Mashua yauwa watu 30 nchini Guinea

Gumzo

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
211
7
Wakuu wa Guinea wanasema kuwa watu takribani 30 wamekufa kwenye ajali ya mashua katika bahari ya Atlantic, Ghuba ya Guinea.

Inaarifiwa kuwa mashua hiyo ilikwenda mrama kwa sababu ya dhoruba wakati ikisafiri kutoka mji mkuu, Conakry, kuelekea kisiwa cha Kassa, safari ya kilomita 10. Shughuli za uokozi zimesimamishwa.

Ajali kama hizo zinatokea mara kwa mara nchini Guinea na kwengineko Afrika, ambako mashua hupakia abiria wengi na hazitazamwi sawa sawa.
-BBC

Ajali-ya-mashua-nchini-Guinea.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom