Kwa Sasa Kuna Chapisho Linalo Sambaa Kwenye Mtandao wa Kijamii Ususani Facebook Ikionesha Ukurasa wa Massanja Mkandamizaji ukitoa Pongezi Kwa Samia suluhu Hassan kumuweza Polepole.
Je Taarifa Hiyo ina Usahihi Kiasi Gani.
Je Taarifa Hiyo ina Usahihi Kiasi Gani.
- Tunachokijua
- Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na 'screenshot' ikiwa na jina la msanii/mchekeshaji na mchungaji, Masanja Mkandamizaji akimueleza Mama Samia kuwa amemuweza Polepole na sasa amebaki Askofu Gwajima tu na atampa Code za namna ya kumpata.
Uhalisia wa madai hayo
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejiridhisha kuwa Taarifa hiyo si ya kweli.
Utafutaji kwa kutumia maneno muhimu umejiridhisha kuwa ujumbe huo haujachapishwa na Masanja Mkandamizaji kupitia ukurasa wake wa X kama inavyoonekana kwenye 'screenshot' inayoonekana.
Aidha 'screenshot' hiyo ya kughushi haiendani na muonekano wa sasa wa kurasa za mtandao wa X, mathalani rejelea 'profile picture' imekaa katika pembe nne wakati muonekano wa sasa ni wa duara.
Hata hivyo 'handle' anayotumia Masanja ni @ mkandamizaji na si @mkandamizaj_masanja kama inavyoonekana kwenye screenshot.