Masheikh wako wapi? Nchi inapotea

Masheikh wako wapi? Nchi inapotea

Kwa muda huu katika mitandao ya kijamii habari zinazozngumzwa ni vipi Maaskofu na wachungaji wa dini ya Kristo wanavyomkosoa Raisi Magufuli vipi anavyoingoza nchi ya Tanzania

Binafsi naona kama hawa watu wa Mungu wamechelewa,walikuwa wamkosoe raisi pale tu alipoanza kuwakashifu na kuwaadhiri raia anaowaongoza hadharani mbele ya halaki ya watu.

Hawa watu wa mungu walitakiwa waanze kumkaripia kumkosoa Raisi pale tu yeye na mtoto wake mkuu wa mkoa walipokuja na tabia wanayoita "Kutumbua majipu"..

Lakini sio mbaya afadhali hawa watu wa Mungu wenye imani ya kristo wameweza kusimama na kuwatetea wanyonge ambao hawana nguvu za kumwambia Raisi kuwa anachofanya sicho,ambacho haifai kumfanyia hata mtoto wako..

Sasa kuna hawa watu wa Mungu wenye imani ya Kiislam masheikh,hawa watu ndio wananishangaza mimi,Juzi nimesoma katika mtandao wa kijamii Sheikh mkuu wa Tanzania (Bakwata) anawamrisha waislam wasifanye mazoezi ya karate..

Kama mtu wa mungu unaiona nchi wapi inaelekea,unaona raisi kakata kamba,hakamatiki,wananchi wanalalamika kila kona wewe unakwenda kuwaambia watu wa imani yako wasifanye mazoezi ya karate..,Ajabu

Ningependa kumwambia Sheikh mkuu wa dini ya kiislam kuwa mazoezi ni njia moja ya kuondoa mkusanyiko wa mawazo(stress) katika akili ya binadamu,Jela zote ulaya lazima wafungwa wawekewe sehemu ya kufanya mazoezi,dakini 30 kwa siku..,sijui jela za Tanzania ziko je kwa hili,wanafanya hivyo ili kuondoa "stress" za wafungwa

Watanzania kwa sasa wanahitaji mazoezi ya nguvu ili kuondoa "stress",maisha yamekuwa maugu kila mtanzania ana mawazo yaliyomzidi uwezo...

Huyu Sheikh angeligombania mambo ya msingi wanayoyataka waislam mfano mahakama ya Kadhi ambayo imepigwa vita na wafuasi wa dini nyangine,Masheikh kutoka Zanzibar wamewekwa ndani zaidi ya miaka mitano(5) sasa bila kupewa huku yoyote...

Au angalau huyu Sheikh asimame pamoja na watu wa Mungu wenye imani tafauti na yeye ili kumkosoa raisi kwa haya anayowafanyia watanzania ambao ndio anaowaongoza

Nawapa hongera kwa watumishi wa Mungu wenye imani ya Kikiristo kwa kusimama kuitetea demokrasi na haki za msingi za watanzania wote bila ya kujali imani zao
Viongozi wadini wengi ni matapeli tu kama matapeli wengine !wako mbali na Mungu ....msiwaone wamejivika misalaba mikubwa au kupaka hina ndevu zao na sigda uchwara!wasitupotezee muda!wenye akili timamu hatuna muda wa kijinga kuwasikiliza.....fanya kazi!
 
Unajifanya kiziwi wa upande mmoja wa dini fatilia utona uonevu uliopo asubutu Sheikh kuongea atawakaribisha wenzie Kina Kakobe sero na ninani kakuambia hilo baraza ni la waisilamu una changanya jumuia za kiisilamu na jumuia za chama tumuombe Mungu viongozi wageuke na kuongoza nchi kwa misingi ya sheria bila ubaguzi
Unazungumzia wale magaidi mulowaweka ndani bila kosa eee
 
Ni vema ungejiuliza kwanini mashekh wakiikosoa serikali wanakamatwa na kufungwa na je kwanini maaskofu wakifanya tukio kama hilo hawafungi wala kukamatwa.labda tungeanzia hapo
 
Amkeni masheikh tunawategemea sn kwenye hili vivinginevyo nisijesikia sheikh yeyote baadae anaombea amani wkt alikiwa na nafasi na kukemea maovu ya sirikali
 
Masheikh wako madrasa wanawapa watoto elimu ya akhera baba magufuli kashawapa elimu dunia bure. Mbona amani yakutosha tu ipo tunaenda masjid kila siku saa 9 au 10 usiku natunarudi salama. Apambane tu huyo alishikiliwa pu.mbu kwa maslahi yake
 
Naona watu wamejielekeza kwa Bakwata tu kana kwamba bakwata tu ndiyo kuna masheik pekee.
Mkuu BAKWATA=Baraza kuu la waislam Tanzania,sasa watu uwanaka wajielekeze wapi
 
Tehetehetehe! Kikwete waliswali naye wakashindwa kumshauri kwa wizi na ufisadi uliofanyika na wateule wake. Leo wataweza wataanzia wapi? Wahusika wakubwa wakubwa wa hayo maovu wengine ni mashekhe na maaskofu. Dini ni vivuli tu.
 
Back
Top Bottom