Maria Sarungi ni mwanaharakati kutoka nchiniTanzania, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za binadamu, utawala wa kisheria unaozingatia misingi ya kidemokrasia. Kadhalika Maria amekuwa akijihusisha na masuala mbalimbali ya harakati za kisiasa kwa kipindi kirefu sasa, ambapo amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kuendsha harakati zake ikiwemo X awali ukijulikana kama twitter.
Madai
Kumekuwapo na taarifa zinazomuhusisha Maria Sarungi, zikidaiwa kuchapishwa na
ITV, pamoja na
East Africa Radio kuwa Mwanaharakati huyo amesuka mipango ya CHADEMA kuvamia mahakamani tarehe 24
Uhalisia
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu (Key Word Search), imebainika kuwa Taarifa hiyo si ya kweli, kwani haikuchapishwa katika kurasa za ITV pamoja na East Africa Radio kama inavyoonekana katika machapisho hayo.
Aidha taarifa hiyo imebainika kuwa ni ya kutengenezwa kwani machapisho husika yana mapungufu ambayo yanatofautisha na machapisho rasmi ambayo huchapishwa katika kurasa rasmi za vyombo hivyo. Chapisho lililotumia utambulisho wa ITV sehemu ya kichwa cha habari inaonesha kufutwa kwa maandishi ya awali na kuandikwa maneno hayo, jambo lililoharibu muonekano wa picha (backgroung) iliyo nyuma ya maandishi hayo.
Chapisho linalodaiwa kuchapishwa na Clouds Media
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa Chapisho hilo si la kweli, ni la kutengenezwa kwani halijachapishwa na
Clouds media kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii. Chapisho hilo linaonesha lilihaririwa kwa kuwekewa picha ya
Tundu Lissu na
Sheikh Issa Ponda juu ya picha ilikuwapo awali katika chapisho hilo.