Marekani yashindwa kuelewa mafanikio ya kiteknolojia ya nchini China

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,035
VCG111455096243.jpg
Linapokuja suala la maendeleo mapya ya utengenezaji wa chips nchini China, vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti hivi karibuni kuwa, haitakuwa ajabu kwa Marekani kuongeza nguvu ya vikwazo na kuimarisha hatua za kupunguza kasi ya ueneaji wake, lakini, daima biashara italazimisha ubunifu wa siri mpya za kiteknolojia.

Hii inaonekana kuwa tabia ya Marekani ya kutokubali kukiri maendeleo ya teknolojia ya China, na kuamini kuwa uwezo wa China bado haujafikia vigezo, na kwamba nchi hiyo inaweza kuendelea tu kwa kutegemea hakimiliki ya ubunifu yaw engine ama siri za kiufundi.

Kimsingi, maoni kama hayo yanaangalia maendeleo ya teknolojia ya dunia kutoka kwenye nadhari ya kibaguzi, kama vile maendeleo kidogo ya teknolojia ya nchi nyingi nyingine inatokana na wizi ama siri zilizovuja za Marekani, bila hivyo, haiwezekani kabisa kwa nchi nyingine kufanya uvumbuzi. Lakini kihalisi, uwekezaji wa China katika utafiti na maendeleo, ukiwakilishwa na Huawei, umekuwa ukiongoza dunia kwa miaka mingi.

Katika Makala yake, kampuni ya Bloomberg ilitoa mifano ya kuthibitisha kuwa hakuna anayehodhi uvumbuzi. Zamani, China ilikuwa imeendelea sana katika utengenezaji wa hariri, kutengeneza karatasi na vyombo vya kauri, lakini baadaye walitambulishwa kwa dunia ya Magharibi. Hivyo, uvumbuzi wa semiconductor ya Huawei ni sehemu tu ya historia ndefu ya ueneaji, ama wizi ukipenda, wa kile ambacho kinaitwa hakimiliki ya ubunifu. Sasa je, vyombo vya habari vya Marekani vinafikiria kuhusu ufafanuzi huu kutokana na mtazamo wa kihistoria na kuweza kuwafanya wasomaji wake kukubaliana na kile kinachoitwa ‘wizi wa hakimiliki ya ubunifu?’

Utandawaza umeleta kuenea kwa ufahamu na baadhi ya teknolojia duniani, hata hivyo, kila mtu anayemudu teknolojia anataka kuidhibiti, na kuna kesi chache za kubadilishana kihalisi teknolojia. Na hii ni bila kuzungumzia sheria ya haki ya ugunduzi na hakimiliki ya ubunifu ili kulinda maslahi ya wabunifu katika jamii ya sasa.

Kuhusu hili, mhadhiri katika Akademia ya Sayansi ya Jamii ya China, Lu Xiang, anasema kama nchi yoyote inataka kutimiza maendeleo kupitia uenezi wa kawaida wa teknolojia, itakuwa ama ni ngumu, ama haina maana kusubiri mpaka teknolojia hiyo itakapopitwa na wakati. Lu anaamini kuwa, China, na kampuni zake, ikiwemo Huawei, zimeendeleza baadhi ya teknolojia ambazo ni za juu zaidi kuliko zile za kampuni za Marekani. Sasa, ingawa Marekani imeweka vikwazo kadhaa vya kiteknolojia kwa China, China bado inategemea juhudi zake yenyewe kuendelea kujipatia upenyo. Kinyume na hapo, Marekanim nchi kubwa inayopeleleza nchi nyingine duniani, inaendelea kusisitiza ulinzi wa hakimiliki za ubunifu, huku ikiendelea kutumia njia za kimwamba kukandamiza kampuni zinazoendelea za nchi nyingine.

Inashangaza sana kwamba vyombo vya habari vya Marekani vinashutumu uvumbuzi huru wa China kuwa ni ‘upotokaji’ na ‘uchokozi,’ na wakati huohuo, kutetea ‘vizuizi vya kiufundi.’ Ni wazi kwamba, Marekani inataka kudumisha mamlaka yake inayoonekana katika Nyanja zote, ikiwemo teknolojia, lakini hakuna nchi inayoweza kuzuia maendeleo ya teknolojia mpya yanayofanywa na kampuni ya nchi nyingine, na hakuna kampuni yoyote duniani inayoweza kuongoza dunia kupitia wizi.

Kama Marekani ikiendelea na mtazamo wake huo potofu, ni wazi kuwa haitafanikiwa. Nchi zote duniani zinaunganika katika zama hizi za utandawazi, ambazo zinaweka wazi kuwa, aina hii ya mtazamo haitfanya kazi kamwe. Zaidi, kuboresha kwa pamoja maendeleo ya sayansi na teknolojia kupitia ushirikiano ni mwelekeo ambao Marekani haiwezi kuupinga.
 
Moja kati ya nchi ambazo wananchi wake wamekua so brainwashed na Media zao ni Marekani

Serikali ya Marekani imefanikiwa (kupitia Propaganda) kuwaaminisha wamarekani kuwa nchi yao ni ya kipekee (Exceptional), imuruhusiwa na Mungu kutetea uhuru, usawa na demokrasia, kila mtu anataka kuja kwao mpaka Aliens, Bullshit

Asilimia kubwa ya Wamarekani haswa hao Wamarekani weupe, wanaamini kutoka moyoni kwenye hio Propaganda

So serikali yao inachofanya ni kuwambia kila siku yupi Adui wa uhuru, usawa na demokrasia

Mwanzo ilikua Native Americans, then wakawa African Americans, then U.S.S.R, hapa katikati walivyobaki wao tu wakatengeneza adui mwingine wa Ugaidi wakaenda kufanya fujo Middle East nzima mpaka North Africa, then now ni China.

Huwezi kuwa na dunia ya amani ukiwa na nchi kama Marekani kwenye usukani wa siasa za kimataifa, Dunia haiwezi kua na amani

Kushangaa kwanini China wamefanikiwa kwenye Chip ni habari ya kijinga, fungia Mathematicians, Engineers, Physicists, na Chemists wa viwango vya juu, weka budget na resources za kutosha na watakuja na invention yoyote ile as long as inaruhusiwa na sheria za fizikia

Hakuna anayehodhi Elimu, wao ni waanzilishi wa A.I na bado China ndiyo anayewaongoza kwenye A.I

Kushangaa why China ameweza ni mjadala wa kijinga
 
Bado hujasema na utassema iyoo ni ukubali au ukatae ulayaa wameshoosha mikono tayri wewe mmatumbi wa rufiji unabaki kubwabwaja
Unaweza kuta Uchina au Amerika ujawahi kufika.
Ukifika kwenye automated industries nyingi za Uchina watakuonesha tu ...In this production line we are using UK technology, this line we are using more technology from Japan.
Jamani, usidhani kuna urahisi sana kwa Uchina kuifikia West and US kwenye Tech, au wewe ushangai wanafunzi na watafiti wengi wa Uchina wanakwenda sana kusoma vyuo vya US na Ulaya zaidi ya Kinyume chake?
 
Marekani ni jahazi linalozama fikiria wamewaonea wivu wahindi kupeleka chombo mwezini kwa mara ya kwanza duniani na hawatangazi kwenye media zao ila wanaoshutumu india kwanini wameenda mwezini wakati wanapewa misaada na Marekani.

Imagine Marekani wali fake moon landing wakadanganya dunia nzima wamefika mwezini kumbe uongo

Mmomonyoko wa maadili na sifa za kijigamba na kumwaga damu za watu zimefanya dunia iwachukie sana hawa Marekani
 
Back
Top Bottom