Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Gemini AI

Member
May 8, 2024
91
265
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema yeye binafsi atabeba gharama zote za matibabu ya Kijana Edgar Mwakabela (27) maarufu Sativa, kuanzia sasa mpaka atakapopona kabisa pamoja na kuhakikisha unafanyika uchunguzi wa tukio lililomtokea Kijana huyo ambaye hivi karibuni alikiri kuwa alitekwa Jijini Dar es salaam June 23,2024 na kupatikana akiwa amejeruhiwa usiku wa kuamkia June 27,2024 katika Hifadhi ya Katavi.

Taarifa iliyotolewa leo July 02,2024 na Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe imesema “Jana, July 01, 2024 nimepata nafasi ya kumtembelea Kijana aliyetekwa, kuteswa kwa kujeruhia vibaya kwa risasi kwa Sativa, nimezungumza na Sativa, Ndugu zake pamoja na Watu wanaomhudumia, tangu Katavi mpaka sasa, nimeuona umoja wa kitanzania kwenye jambo hili, nawashukuru wote waliomchangia na wanaondelea kuchanga, hivi ndivyo inavyopaswa kuwa, aliyoyapitia yanaumiza na kusikitisha sana, yaliyomtokea Sativa ni lazima tuyakomeshe”

“Baada ya kutoka Hospitali, nilifanya jitihada za kumtafuta Rais wa Tanzania, kuzungumza nae, kumuelezea tukio la Sativa kutekwa, kupigwa risasi, na kutupwa msituni Katavi, pamoja na matukio mengine ya Watu kupotea, ambayo yamekithiri katika siku za karibuni, nimemueleza, yeye kama Rais na Amiri Jeshi Mkuu anao wajibu wa kulinda usalama wa Raia, na kwamba matukio ya namna hii yanachafua taswira na haiba yake, na yanaondoa murua wa R Nne zake (4R's)”

“Nimemnasihi Ndugu Rais juu ya umuhimu wa yeye binafsi kuagiza ufanyike uchunguzi wa vyombo vya ulinzi na usalama ju ya tukio hili pamoja na mengine ya namna hii, kama Taifa tunahitaji kushirikiana pamoja kukomesha mambo ya Watu kutekwa, kuuawa, kupigwa na kutupwa misituni, yeye Rais anapaswa kuwa wa kwanza kwenye hili, Ndugu Rais amenisikiliza, na ameahidi kufanyia kazi ushauri wangu kwake”

“Kama hatua ya awali amenieleza kuwa yeye binafsi atabeba gharama zote za matibabu ya Sativa, kuanzia sasa mpaka atakapopona kabisa, pamoja na kuhakikisha unafanyika uchunguzi wa jambo hili, ninamshukuru Ndugu Rais kwa mwanzo huu, kila safari ndefu, inaanza na hatua ya kwanza, naamini sasa tutaanza safari ya kwenda kule tunakotaka, ambako tabia za kutekana zitakomeshwa”

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha Shilingi milioni 35 kwa ajili ya matibabu ya Edger Mwakabela maarufu Sativa ambaye anapatiwa matibabu katika hospitali ya Aga khan baada ya kupitia masaibu ya kutekwa na kuteswa.Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Wakili Onesmo Olengurumwa kupitia chapisho lake la karibuni alilolitoa katika ukurasa wake wa mtandao wa X (Twitter) ambapo amemshukuru Rais Samia kwa kutimiza ahadi kwa kulipia gharama za awali za matibabu ya Sativa."Tumepokea nakala ya malipo kiasi cha 35 milion kwenda Agakhan Hosptali.

Leo (Julai 02, 2024) jioni Sativa atafanyiwa upasuaji. Hizi ni gharama za awali tuombe kila kitu kiende sawa na gharama zisiwe kubwa huko mbele. Kuna faida kubwa kwa Mhe Rais kuweka mkono wake katika hili. Hii ni salamu kwa walioko nyuma ya swala hili" Ameandika Olengurumwa.Aidha ameeleza kuwa na tumaini na ushauri walioutoa kama THRDC wa kuundwa kwa tume huru itakayochunguza tukio lililomtokea Sativa huku akiwashukuru wadau waliosimama mstari wa mbele katika kuhakikisha Sativa anapata huduma bora kama vile Kiongozi Mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao ni Martin Masese na Boniface Jacob ambao walihakikisha taarifa za kupotea kwa Sativa zinajulikama ndani ya majukwaa ya kimitandao na nje ya majukwaa.
Pia soma

ACT.jpg
 
Kiongozi Mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema amemueleza na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan juu ya tukio la Edger Mwakabela maarufu kama Sativa kutekwa, kuteswa na kujeruhiwa vibaya kwa risasi na watu wasiojulika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ACT Wazalendo Julai 02, 2024, Zitto Kabwe alimtembelea Sativa aliyepo katika Hospitali ya Aga Khan akipatiwa matibabu na kuzungumza naye, na ndipo jitihada za kumtafuta Rais zikafanyika ambapo amemueleza Rais kama Amiri Jeshi Mkuu kuwa anao wajibu wa kulinda usalama wa raia.

Taarifa hiyo imeeleza zaidi kuwa

"Jana, tarehe 01 Julai, 2024 nimepata nafasi ya kumtembelea kijana aliyetekwa, kuteswa kwa kujeruhiwa vibaya kwa risasi, Ndugu Edgar Mwakabela, maarufu kama Sativa. Nimezungumza na Sativa, ndugu zake pamoja na watu wanaomhudumia, tangu Katavi mpaka sasa.

Nimeuona umoja wa kitanzania kwenye jambo hili, nawashukuru wote waliomchangia na wanaondelea kuchanga, hivi ndivyo inavyopaswa kuwa Aliyoyapitia yanaumiza na kusikitisha sana! Yaliyomtokea Sativa ni lazima tuyakomeshe

Mara baada ya kutoka hospitali, nilifanya jitihada za kumtafuta Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuzungumza naye, kumuelezea tukio la Sativa kutekwa, kupigwa risasi, na kutupwa msituni Katavi, pamoja na matukio mengine ya watu kupotea, ambayo yamekithiri katika siku za karibuni.

Nimemueleza, yeye kama Rais na Amiri Jeshi Mkuu anao wajibu wa kulinda usalama wa Raia, na kwamba matukio ya namna hii yanachafua taswira na haiba yake, na yanaondoa murua wa R Nne zake (4R's).

Nimemnasihi Ndugu Rais juu ya umuhimu wa yeye binafsi kuagiza ufanyike uchunguzi wa vyombo vya ulinzi na usalama juu ya tukio hili pamoja na mengine ya namna hii. Kama Taifa, tunahitaji kushirikiana pamoja kukomesha mambo ya watu kutekwa, kuuawa, kupigwa na kutupwa misituni, yeye Rais anapaswa kuwa wa kwanza kwenye hili.

Ndugu Rais amenisikiliza, na ameahidi kufanyia kazi ushauri wangu kwake. Na kama hatua ya awali amenieleza kuwa yeye binafsi atabeba gharama zote za matibabu ya Sativa, kuanzia sasa mpaka atakapopona kabisa, pamoja na kuhakikisha unafanyika uchunguzi wa jambo hili.

Ninamshukuru Ndugu Rais kwa mwanzo huu. Kila safari ndefu, inaanza na hatua ya kwanza. Naamini sasa tutaanza safari ya kwenda kule tunakotaka, ambako tabia za kutekana na kutesana zitakomeshwa.

Mungu Ibariki Tanzania.

ACT.jpg
 
Rais Samia kama kweli ana dhamira anatakiwa aagize waiohusika wote wakamatwe, kwa sababu wanafahamika, siyo kuchunguza, kwa sababu wanajulikana. Isije ikawa anajikosha kwa kujua kuwa uchafu wa Serikali yake umejulikana. Tujiulize, kama Sativa angekuwa amekufa na kuliwa na wanyama, na hivyo kukosekana kwa first hand information inayowataja polisi kuhusika, huo uchunguzi kweli ungefanyika?

Yaani Serikali iliyohusika kilutaka kumwua, baada ya kunusurika, inajifanya ina huruma ya kutaka kumtibu!!

Kama Samia kweli ana dhamira njema, aagize wahusika wote wakamatwe mara moja.
 
“Nimemnasihi Ndugu Rais juu ya umuhimu wa yeye binafsi kuagiza ufanyike uchunguzi wa vyombo vya ulinzi na usalama ju ya tukio hili pamoja na mengine ya namna hii, kama Taifa tunahitaji kushirikiana pamoja kukomesha mambo ya Watu kutekwa, kuuawa, kupigwa na kutupwa misituni, yeye Rais anapaswa kuwa wa kwanza kwenye hili, Ndugu Rais amenisikiliza, na ameahidi kufanyia kazi ushauri wangu kwake”
Kwahiyo Rais anaendeshwa kwa remote control yeye mwenyewe hajui yanayoendelea nchini mwake
 
Kuna jamaa mmoja alikuwa anasema hata kwa msiba wachawi huwa wanalia sana na akikuroga hadi Hospital anakuja kukuangalia unavyoteseka, anakupa na pole anakuletea na chakula.

Pia soma: Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na ‘watu wasiojulikana’

Wachawi wapo hivyo. Kusema Rais anagharamia matibabu ni uchawi tu huo huo kama wa miaka ya Kikwete. Aliyemteka Dr. Ulimboka mnajua alipelekwa wapi? Aliye muua Mwangosi?

Huo ni UNAFIKI!

Rais amuru waliofanya huo mnyama wakamatwe, wanajulikana. Si alipelekwa Oysterbay? Waanzie pale na mawasiliano yote.
 
Back
Top Bottom