Msambichaka Mkinga
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 1,646
- 2,911
Safi waambie hao wa Lumumba. wamekaa kwenye key board tu. ombeni safari moja ya Marekani mbadilishwe akili zenu
Huwezi kumjua maskini mpaka umwone tajiri kwanza.
Kule Marekani kulipotokea kimbunga, kuna bandari moja ilifungwa. Mapato yake kwa siku bandari ile ambayo si moja ya bandari kubwa za Marekani ilikuwa ni dola milioni 400. Tanzania tuna nini mpaka sasa kinachokaribiana angalao na hicho? Umaskini wetu utaondoka kwa mipango thabiti siyo kwa kelele hizi za kusema sisi ni matajiri, Marekani imesalimu amri, n.k.
Ukiwa mjinga na unataka kuifurahisha nafsi yako, hata leo unaweza kusema, 'mimi ni tajiri kama Bakhresa, kuna siku Dangote atanipigia magoti', lakini hiyo haitabadilisha umaskini wako, na wala haitabadilisha utajiri wa Dangote au Bakhresa. Umaskini wako utaondoka kwanza kwa kukiri kuwa wewe ni maskini kuliko hao matajiri, na baadaye kwa kuwa na mipango thabiti ya kuondoka mahali ulipo.
Mpaka leo hii, hapa mahali tulipo, na kwa mwendo tunaoenda nao, kwa kadiri ya taarifa za UNDP, itatuchukua miaka 250 kuifikia Malaysia (wao wakiamua kubakia walipo!) ilipo leo ingawa miaka ya 1960 tulikuwa tunalingana kwa umaskini. Hiyo ni Malaysia wala siyo Marekani.
Hata tukijitahidi vipi watakaoifikia Marekani siyo hiki kizazi chetu. Maendeleo ni process, hulali na kuamka ukashtukia umeendelea. Tulipotea njia mwanzoni. Hata tukiipata njia leo ni lazima tuanze safari, na baadaye tufike tunakotaka kwenda.Safi waambie hao wa Lumumba. wamekaa kwenye key board tu. ombeni safari moja ya Marekani mbadilishwe akili zenu