MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,384
- 22,967
Nimesikitishwa sana na kauli yenye nia ovu kutoka kwa bibi Maria Sarungi kuwa Tundu Lissu hakulipwa stahiki zake hivyo inatupasa watanzania tuchange kumnunulia Lissu gari lingine (V8, VXR) ili kumrahisishia shughuli zake. Huo ni uongo kwa sababu Lissu mwenyewe alishakiri kulipwa stahiki zake zote na serikali ya awamu ya 6 chini ya Mama Samia. Soma uzi huo hapo.
- Tundu Lissu: Rais Samia amenilipa stahiki zangu nilizonyimwa na Magufuli
Kusema kwamba Lissu anakodisha gari kwa pesa nyingi ni uhuni mwingine wa CHADEMA chini ya Mbowe. Naibu mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani kukosa gari la kupewa na chama ni aibu isiyoelezeka. Michango ya Join The Chain ingetosha kununua gari la kiongozi kama Lissu. Mbowe anafakamia ruzuku kumbe kiongozi wake anakodi gari kwa pesa nyingi. Yale magari ya M4C huwa yana kazi gani kama Lissu hana gari. Au Lissu alikataa double cabin akataka LC300?
Ninawasihi watanzania msiingie kwenye huo uhuni wa kuchangia mambo ya kipuuzi. Lissu ni tajiri anayeweza kumudu kusomesha watoto Marekani na kuwahudumia kwahiyo hashindwi kujinunulia hata Prado ya 50m. Pia kama Mbowe aliweza kuchangisha zaidi ya Tsh 400m kumnunulia gari la kifahari Askofu wa chama chake hashindwi kukusanya matajiri wenzake na kuwachangisha 400m kumnunulia Lissu gari la kifahari baada ya kusumbua nyumbu wenye hali ngumu kimaisha.
Kwenye maandamano yenu mmekuwa mkiongelea ugumu wa maisha sasa inakuwaje mnataka kuwakamua tena wananchi hela zao kidogo ili kumfurahisha Lissu kwa gari la anasa? Nyie mkiingia madarakani mtakuwa wabaya mara 10 ya CCM mnaotulaumu.