Marekani yatangaza vikwazo vya viza dhidi ya Maofisa wa Somalia

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Marekani imetangaza vikwazo vya viza dhidi ya maafisa wa sasa au wa zamani wa Somalia wanaotuhumiwa kuhujumu michakato ya kidemokrasia.

Hatua hiyo inakuja wakati ambapo Marekani inasukuma kufanyika kwa uchaguzi wa kuaminika nchini Somalia - ambao umechelewa kwa muda mrefu.

Katika taarifa, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alisema vizuizi vya visa vinatumika kwa watu “ambao wameshindwa kutekeleza majukumu yao ya kutekeleza uchaguzi kwa wakati na wazi“.

Pia vinalenga maafisa ambao “wamewalenga waandishi wa habari na wanachama wa vyama vya upinzani kwa unyanyasaji, vitisho, kukamatwa na vurugu“.

Somalia imeahirisha uchaguzi tangu mamlaka ya Rais Mohamed Abdullahi Farmajo yalipokamilika Februari mwaka jana.


Chanzo: Star TV
 
Back
Top Bottom