Mashabiki wa Madonna wamshtaki kwa kuchelewa kuanza Show. Kibongo bongo Wasanii wengi watafungwa wakianza kushtakiwa

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,616
Mashabiki wa Mwanamuziki Madonna (65) wa Jijini New York wamemshtaki mwimbaji huyo kwa 'Udanganyifu' na 'Mazoea Mabaya' baada ya kuchelewa kuanza tamasha lake, la Disemba 13, 2023 wakidai kuwa "walilazimika kuamka mapema kwenda kazini" siku iliyofuata

Kwenye kesi iliyowasilishwa katika Mahakama ya shirikisho ya Brooklyn, Michael Fellows na Jonathan Hadden wanasema walinunua tiketi za tamasha la Madonna la Disemba 13, 2023 ambapo alipanda Stejini Saa 4:30 (Nne na Nusu) Usiku badala ya Saa 2:30 (Mbili na Nusu) Usiku muda ulioandikwa kwenye tiketi

Upande wa Mashtaka umedai tamasha lilichelewa kuisha hivyo kusababisha Mashabiki hao kukumbana na changamoto kama uhaba na gharama kubwa za usafiri wa umma na binafsi, kuchelewa kazini na kushindwa kutimiza majukumu yao ya kifamilia siku iliyofuata

Vipi Mdau, unadhani ni wakati wa Mashabiki Tanzania kuanza kushtaki Wanamuziki waliozoea kuchelewa kupanda 'Stejini'?


Chanzo: The Guardian
 
Back
Top Bottom