Mashindano ya U-miss TZ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashindano ya U-miss TZ!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by jebs2002, Sep 4, 2011.

 1. jebs2002

  jebs2002 JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 4,327
  Likes Received: 2,386
  Trophy Points: 280
  Kila kukicha tunasikia na kuona mashindano ya u-miss, ina maana TZ kwa sasa haina njia nyingine ya kusaidia watoto wake wa kike zaidi ya kuwatembeza na kuwavalisha vichupi hadharani?
  Kwani Voda, Airtel na TBL hawana mashindano mengine ya kusaidia watoto wa kike, kama ya business plan, kufanya vizuri O'level, A' level, vyuoni au kuwapa tuzo wale wanaosaidia jamii?
  Wadau mnasemaje?
   
 2. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Mlitaka utandawazi, acha uwaweke wazi!
   
 3. jebs2002

  jebs2002 JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 4,327
  Likes Received: 2,386
  Trophy Points: 280
  Ndio ivyo mkuu, maana haiingii akilini kwa haya mashindano kila kukicha, ina maana hakuna njia zingine za kusaidia watoto wetu wa kike?
   
 4. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Halafu kinachonichefua ukiwaona kwenye TV wanavyokenua meno, kila mmoja anajifanya eti ndoto zake zimetimia kuwa miss upuuzi mtupu
   
 5. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #5
  Sep 4, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  jebs2002,

  Ama kwa hakika hii ni moja katika mada nzuri sana nilizopata kuziona humu JF, nakupa pongezi kwa hilo.

  Watoto wa kike wa Kitanzania, Waislaam kwa Wakristo, walio na dini na wasio na dini. Wanatembezwa nusu uchi wakionesha uzuri na haiba zao kwa maslahi ya wengine. Kama si utumwa ni nini?

  Ukitazama hayo makampuni yanayo dhamini hayana zaidi ila ni kuhakikisha wanatangaza biashara zao kupitia watoto zetu wakike, wakipita kuonyesha maungo yao na jinsi walivyoumbika. Jee, kama huu si utumwa ni nini?

  Tunaiga mambo ambayo si mila wala desturi za Kitanzania wala za Kikristo wala za Kiislam ni za kishetani. Hao watoto maskini ya mungu utakuta wana support yote kutoka kwa wazee wao. Jee, ni tamaa ya maisha, ulimbukeni au ni ujuha? unaowapelekea wazee wa hawa watoto kuona kuwa wanafanya cha maana wanapofikia kuwauza watoto zao kwa njia hii?

  Halafu wengine utaona wakishindwa hujiliza kwa uchungu wa kukosa. Na wanaoshinda utaona eti wanajiliza kwa furaha! Ni nini wanacholilia? kukosa fedha za ushindi au furaha ya kuwa sasa watakwenda kuanikwa zaidi?

  Halafu kinachokera zaidi ni pale vyombo vya habari vinapowafanya hawa kuwa ni mabalozi wa mambo mema na kuwapeleka sehemu za kulelea watoto wadogo ili wawe mfano bora na waige dada zao wanafanya nini.

  Hii ni laana na ushetani na siungi mkono hata kidogo. Ndio hayo, leo mwanao anapita nusu uchi anajianika wewe mzee wake unashangilia. Khaaa.
   
 6. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Haya yote yanatokea kwasababu watu wameipa mkono dini, utandawaz umetawal. Tamaduni za mtanzania si kitu tena. Wazazi wamesahau majukumu yao. Huu ni utumwa. Ushetani. Naupinga.
   
 7. O

  Old Moshi Senior Member

  #7
  Sep 4, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ayo makampuni kama voda na mengine sio ya kulaumiwa, wao wako kimaslahi zaidi. Wakuwalaumu ni hao wanaoshiriki.
   
 8. jebs2002

  jebs2002 JF-Expert Member

  #8
  Sep 4, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 4,327
  Likes Received: 2,386
  Trophy Points: 280
  Nashukuru kwa kunipongeza kwa kuongea mchele! Kwa kweli kama baba wa watoto wa kike 2, hili swala naona limezidi kuburuzwa machoni petu, ingekua mara moja kwa mwaka poa, ila ni kila mwezi utasikia haya mashindano, mpaka tunajiuliza wazee, ina maana voda,zantel, airtel, tbl na wengineo hawana idea nzuri zaidi ya kusaidia watoto hawa wa kike zaidi ya hili?!
   
 9. jebs2002

  jebs2002 JF-Expert Member

  #9
  Sep 4, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 4,327
  Likes Received: 2,386
  Trophy Points: 280
  Ni kweli, ila nao ni wakulaumu, ila ina maana haya makampuni nayo hayawezi kufikiria kama sisi na bado wakatangaza kampuni zao ethically?
   
 10. Nkwesa Makambo

  Nkwesa Makambo JF-Expert Member

  #10
  Sep 4, 2011
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 4,765
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  makampuni yanataka kutangaza bidaa zao kupitia mradi huo, yenyewe yamekosa nini ? hao watoto wa kike hawana wazazi,binafsi mwanangu kwa ruksa yangu hawezi,lakini kwa maamuzi yake siwezi kumzuia akiprove kwamba she is grown up and can take her own course in life...
   
 11. O

  Old Moshi Senior Member

  #11
  Sep 4, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mkuu wanachojali ni pesa hawajali ethics. Lakini cha kushangaza hao wanaowadhamini hawaruhusu watoto wao kushiriki
   
 12. jebs2002

  jebs2002 JF-Expert Member

  #12
  Sep 4, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 4,327
  Likes Received: 2,386
  Trophy Points: 280
  Basi nasi tunaweza kuhusika na kuyauliza haya makampuni kama wataweza kubadilisha mwenendo wao, tatizo hapa sio kuvunja sheria, its a moral issue, nasi wananchi ni lazima tuulize maswali, kwetu bongo inakua ni kawaida kukaa kimya kwenye mambo kama haya, lakini imefika muda nasi tuwe tunapaza sauti kuuliza maswali kama haya, nimefurahi kuna baadhi ya wananchi wameanza pia kulaumu makelele ya promotions za haya makampuni mitaani kwetu, hio ni noise pollution, na pia wanavunja sheria kwa makelele namna hio mtaani, ila naona bado wengi wetu tunayaweka kifuani tu!
   
 13. N

  Nehondo JF-Expert Member

  #13
  Sep 4, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Watoto wa watu wanatumiwa sana maana waandaaji wanapata mamilioni ya fedha wao wanapewa used car....umaskini unachangia
   
 14. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #14
  Sep 4, 2011
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 743
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  hawa wasaidii watoto wa kike wanawatumia!
   
 15. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #15
  Sep 4, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 905
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Niliwahi kuandika makala kwenye gazeti moja la Kanda ya ziwa juu ya hili suala namna mabinti wa U-MISS katika mkoa wa Kagera wanavyodhalilishwa kupitia dhana ya mashindano ya UMISS na kuna jamaa mmoja aliipost humu JF ngoja niitafute,
  nitarejea
   
 16. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #16
  Sep 4, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 905
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Waandaaji wa Mashindano ya Urembo Nchini Tanzania wanavyowaibia Mabinti Zetu!
  Mrembo anajiandaa kwa sh 200,000 anaambulia 50,000 tu[/B


  ]Mchakato wa kutafuta warembo wanaowakilisha mikoa,vitongoji na vyuo ama upo katika hatua za mwisho na baadhi ya sehemu warembo wenyewe wamekwisha patikana.

  Mashindano hayo ambayo yalianza tena mwaka 1994 baada ya kupigwa marufuku na Serikali mwaka 1967 ambapo mrembo Theresa Shayo aliibuka kidedea.

  Mashindao hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka ambapo uanzia katika ngazi za vitongoji hadi ngazi ya taifa ambapo mrembo wa Tanzania hupatikana.

  Ukitazama takwimu za mashindano hayo utagundua kuwa tangu mashindano hayo yaanze hakuna hata Mtanzania mmoja aliyewahi kutwaa taji la urembo wa dunia ,ingawa kuna mafaniko kadhaa yaliyopatikana kutokana na mashindano hayo.

  Inaelezwa na kutanagazwa na waandaaji kuwa washiriki wamekuwa wakipata zawadi mbalimbaki ikiwemo fedha taslimu,bidhaa na wengine kusomeshwa fani mbalimbali hasa za utalii na masuala ya hoteli.

  Jambo ambalo ni muhimu kujadili hapa ni je mashindano hayo yapo kwa ajili ya kuwasaidia wasichana hawa kimtazamo,kifikra,kielimu na suala la kujiamini au ni kwa ajili ya waandaaji kukusanya fedha kutoka kwa wadhamini na viingilio vya milangoni basi !.

  Ebu fikiria mchakato wa kukaa kwenye kambi takribani wiki mbili ambapo licha ya kwamba wanalipiwa malazi na chakula lakini wanajihudumia vitu vingine muhimu kama mawasiliano,mafuta ,vipodozi,nguo nk vitu ambavyo ni gharama kubwa kulingana na hali halisi ya maisha ya sasa na upatikanaji wa vitu hivyo.

  Imeripotiwa hivi karibuni kuwa wasichana waliokuwa wakishiriki shindano la Umiss katika kitongoji cha Bagamoyo 2009 walijikuta wakitapeliwa baada ya kile kilichodaiwa ni zawadi kuyeyuka gafla ukumbini.

  Imeelezwa na vyombo vya habari kuwa washindi wa shindano hilo walitinga katika Ofisi za Kampuni ya Lino Interenational Agency Jijini Dar Es Salaam wakitaka mkurugenzi wa kampuni hiyo ambayo ndiyo waratibu wa shindano hilo washinikize mwandaaji wa shindano hilo kuwalipa zwadi zao.

  Hata hivyo Mkurugenzi wa kampuni hiyo Hashim Lundenga alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa kapuni hiyo hausiki na suala la makubaliano ya washiriki hao na mwandaaji.

  "Kanuni zipo wazi ,kamati ya Miss Tanzania haiwajibiki kwa lolote na suala la zwadi za ngazi za chini yake,kwani hatujui waliahidiwa nini ,hilo litafanywa na muaandaaji mwenyewe na sisi tunafuatilia utekelezaji wake" Alisema Lundenga wakati akihojiwa na gazeti la Bingwa.
  Kwa ufupi ni kwamba washiriki hao tayari wametapeliwa na inawezekana hakuna atakayechukuliwa hatua zinazoweza kuwasadia washiriki bali kamati ya Miss Tanzania inaweza tu kuamua kuwanyima kibali za kuandaa mashindano hayo kwa miaka ijayo.

  Mbali na Bagamoyo ,imetangazwa kuwa Mshindi wa Miss Kigoma taambulia tu sh 250,000 .hivyo washiriki wengine wanaweza kuandoka na kifuta machozi cha sh 30,000 kila mmoja.

  Hivi hizi fedha wanazopata mabinti hawa zinakidhi haja ya ushiriki wa mashindano hayo au ni udhalilishaji wa mambinti zetu ambao kulingana na umri wa miaka 18 hadi 24 badi inawezekana wengi hawajui mipangilio ya maisha yao.

  Hii inatokana na uweli kwamba umri huo wanakuwa bado ni vijana ambao wengi wao wanakuwa ni wanafunzi ambao kimsingi hawajawaha na maamuzi sahii kuhusu nini watafanya katika maisha yao.

  Hivyo hii tabia ya kuwadhalilisha kwa kuonesha maungo yao mbele ya jamii na kulipwa ‘ujira' wa sh 50,000 tu baada ya kutumia fedha nyingi za kujiandaa na kuwapotezea muda ni utapeli wa kiwango cha juu unaofanywa na waandaaji wa mashindano hayo.

  Hata hivyo hiyo ni tisa,kumi na tabia ya waandaaji wote karibu nchini Tanzania kuwa na mtindo wa kutoa kile wanachokiita ‘ofa' ya kusomea fani ya masuala ya Hoteli na utalii.

  Hivi mambiti wote hawa wanataka kusomea fani hiyo,nani alisema kuwa wanaofaa kusomea fani hiyo ni warembo,je fani ya utalii na hoteli haina mahitaji ya mchepuo wa ufauru wa aina ya masomo ?.

  Ina maana hata washiriki wa urembo ambao wao wanafaa kuwa wana- mahesabu,wana-michezo au madaktari kulingana na taranta zao wakifauru kushiriki urembo na kushinda ni lazima wasomee fani hizo?.

  Hivi ni kwa nini mshindi asiulizwe fani anayotaka kusomea ili aweze kupata kile ambacho anapenda kutoka rohoni mwake au kutokana na taranta yake.

  Kulingana na michepuo ya masomo kati ya wanaowania mashindano hayo wamo wenye uwezo katika masomo ya sayansi ambao vipaji vyao labda ni kuwa madaktari au wana-mahesabu ambao wanaweza kuwa wahasibu nk.

  Licha ya kwamba wana sifa hizo na ndoto zao ni kusomea fani hizo lakini hapo hapo wanafaa kuwa warembo iweze kulazimishwa kusoma fani za utalii na huduma za hotelini ? ,Huu ni udhalilishaji.

  Soko la masomo hayo likoje kwa sasa kwani tumeshuhudia wasichana wengi wakisoma fani hizo na matokeo yao ni wachache wanaofanikiwa kupata ajira za uhakika katika sekta hiyo huku wengine wakijikuta wanafanya kazi za kuwadhalilisha ikiwemo kuuza pombe kwenye mabaa .
  Kazi hii kimtazamo wa mazingira yetu ya kitanzania hivi sasa ambapo watalii(wanaodhaniwa ni wastarabu) ni wa kuokoteza ,zinafganywa na watu ambao hawakusome fani husika na wananchi wengi wengi wanasema kama yeyote anayeweza kuvaa kimini,kufungua bia na kuwachekea walevi unaweza kufanya kazi hiyo.

  Inabidi tufike mahali watanzania tuelezane ukuiweli kwamba mashindao haya ni muhimu kwa wasichana hawa kuonesha vipaji vyao vya kujiamini,kujieleza nk lakini kile wanachopata ni sawa na bure .

  Pia kuna huii tabuia ya wasanii wanaotumbiza siku ya Mashindano ambao hulipwa zaidi ya mara kumi ya mshindi wa Kwanza,Hii ni aibu.

  Ni wajibu wa serikali kuingilia kati kuhakikisha mashindao haya yanakuwa na usimamizi unaostahili tofauti na sasa ambapo wasichana hawa wanaibiwa mchana kweupe na wezi(waandaaji) hawakamatwi.

  Ni ajabu Serikali kupitia idara ya Polisi kukimbizana na mwizi wa mayai ya sh 500 tena kwa kutumia bunduki zenye risasi,filimbi,magari nk huku matapeli hawa waandaaji wa mashindano ya urembo wakiachwa ‘wakiwachuna' washiriki wa urembo.

  Ajabu ni kwamba siku warembo hawa wanapokuwa wakitapeliwa ,katika siku ya kutafuta yule ‘wanayemuita' mrembo ukumbi mzima unalindwa na polisi au kwa lugha nyingine ni kwamba polisi wanawasaidia wezi kuimbia mambinti zetu.

  Kibaya zaidi hata baadhi ya viongozi wa serikali ndiyo wanakuwa wageni rasmi hali .

  Imeripotiwa na vyombo vya Habari wiki jana kuwa Waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki dk diodorous kamala aliyekuwa mgeni rasmi katika mashindano ya kumsaka mrembo wa Kagera alilazimika kuongeza fedha kwa mshindi wa kwanza.

  Haikuelezwa kama aliongeza fedha hizo baada ya kusikia kiasi ambacho kilitanagzwa kwa mashindi wa kwanza kuwa ni kidogo au aliamua kutoa motisha lakini ukuweli ni kwamba hata yeye mwenyewe aliona soni ya kutoa zawadi kwa mashindi wa kwanza ambayo ni kiduchu.

  Nadhani tufike mahali tubadilike vinginevyo tutaendelea kuwalea waandaaji wakiendelea kuwaibia washiriki huku wao wakipata faida kibao kutoka kwa wadhamini kwani ni vigumu kupata wadhamini zaidi ya 14 huku mshindi wa kwanza akapata sh 250,000 ,achilia viingilio vya milangoni.Tumechoka wezi hawa wafikishwe mahakamani !.


  Hii makala iliandikiwa na mimi mwenyewe na ilichapishwa na gazeti MALENGO YETU(la kanda ya ziwa June,mwaka 2009)
   
 17. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #17
  Sep 4, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mtoa mada asante sana kwa kuling'amua hili,na cha kuongezea si kwenye umiss tu hata kwenye matangazo ya biashara,wanawake ndio wanaotumiwa sana,hebu fikiria tangazo la sigara lakini mwanamke lazima awekwe pale,ila kinachofanya tuwe hapa ni kwa sababu ya Ubepari,mfumo huu ndio unaofanya mwanamke adhalilishwe sana,kwa sababu BEPARI huangalia fursa,tazama hayo makampuni yanayodhamini,yoooote ni ya kibepari,wanaamin bila kumtumia mwaamke hakuna faida,pili angalia waandaaji,mwandaaji wa miss tanzania ni mwanaume na wa miss utalii ni mwanaume,angalia wanamitindo weengi ni wanaume,lakini wanawalenga nani???WANAWAKE,kingine ni kuikubali,kama watanzania wangeyakataa haya baasi hakuna ambae angeyaendekeza,lakin hata viongoz wetu wanaunga mkono,sijamsikia nchimbi akikemea hili,amekemea big brother tu,kwakuwa haipo TANZANIA,kwa mabinti nao wana tamaa zao,wanataka pesa,umaarufu na kuendesha magari,watafanyaje????kukubali kuuza utu wao ili wafikie malengo yao,hapo sasa!!!!!majaji ndio huwabeba,mda mwingine hata waandaaji,ajabu mashindano haya huwa na majaji wanaume,dah
   
 18. jebs2002

  jebs2002 JF-Expert Member

  #18
  Sep 4, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 4,327
  Likes Received: 2,386
  Trophy Points: 280
  Ni kweli bwana bajabiri na uyasemayo, hasa kwa watoto wa kike kutaka kuendesha gari, kupata vihela labda vya kuanzisha biashara na kujikomboa. Lakini kwa makampuni kuwatumia mabinti zetu namna hii ni hatari sana. Mabinti zetu itakua rahisi kwao kufikiria kuwa haya mashindano ndio yatakayowatoa kwenye umaskini, si kweli, zaidi ya kuwaletea madhara.
  Hatukatai kwa makampuni haya kutumia wanawake au wanaume, swala wanawatumia kwa njia zipi, kwanini wasi promote nembo na biashara zao kwa njia zilizotajwa nami na wadau wengine hapo juu?

  Na hili swala la makelele mtaani ya promotions zao, litabidi nalo likomeshwe pia
   
 19. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #19
  Sep 4, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  <br />
  Kinachowavutia ni pesa na kwa kua walishindwa kupata misaada ya kiilm lazima watoto watafuta njia mbadala. Hapo unategemea wewe mzazi ulieshindwa kumsaidia utamzuia?
  Kwa ujumla inahitaji maangalizi tangu nyumbani. Sisi wazazi ndio mas-ul.
   
 20. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #20
  Sep 4, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Last week nilikua naangalia tv nikaona wapo camp wanafanya mazoez,ukiangalia anaewafanyisha mazoez ni mwanaume,mpiga picha ni mwanaume,na nguo walizovaa ni za utata mtupu,coz walikuwa ufukweni,,,,,,,,,
  <br />
  <br />
   
Loading...