Kilimo cha mpunga Tanzania

Vitalis Msungwite

JF-Expert Member
May 11, 2014
3,270
7,769
Huu ni uzi utakaobeba mambo mengi kama sio yote kuhusiana na kilimo cha mpunga nchini Tanzania.

MPUNGA
Hili ni zao la chakula linalolimwa kwa wingi kwenye maeneo ya ukanda wa joto.

Zao hili linastawi zaidi kwenye udongo wa tifu tifu na eneo lenye maji ya kutosha. Baadhi ya maeneo (,Mikoa) yanayolima zao hili kwa wingi na kulitumia kama zao la biashara ni Morogoro,Mbeya, Tabora, singida na shinyanga.

NAMNA YA KULIMA MPUNGA
Kwa Tanzania mpunga huzalishwa kwa mifumo ya aina mbili. Yaani kumwaga/ kusia na kupandikiza miche.

1: KILIMO CHA KUMWAGA/ KUSIA
Huu ni mfumo wa kulima mpunga kwenye maeneo yenye uhaba wa maji. Katika kilimo hiki mkulima hukwatua shamba na kulitifua tifua/ kupiga piga mabonge na kuanza kumwaga mpunga katika eneo lote la shamba. Baada ya kumwaga mpunga hutifua tifua tena ili kuufukia mpunga kwenye udongo tayari kwa kuoteshwa.

Wakati mwingine kama eneo lina maji basi mkulima huloweka mbegu kwa masaa 24, huiopoa na kuivundika kwa siku tatu. Ikianza kuota basi hubebwa na kumwagwa shambani bila kufukiwa tayari kwa ukuaji. Katika umwagaji huu hatua ya kukatua na kuvuruga/ kutifua eneo haikwepeki. Baada ya kumwaga mkulima anatakiwa kuhakikisha ulinzi wa ndege unakuwepo.

Kutokana na maendeleo ya teknologia kazi zote zinzfanywa na mashine kwa wenye mitaji. Mfano kazi ya kukatua hufanywa na trekta, kazi ya kutifua / kuvuruga hufanywa na trekta na pawatila zenye rota. Vile vile kazi ya kumwaga mpunga hupandikizwa kwa kutumia mashine maalumu.

Maeneo mengi nchini hutumia mfumo huu lakini maeneo maarufu ni Morogoro na Kyela Mbeya.

GHALAMA ZA UZALISHAJI KWENYE KILIMO CHA KUMWAGA

Ghalama za kilimo hiki ni kama ifuatavyo.

a) Kukodi shamba ....... Tsh 50,000 - 100,000 kwa heka kutegemeana na location kwa Moro ni 50,000 kwa heka.

b) kukatua shamba kwa disc ....... Tsh 40,000 - 65,000.

c) kumwaga ........Tsh 30,000

d) Kung'olea/ kupalia ........Tsh 30,000- 60,000

e) kuvuna ......... Tsh 30,000 - 60,000

Ghalama nyingine ni roundup, 2-4D ambazo ni Tsh 30,000- 45,000, kufukia mpunga kwa rota 30,000 - 50,000, Mbegu debe 2-3 kwa Tsh 20,000/30,000.

Jumla ya ghalama za uzalishaji kwa kilimo cha kumwaga kwa wastani ni Tsh 200,000- 300,000.

Kipato kwa kilimo cha kumwaga wastani ni gunia 4- 8.


2: KUPANDIKIZA MICHE
Huu ni mfumo ambao hutumia mbegu iliyooteshwa kwenye vitalu katika kupandikiza mpunga. Mbegu hii huandaliwa kwa namna mbali mbali kama vile.

i) kumwaga mpunga mkavu moja kwa moja. Katika njia hii mkulima huandaa kitalu, na kumwaga mpunga alioutenga kwaajili ya mbegu. Baada ya kumwaga humwagilia maji ili mpunga upate maji tayari kwa kuota. Kitalu ili kilete manufaa inashauriwa kifunikwe kwa turubai la mifuko ya maroba au nyasi.

Kipimo kizuri cha kitaru kwa heka moja ni hatua/ mita 10× 15 na mpunga ni debe 3 kwa mpunga usio na taka taka. Ukikata kitaru cha 10×15 basi unatakiwa kugawanya Mara tatu yaani upate vitaru vya 3×10 ambavyo utamwaga debe moja la mpunga kwa kila kitaru.

ii) Kumwaga mpunga uliooteshwa
Katika mfumo huu, mbegu ya mpunga huandaliwa na kulowekwa kwa masaa 24. Baada ya kulowekwa huvundikwa kwenye mfuko au katika kifaa chenye sifa sawa na hicho kwa siku tatu na kwenda kumwaga. Kitaru kitakuwa na sifa sawa na zile za 2(i) lakini hapa lazima kiwe na unyevu wa kutosha kama sio ubichi kabisa ili mbegu isiungue. Kitaru kisiwe na maji ili kuepusha mbegu kuoza.

Kwa wanaotumia planter wao hutumia njia hii lakini wao huvundika kwenye trei au kumwaga kwenye vitalu vinavyotandikwa kitambaa au kitu mfano wa kapet maalum. Hapa sitaeleza sana maana hapa nchini ni wakulima wachache wanaotumia planters.

Kwa kawaida miche ya mbegu huwa tayari kupandikizwa baada ya siku 21 na haishauriwi kuipandikiza ikiwa na siku 45. Kuna wale watu wa shadidi mbegu zao huwa tayari kupandwa ndani ya siku 7-14.

Mfumo huu wa kuwatika mbegu unatumiwa sana maeneo mengi yanayoendesha kilimo cha umwagiliaji hasa Mbarali (Mbeya), na maeneo mengine yenye mvua za uhakika.


GHALAMA ZA UZALISHAJI KWA HEKA

a) kukodi Shamba ...... Tsh 100,000 - 300,000 kutegemeana na location

b) kukatua ....... Tsh 60,000- 70,000

c) kukata matuta ...... Tsh 15,000

d) kuvuruga/ kuchabanga .......Tsh 60,000- 70,000.

e) Kupanda ...... 60,000- 90,000

f) kungo'olea/ kupalia ...... Tsh 30,000- 45,000

g) kulinda/ kuamia ndege..... Tsh 30,000- 40,000

h) kuuvuna .....Tsh 200,000 kwa combine/ 150,000 kwa kutumia nguvu kazi.

Ghalama nyingine ni mbegu debe 3 (30,000), 2-4D (10,000-15,000), mbolea mifuko 2-4 ( 120,000- 200,000), kuandaa kitalu cha mbegu 10,000.

Jumla ya ghalama za Uzalishaji kwa heka kwa wastani ni Tsh 500,000 bila mbolea na 700,000 pamoja na mbolea

Kipato ni gunia 10 - 35 kwa heka kutegemeana na eneo na matunzo.

MATUMIZI YA CHEMIKALI KWENYE KILIMO CHA MPUNGA.

Kilimo cha mpunga hutumia chemikali za aina mbali mbali kama vile.

1. Dawa za kuunguza majani aina zote.

Hizi dawa hutumika kuangamiza majani yote shambani ili shamba likatuliwe au kuvurugwa. Dawa zinazotumika na muda wa kuisha makali shambani ni kama ifuatavyo; Round up ..... Siku 21, melaxone.... Siku 7 na chemikali nyingine zenye sifa sawa na hizo.

2: Dawa za kuua majani yenye asili ya majani mapana na ndago. Hizi hufahamika kama 2-4D, hutumika kudhoofisha na kuua kabisa magugu yasiyotakiwa kwenye mpunga. Majani yenye asili ya mpunga hayafi ndio maana inashauriwa baada ya kupiga dawa ungolee ili kuondoa magugu yasiyokufa kwa dawa. Dawa hizi zipigwe siku 21 toka siku ya kupanda mpunga na kwa wanao mwaga wapige siku 28 -30 toka siku ya kumwaga. Haishauriwi kupiga awamu mbili au zaidi kwani licha ya kuua magugu hudhoofisha mpunga.

3: Dawa za kuzuia magugu kuota.

Hizi ni dawa ambazo hupigwa siku ya tatu baada ya kupanda mpunga wakati shamba likiwa katika hali ya tope tope. Huzuia mbegu za magugu zisipasuke na kuota. Haishauriwi kupigwa kwenye mpunga wa kumwaga maana hatà mpunga hautaota . baadahi ya dawa hizo ni RILO R500, na Maguguma na dawa nyinginezo zenye sifa sawa na hizo.

4:Mbolea

Kuna aina mbali mbali za mbolea lakini kwa kifupi ni

DAP... Kupandia, hupigwa siku saba toka siku ya kupandikiza au siku ya kupandikiza.

UREA......Kukuuzia hupigwa siku 21 toka siku ya kupandikiza.

S.A ..... Mbolea ya magadi hupigwa pamoja na mbolea za kukuuzia au kuzalishia.

CAN..... mbolea ya kuzalishia hupigwa wakati mpunga umeanza kufunga(mimba)

AMIDAS..... Kukuuzia, kuondoa magadi, kuzalishia.

Utaratibu wa upigaji mbolea ni siku 14 toka mbolea ya awamu ya mwanzo.
 
Umetisha sana mkuu.

Hope huu uzi utachanganya ili watu waelewe vizuri kulimo hichi.
 
Bw. Vitalis Msungwite, michele inayosifika Tanzania kwa ubora/kunukia ni mitatu - Kyela, Magugu, na Shinyanga. Michele hii haiwezi kustawi maeneo mengine ya nchi kunakolimwa mpunga mfano Morogoro, Pwani, Tanga, n.k?
 
Bw. Vitalis Msungwite, michele inayosifika Tanzania kwa ubora/kunukia ni mitatu - Kyela, Magugu, na Shinyanga. Michele hii haiwezi kustawi maeneo mengine ya nchi kunakolimwa mpunga mfano Morogoro, Pwani, Tanga, n.k?
Kikubwa ni mbegu ya mpunga uipate inayozalisshwa maeneo hayo. Mpunga haubadiliki kulingana na mazingira isipokua ubora wa mchele unaweza kuathiriwa na aina ya udongo na matumizi ya kemikali hasa mbolea, viuadudu, viuagugu na madawa mengine yanayofanana na hayo.
 
Niliwahi kusikia zipo mashine unaweka shambani zinatoa mlio wa sauti ambayo hakuna ndege anayeweza kutua eneo hilo kwa mzunguko wa nusu kilomita. Mtaalam hizi mashine zipo, kama ndiyo nitazipataje na bei gani. Nataka nizifunge mwenye mashamba ya mpunga.
 
Niliwahi kusikia zipo mashine unaweka shambani zinatoa mlio wa sauti ambayo hakuna ndege anayeweza kutua eneo hilo kwa mzunguko wa nusu kilomita. Mtaalam hizi mashine zipo, kama ndiyo nitazipataje na bei gani. Nataka nizifunge mwenye mashamba ya mpunga.
Kuhusu hili LA mashine silijui kwakweli ndo nasikia kwako. Kwa sehemu kubwa watu katika udhibiti wa ndege wanatumia vibarua au kupanda mbegu zisizopendwa na ndege.
 
Niliwahi kusikia zipo mashine unaweka shambani zinatoa mlio wa sauti ambayo hakuna ndege anayeweza kutua eneo hilo kwa mzunguko wa nusu kilomita. Mtaalam hizi mashine zipo, kama ndiyo nitazipataje na bei gani. Nataka nizifunge mwenye mashamba ya mpunga.
Asee ni kweli nilishawahi kuziona kwenye maonesho ya nanenane morogoro mwakajuzi kama sijakosea. Zilikua zimetengenezwa na veta

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kuna gharama zengne za ziada kama kukusanya mpunga baada ya kukata,kupiga,kupepeta/kuisafishia,kushona Kwenye viroba na kuusafirisha kutoka shambani adi godown/store.
 
Niliwahi kusikia zipo mashine unaweka shambani zinatoa mlio wa sauti ambayo hakuna ndege anayeweza kutua eneo hilo kwa mzunguko wa nusu kilomita. Mtaalam hizi mashine zipo, kama ndiyo nitazipataje na bei gani. Nataka nizifunge mwenye mashamba ya mpunga.
Mkuu kuunda mashine ya kutoa sauti sio ishu ishu ni gharama ya vifaa but unaweza kumodify baadhi ya vifaa mfano amplifier wanazotumia wauza mitumba kuita qateja. Wanaiset inakuwa inasema mda wote.
Mfizikia au fundi/ injinia anaweza Ku design kifaa cha kutoa sauti inayojirudia rudia ambayo itatumia sola au betri ya kuchaji.Waone wataalamu wa veta au mafundi mfanye makadirio, atakuundia sio ishu kubwa.
Je ndege ni sauti zipi hawazipendi za watu au hata king'ora.Kama king'ora hawapendi basi ni rahisi sana kupata king'ira na kumodify kidogo kisha unaenda kukitega shambani.
 
Mpunga sikuhizi kyela hakuna kitu ns usangu wanaweka mbolea na madawa mpunga mzuri ni wa kamsamba rukwa huo ndo super kwa sasa ni mtamu na unanukia balaa na kule hawaruhusu mbolea mashambani mwao
 
Mpunga sikuhizi kyela hakuna kitu ns usangu wanaweka mbolea na madawa mpunga mzuri ni wa kamsamba rukwa huo ndo super kwa sasa ni mtamu na unanukia balaa na kule hawaruhusu mbolea mashambani mwao
Naomba connection ili noanze jiki kilimo next zone
 
Mpunga sikuhizi kyela hakuna kitu ns usangu wanaweka mbolea na madawa mpunga mzuri ni wa kamsamba rukwa huo ndo super kwa sasa ni mtamu na unanukia balaa na kule hawaruhusu mbolea mashambani mwao
Kamsamba ni songwe, kule mpunga wanajitahidi sana,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom