Domo Kaya
JF-Expert Member
- May 29, 2007
- 531
- 59
Yasema itasiaidia kurejesha fedha zilizoibwa BOT.
MWANANCHI
NA DENNIS MSACKY.
Balozi wa Marekani nchini, Mark Green amesema kwamba serikali ya nci yake inaweza kumrejesha aliyekuwa Gavana wa Benki kuu ya Tanzania (BOT) Daudi ballali endapo serikali ya Tanzania itaomba arejeshwe.
Akizungumza na wahariri wa baadhi ya vyombo vya habari jana jijini Dar es salaam,Balozi huyu alisema suala la kumrejesha Ballali nchini kwa ajili ya kujibu tuhuma za ufisadi wa babilioni ya fedha uliofanyika BOT uko mikononi mwa serikali ya Tanzania.
"kwanza kabisa hatuna uhakika kwamba Ballali yuko Marekani, lakini hata hivyo ni wajibu wa serikali kutuambia kama wanataka kumrejesha na sisi tutawasaidia kufany hivyo", alisema balozi huyo.
Alisema tokea awali nchi yake ilishasema kwamba itashirikiana na Tanzania katika vita yake dhidi ya rushwa hivyo wako tayari kumrejesha Ballali kama yuko Marekani kwa matibabu au kwa shughuli zozote.
Viongozi wa serikali na wa BOT wamenukuliwa mara kwa mare wakisema kwamba Ballali yuko nchini Marekani kwa ajili ya matibabu, lakini wameshidwa kutaja hospitali anayotibiwa jambo ambolo limekuwa likizua maswali mengi kuliko majibu.
Kwa nyakati tofauti, pia ubalozi wa Marekani nchini umenukuliwa ukisema kwamba umekuwa ukisoma kwenye vyombo vya habari kuhusiana na Ballali kuwepo nchini Marekani, lakini hauna uhakika.
Pia kumekuwa na madai kwamba Ballali ni raia wa Marekani, licha ya kufutiwa viza alipopewa kwa wadhifa wake wa gavana wa BOT.
Akizungumzia hiyo balozi Green alisema kwamba kama Ballali angekuwa raia wa Marekani basi asingweza kuomba visa .
"Hakuna raia wa Marekani ambaye anaomba visa na hana haja ya kuomba visa hivyo Ballali si raia wa Marekani . Visa ya Ballali aliiomba mwaka jana". Alisema balozi huyo.
Kabla ya kujerea Tanzania Ballali alikuwa akifanya kazi nchini Marekani kwa zaidi ya miaka 20 katika mashirika ya kimafaifa. Ballali aliondoka nchini miaka ya 70 kwenda Marekani wakati huo akiwa Mkurugenzi wa Utaifa wa BOT.
Kuhusiana na nchi ya Marekani kusaidia kurejesha fedha zilizoibwa BOT kama zimeweka katika mabenki ya nchi hiyo, Balozi alisema kwamba nchi yake ipo tayari kufanya masako katika mabenki na kurejesha fedha zote ambazo zitabainika kwamba zilichukuliwa BOT.
"Marekani itasaidia kutafuta fedha zote ambazo zimeibwa na kuzirejesha nchini , hiyo ni sera yetu kwamba haturuhusu fedha za aina hiyo kuwepo katika nchi yetu.