Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,566
Ikulu ya White House ya Marekani, imesema kuwa Urusi inaendelea na mazungumzo ya siri na Korea Kaskazini ili kupata risasi na nyenzo nyingine za kivita dhidi ya Ukraine.
Mtandao wa BBC umeripoti kuwa msemaji wa usalama wa taifa hilo, John Kirby, amesema kuwa pamoja na vifaa vya kijeshi, Moscow inaweza pia kuingia katika mikataba ya kununua malighafi ili kuipatia sekta yake ya ulinzi.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield alizikosoa Urusi na Korea Kaskazini.
“Katika harakati zake za kutafuta silaha hizi, Urusi itakiuka maazimio ya Baraza la Usalama, yakiwemo yale ambayo Urusi yenyewe iliyapigia kura.
Mkataba wowote wa silaha kama huo utakuwa ukiukaji mkubwa wa azimio la Baraza la Usalama lililopitishwa kwa kauli moja baada ya majaribio ya nyuklia ya Korea Kaskazini na kurusha makombora ya balestiki," Linda Thomas-Greenfield amesema.