Masharti ya suti

Masharti ya suti

Mfalme Daudi

Senior Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
110
Reaction score
245
Jamani nimenunua suti mpya Na ni mara ya
kwanza kuvaaa!nimeambiwa ina taratibu zake,so naombeni mwongozo Na kanuni za suit kabla sijaivaa..
 
Sheria ya kwanza usivue koti lake hata kama kuna joto kali kama maji ya kunyonyelea kuku!
 
La pili usibebe mfuko wa rambo.hatakama ukinunua mchicha na nyanya sokoni weka kwenye bahasha
 
Jamani nimenunua suti mpya Na ni mara ya
kwanza kuvaaa!nimeambiwa ina taratibu zake,so naombeni mwongozo Na kanuni za suit kabla sijaivaa..

Nakusihi usiwasikilize hao wote waliokupa ushauri maana utakuja kukosea. Sharti kuu na la kwanza kuhusu suti linasema kuwa kama ni mara yako ya kwanza kuvaa suti, basi usiivae

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
5.usiivae na yebo yebo 6:usipande daladala tembelea gari yako
 
7. Usikimbie hata kama utahisi kama kuna vitu vizito na vyenye ncha kali, we tembea tu.
 
Usitembee na vimia mia kwenye mfuko na hata ukinunua kitu chenji acha kwa mwenye duka
 
Ukivaa suti usipige chafya
Usiteme mate, kikoozi wala kutoa kamasi ovyo
Usitembee kwa mguu wala kupanda bajaj, au boda boda
Usidai change uendapo dukani
Mara zote meno nje kwa tabasamu
Usibebe bidhaa yoyote kwa mfuko wa rambo


NK
 
-usilalamike ukiibiwa ama kutapeliwa.
-usisahau kunyonga tai.
 
Ucnunue karanga,icecream wala maandazi njiani ukaanza kutembea unatafuna
 
Kufua. Dry cleaners ndio kazi zao. Marufuku kwenda kwa dobi au kufua mwenyewe au mwenzi wako au haude girl.
 
Aya mashari naona wazungu tu ndoo naona wana yawezaa lakini kibongo bongo mmmmh uvaliee malapa au uchomeke koti nani ata kuulizaa waraiyaa washaa vurugwaa uku kama sunuraa wamajaangaa?
 
Back
Top Bottom