Hiyo hoja ni kweli viongozi wengi wa kikristo kama wanatapa upendeleo fulani hivi kwa serikali pindi wanapofanya mambo ambayo ni kinyume na serikali.
Lakini ishu inakuja kwa mfano hapa kwetu Tanzania kwa upande wa Kiislam taasisi kubwa ni BAKWATA, wao ndiyo wenye wajibu wakutoa muongozo, kutetea au kukemea vitendo vibovu vya watawala, lakini wao wamekuwa kama mawakala wa watawala kwa miaka mingi sana, shida inakuja hata ambao wamejaribu kujitoa Muanga kama Sheikh Farid/Mselem/Ponda na wengine wote mwisho wa siku wanawageuka na kuwa upande wa watawala. Huu unafki wanaofanya ni miaka na miaka.
Kama BAKWATA hawataki kujihusisha na siasa, basi wasiwe nasifia pia mambo mazuri ya wanasiasa!!! Sheria ya kusifia inaenda sambamba na kukosoa.