na jamii dada!!!
 
Pole najua una maumivu cos una akili timamu co kama wazee wa kuwepowepo kwanza,i do know ur c'tuation but nakushauri jiweke ktk mazingira ya kuoleka co kutamanisha,bleave or not wapo wanaume wanatafuta wanawake wenye cfa za kuoleka wanakosa even i b4 cjakutana na wangu nime2mia 6yrs kumpata,jipe moyo na utulie mweke Mungu mbele
 
je wewe ni bikira????????
probably not...

je una sex?probably yes...

na akina nani??????......

how about uanze kuwaambia kila anaetaka ku sex na wewe kuwa 'unajiona huna thamani bila ya kuolewa'
na kwamba uko 'desperate ' kuolewa by 'any means' na hutajali 'lolote lingine' ili mradi akuoe????
jibu hayo maswali hapo juu siyo mnakaa kujirusha 2 na wahuini unashtuka umri umekwenda,kaka kwa kifupi siyo bikira huyo coz hizo hazipo siku hizi
 
Mapenzi pekee ndo mchezo usio na mwanzo wala mwisho. Huyu anaingia yule anatoka, huyu hana hamu yule anataka. Omba Mungu zaidi utafanikiwa ila isije ikawa mkamia maji hayaogi pindi utakapopata!
 
Kwa sasa cha kufanya badilisha mfumo wa maisha, hilo linaweza kuwa ni tatizo kubwa sana!! Kwa mfano kama unapenda sana kujirusha, mlevi, na unapenda kuonekana expensive kila wakati!!

Wanaume wengi hawapendi wanawake wenye sifa hizo hapo juu

Kuwa karibu na Mungu wako, kuwa na maisha ya kawaida kabisa na jichanganye na watu wa aina zote!! Hakuna anayependa kuoa then atengwe na jamii dada!!!
siko hivyo kaka mie wa kawaida kabisa sina mashauzi , siringi wala sijisikii, siendagi kwenye starehe wala pombe sio mnywaji, nakubalika sana kwenye jamii tatizo ni hilo tuu siolewi sijui nimemkosea nini mwenyezi mungu najuuta
 
Dada umenkumbusha wimbo mmoja wa dr remmy na kale ka wimbo ka tankat almas...kwa umri wa 32 mbona bado sana! Yule bib wa ufaransa mbona kaolewa akiwa above 70, we subiri tu!
 
Miaka 32 tu unakata tamaa hivo wenzako wanadunda tu, nahisi kama unapenda familia sidhani ni lazima kwanza uolewe ndio ujenge family,waweza kuwa na mpenzi wako mkapatana na kuanza family,pole sana kwa mawazo yako haya, umekosa tu mshauri ndugu yangu, kuolewa sio ishu kabisa kama unataka kujenga familia, ile ni hitimisho tu
 
siko hivyo kaka mie wa kawaida kabisa sina mashauzi , siringi wala sijisikii, siendagi kwenye starehe wala pombe sio mnywaji, nakubalika sana kwenye jamii tatizo ni hilo tuu siolewi sijui nimemkosea nini mwenyezi mungu najuuta
Dada unaonekana uko desperate sana na ndoa, kiasi ukipata mchuchu unakuwa hau concentrate kwenye kuboresha mapenzi, bali kuulizia tu ndoa, relax, let things flow....utashangaa, umri wako bado bwana
 
Miaka 32 tu unakata tamaa hivo wenzako wanadunda tu, nahisi kama unapenda familia sidhani ni lazima kwanza uolewe ndio ujenge family,waweza kuwa na mpenzi wako mkapatana na kuanza family,pole sana kwa mawazo yako haya, umekosa tu mshauri ndugu yangu, kuolewa sio ishu kabisa kama unataka kujenga familia, ile ni hitimisho tu

Ushauri huu haujatulia hata...akitemwa mbele ya safari?...mabinti wazuri msicheze kamari na future zenu na viumbe muwaletao duniani..
 
Back
Top Bottom