Masanja na Uropokaji kwa Wazee!

Paka jimmy ulitaka asemeje? maana yeye amesema tu! hao EATV wametenda kabisa! nani unafikri wa kulaumiwa zaidi?

after all ni ze comedy
 
Kwanza hakumtaja Mengi.

Pili hata kama angemtaja Mengi, jamii yenye uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza isingejali, as long as angekuwa na vithibitisho.

Tatu, katika jamii inayojali uhuru wa kujieleza, hata mawazo ya kijinga yana ruhusa kupata nafasi.

Nne, hukulazimishwa kuangalia.Katika jamii yenye kufuata mfumo wa soko huria kuna vyombo vya habari vinavyotangaza ujinga makusudi kwa sababu pengine ujinga ndio unauza(The New York Post, Uwazi). Wewe kama unaona huu ni ujinga usinunue bidhaa, usinunue gazeti, usiangalie kipindi. Mwisho wa siku wadhamini watajua kipindi hakiangaliwi, wataondoa matangazo yao na hao mabosi wenyewe wataona ulazima wa kubadilisha.

Ndio maana kuna watu hawanunui vitu Wal-Mart (low price supermarket) kwa sababu wana protest hali mbaya za wafanyakazi.Badala yake wananunua vitu kwa bei ya juu zaidi lakini wanajua hawachangii katika kuitajirisha Wal-Mart.

Watu wali protest kununua ndizi za Costa Rica kwa sababu mabwanyenye walikuwa wanapuliza madawa kwa kutumia ndege na kupulizia sumu kwenye visima vya wafanyakazi wa mashamba ya ndizi waliokuwa wanaishi katika mashamba hayo (plantations).

Kwa hiyo kama hupendi kitu, anzisha "boycott" campaign. Ama sivyo utakuwa unaleta advertisement zitakazoongeza ratings zao tu.
 
Hiyo kwenye mabano aliiweka Masanja au ya kwako?. Kama Masanja hakutaja jina la mtu basi sioni ubaya upo wapi. Maana Mtu si Mengi pekee, sisi sote ni watu.

Tusimuwekee masanja maneno mdomoni mwake. Cha kufanya mtafute umuulize alikuwa anamuongelea mtu yupi?. Then lete jibu tulijadili.
Naona kinachofanyika hapa ni kujaribu kutorosha ukweli ulio dhahiri. Haya mtolee Masanja maneno mdomoni mwake basi !!!
 
Masanja and co.wamefulia,mimi sioni kama kuna komedi ila wachovu wanahangaika na kuchosha minds za watu.Ndiyo maana hata kutazama hicho kipindi nimeacha.Hakuna kinachochekesha!
 
Usingoje utafuniwe na umezewe, weye Hof nini sijui(naogopa name-calling)!
Alianza kwa kusema...jirani kaamua kurudisha kipindi kama hiki katika muda sawasawa na wakipindi chetu hiki...Kashfa nyingi zikafuata.
Unadhani jirani yao huyo ni nani?

Unaogopa nini? call me whatever you like that's part of your freedom. But I am not convinced with the way you have mischaracterised Masanja, If he didn't Mention Mengi by name, why bother?. I like EATV as well as TBC1 and will be watching any programme that will make me happy regardless of which station is behind it. But misrepresentation is not acceptable.
 
Amesahau alikotoka.
Samahani hii ni maisha binafsi, lakini mtu anapokera kiasi hiki inabidi kumkumbusha udhaifu wake- Huyu masanja ni kweli amesahau alikotoka, nadhani hii n i tabia yake maana angekuwa anakumbuka alikotoka asingeigiza kuwacheka watu kuishiwa wakati yeye na umaarufu wote huo nyumba yao pale ubaruku Rujewa ni ya Nyasi-choka mbaya kabisa. Angekuwa anakumbuka alikotoka angeenda kurekebisha kwao kabla ya kushambulia wenzie achalia mbali mtu kama RM
 
Naona kinachofanyika hapa ni kujaribu kutorosha ukweli ulio dhahiri. Haya mtolee Masanja maneno mdomoni mwake basi !!!

Explain more please!, Sijakuelewa unachotaka kuhabarisha! FAFANUA
 
Sio masanja tu, bali pamoja na washirika na washabiki wake wote IQ zao ni finyu sana.

Sijui kigezo gani umetumia kupima Intelligence quotient (IQ) ya hao wasanii kwenye upande huo wa burudani?...Sijui mwenzangu unaIQ ngapi ww ...150?? Hao ni wasanii na kazi yao nikutoa burudani/kuelimisha/kukosoa na kukosolewa pia..boriti..kibanzi..mboni
 
Masanja and co.wamefulia,mimi sioni kama kuna komedi ila wachovu wanahangaika na kuchosha minds za watu.Ndiyo maana hata kutazama hicho kipindi nimeacha.Hakuna kinachochekesha!

Mambo yote iko FUTUHI star tv achana na hao akina masanja, sasahivi ubunifu kwao ni negative(hawastahili hata sifuri).
 
PJ, kwani si usanii tu bana....labda na yeye Mengi anahukumiwa na mungu hapahapa duniani kwa kuwakashifu hadharani watu wazima wenziwe kwa kuwapa kesi na kuwahukum na kuwaita majina ya aibu huku akijuwa kuwa kuna vyombo husika vya kushughulikia madai hayo, na yeye kama mtu mzima,mheshimiwa alipaswa awaheshimu watuwazima wenzake,kushindwa kufanya hivyo kajiweka huru nayeye kukashifiwa na kukosewa heshima si tu na wakubwa zake bali hata watoto wadogo kama kina Masanja,mtenda akitendewa.....!!
 
1st Lady mdomo wa avatar yako..mmmh!!

basi iambie avatar!

1st Lady,

Kuna siku nilikuwa mtaani nikaona jarida fulani likiwa na picha unayotumia kama avatar yako.(kama nakumbuka vizuri tittle inasema "usilie kwa ajili yangu")
Siku nyigine nikaona kuna mtu kavaa T-shirt imeandikwa "NIKO KIZAZI" kama sijakosea.
Kwakweli nilivutiwa na hivyo vitu viwili nikasema siku moja nikiwa jamvini nitakuuliza.
Ninachotaka kujua ni je? , kuna uhusiano wowote kati ya wewe na hivyo vitu?
Kama jibu ni ndiyo basi HONGERA SANA.


Heshima mbele.
 
Kimsingi wale jamaa wa orijino komedi wameshaulia na hakuna vichekesho bali vijembe. Ni vema wakaanzisha bendi ya taarabu na wakapiga vijembe huko.

No one shoots a dead dog!! Ukiona wanashambulia ujue imewauma.

Hongera EATv
 
Hiyo kwenye mabano aliiweka Masanja au ya kwako?. Kama Masanja hakutaja jina la mtu basi sioni ubaya upo wapi. Maana Mtu si Mengi pekee, sisi sote ni watu.

Tusimuwekee masanja maneno mdomoni mwake. Cha kufanya mtafute umuulize alikuwa anamuongelea mtu yupi?. Then lete jibu tulijadili.

Nilitazama hicho kipindi tangu mwanzo hadi mwisho sikusikia jina la Mengi likitajwa.
 
Mjadala huu tusipokuwa makini unaweza leta mambo yasiyostahili, sasa masanja kuongea alivyojisikia kusema imekuwa ni Mengi anapewa hukumu? Je? nani anayejua hukumu yake? Binadamu mara nyingi tunaona tofauti za wenzetu ila za kwetu hatuzioni.
 
Kwani ze comedy au komedi whatever you pronounce it ni nini na ina impact gani kwa jamii na sector ya habari hapa tz? To others ni kama mchiriku na ngoma za mdundiko?
 
Tatizo ni kuwa kwa kuwa mengi ana hela basi haruhusiwi kutafuta nyingine kwa mtazamo wa Masanja , ITV walikuwa na program ya kutangaza habari saa mbili usiku TCB 1 nao walipoanza wanatangaza habari saa mbili usiku basi kwa mtazamo wa masanja TBC 1 ni chombo kikubwa lakini hovyo kwa kushindwa kutafuta muda mwingine wa kutanhfaza habari tofauti na ule wa itv na star tv?
 
Back
Top Bottom