Marekani chini ya Trump ni unguided missile. Hapa Trump amehongwa na matajiri wanaofanya biashara ya mafuta ili akimuwekea vikwazo Iran mafuta yanapanda bei yafike pipa moja dola 80 hata kama ni kwa mwaka mmoja wataingiza fedha nyingi. Shida ya kushindana na Marekani ni kuwa ndo mnunuzi mkubwa wa bidhaa zaChina ,na China ndio mpinzani mkubwa wake kiuchumi. Kumbana Kim wa Korea amemuweza baada ya kupandisha kodi bidhaa za China kisha kaiambia China usipomdhibiti dogo tutatoza kodi zaidi bidhaa zako. China akamwambia dogo ahirisha hayo makombora, ndipo dogo akanywea ,.Itachukua muda kumdhibiti Marekani na Sera zake za ubabe. Lakini Marekani si taifa LA kushabikia, maana hivi mafuta yakipanda yeye ndio anafaika sana ,maana sasa hivi ndio mzalishaji mkubwa ingawa hauzi nje, Lakini mafuta yakishuka dola 50 kwa lita viwanda vyake vya Cracking Shale Oil vinakosa faida na vilianza kufungwa, sasa ili viende kwa faida lazima aanzishe vagi sehemu inayozalisha mafuta mengi kama Iran uzalishaji ushuke na bei ipande duniani . Sisi tutulie huku dunia ya tatu hamna mwema kwetu wote wanalinda maslahi yao . Sana tukishabikia tuna maana nani atatupa makombo zaidi baada ya kula akavimbewa. Huo ndio ukweli.