Masanja: Nimevuna mpunga ekari 15 Mbarali Estate - Mbeya

hasason

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
1,648
1,539
Kijana masanja mkandamizaji as known as Pastor to be akijituma uko ubaruku, inasemekana anazalisha 200 bags per year kwenye hii investment tu, sa soon tu huyu si mwingine kabsa, huu ni model kwa vijana wote wanaopenda mabadiliko so keep stepping forward man!!!

Mchekeshaji maarufu kupitia kipindi cha Ze Orijino Comedy, Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja Mkandamizaji amesema kuwa vijana wanapaswa kufikiria namna ya kuwekeza mashambani kwenye fursa za kutosha kuliko kuendekeza majivuno yasiyo na msingi.

Akizungumza na Starehe Masanja alisema anafurahi kwani mwaka huu amefanikiwa kuvuna tani kadhaa za zao la mpunga katika shamba lake lililopo Mbarali Estate.

"Nimelimia Mbarali Estate namshkuru Mungu kwa kufanikiwa kuvuna mpunga wangu baada ya kuwekeza shamba lenye ukubwa wa ekari 15, huu ni uwekezaji mzuri unaotoa matunda kwa muda mfupi iwapo utahudumia shamba lako ipasavyo."

"Vijana wengi wana nguvu na uwezo wa kuingia mashambani ila wanaendekeza ‘usharobaro' kitu ambacho hakina mavuno kwao," alisema Masanja aliyetumia mashine ya kisasa katika zoezi hilo.

Masanja ambaye pia ni mwimbaji wa kwaya ya New Jerusalem alisema: "Mimi ni mchungaji mtarajiwa lakini huduma yangu ya uchungaji nimeanzia kwenye kundi langu hili la Ze Komedy, kupitia hilo nina washirika wangu ambao natamani wawe kama mimi mchungaji wao wafuate nyayo zangu, naomba maombi ya watumishi wengine wamuombee Joti," alisisitiza!

Kwa sasa, Masanja anahudhuria ibada katika kanisa la EAGT, Mito ya Baraka pia amefanikiwa kutoa nyimbo 10 za Injili na tayari album yake ya ‘Hakuna Jipya' iko mitaani.


Masanja : Nimevuna mpunga ekari 15 Mbarali Estate Mbeya - Makala - mwananchi.co.tz


attachment.php
 

Attachments

  • 5.jpg
    5.jpg
    55.7 KB · Views: 3,440
Kavaa soksi.....mkuu usistaajabu mikate ilikuwa ikikandwa kwa miguu na tulikula. Kwakweli nami nafikiria niwe msanii ili nitoke, kumbe inalipa hivyoo

Hata michicha inayolimwa kwenye bonde la Msimbazi tunakula licha ya kuonywa na serikali mara kadhaa

Kuwepo kwa mazoea fulani hakuna maana kwamba lifanywalo ni sahihi

Mengine hayapendezi
 
Umeonae hawa watu ni wavitendo zaidi mboyoyo ni marufuku me namkubali sana chalii!!!!

Soon mtamuita fisadi, na kuanza kumchukia, kawaida kwa watanzania, wivu halafu kazi hawataki kifanya, ukijituma unaitwa fisadi au freemason, watanzania tujifunze kependa maendeleo, na si kila mali inapatikana kwa wizi au nguvu za giza
 
vijana wanangoja chadema iwalete maendeleo.. wakati serikali tayari imeweka fursa za vijana kuhangaika.... mf.mzuri kuna kijana kajenga nyumba yake anasomesha na anafamilia yake kwa biashara ya kuuza karanga za kukanga ..lakini wako mtaani wanapiga kelele ccm ccm mbaya ccm mbaya ccm mbaya...kalaga bao
 
vijana wanangoja chadema iwalete maendeleo.. wakati serikali tayari imeweka fursa za vijana kuhangaika.... mf.mzuri kuna kijana kajenga nyumba yake anasomesha na anafamilia yake kwa biashara ya kuuza karanga za kukanga ..lakini wako mtaani wanapiga kelele ccm ccm mbaya ccm mbaya ccm mbaya...kalaga bao

ubaya wa ccm ni wezi na wanateteana!
 
He! Hiyo Harvester pia ni ya kwake au ya kukodi? Mbona namuogopa sasa huyu mtu duh! Hongera sana Mkandamizaji.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom