UONGO MTUPU NA FULL OF FABRICATION KAMA ZA DICTATOR ERDOGAN WA UTURUKI !
Mji wa Israel ulianzishwa na Mfalme Daudi zaidi Miaka 3000 iliyopita yani miaka 1000 kabla ya Yesu ambapo ni sehemu Ibrahim Isaka na Yakobo walifanya ibada.
Mwaka 586 kabla ya Yesu Wababiloni walilibomoa hekalu la kwanza na wayahudi wakakimbia kujificha lakini wakarudi muda siyo mrefu mwaka 516 kabla ya Yesu.
Miaka 500 baadae yaani mwaka 70 baada ya Yesu Warumi wakalibomoa hekalu la pili la Yerusalem,katika miaka iliyofuata Falme mbali mbali mbali kama Rumi,Byzantine,Persian,Arabs,Seljuks,Cruseders,Ottoman, British na nyingine zimekua zikivamia Yerusalem lakini siyo kufanya Yerusalem kuwa makao makuu yao
Mwaka 985 baada ya Yesu mwandishi maarufu kutoka Uarabuni Muhammad ibn Ahmad Shams al Din al -Muqaddasi aliandika kitabu akilalamika kuwa wayahudi wana idadi kubwa ya watu pale Jerusalem kuliko jamii yoyote.
Mwaka 1864 bado Wayahudi waliendelea kuwa wengi kuliko jamii yoyote pale Yerusalem kama takwimu zilizotolewa na British Consul of Jerusalem(Noel Temple Moore) mwaka 1864 Wayahudi wakiwa 8000,Waislam wa kiarab 4500,na Wakristo 2500.
Wayahudi hata wakiwa uhamishoni au sehemu yoyote duniani,maombi yao na sala zao zilikua zinaonyesha tumaini la kurudi Yerusalem
Waislam na dini yao iliyoanzishwa miaka 1400 iliyopita wakiwa popote walipo duniani hata walioko Yerusalem swala zao na ibada zao wamekua wakitazama Macca.Macca na Medina ni miji mitakatifu kuliko Yerusalem kulingana na uislam.
Yerusalem haijatajwa moja kwa moja kwenye quran wakati biblia imetaja Yeusalem mara 669.
Nini kilitokea mwaka 1967,kwanza kabisa hakukuwa wala halijawai kuwepo taifa au nchi ya Palestina.Mwaka 1948 Jordan iliteka eneo la Yerusalem mashariki na kuikalia kimabavu, kuwafukuza Wayahudi na kubomoa makazi yao,Yerusalem magharibi ikawa ni makao makuu ya Israel huku Jordan makao makuu yake yakiwa ni Aman.Katika ile vita ya siku 6 mwaka 1967 Israel ikaifukuza Jordan na kuunganisha Yerusalem.Hii ndio historia ya ukweli.