Marekani: Serikali Ikimtaka Daudi Ballali Tutamrejesha

Domo Kaya

JF-Expert Member
May 29, 2007
531
59
Yasema itasiaidia kurejesha fedha zilizoibwa BOT.

MWANANCHI
NA DENNIS MSACKY.

Balozi wa Marekani nchini, Mark Green amesema kwamba serikali ya nci yake inaweza kumrejesha aliyekuwa Gavana wa Benki kuu ya Tanzania (BOT) Daudi ballali endapo serikali ya Tanzania itaomba arejeshwe.

Akizungumza na wahariri wa baadhi ya vyombo vya habari jana jijini Dar es salaam,Balozi huyu alisema suala la kumrejesha Ballali nchini kwa ajili ya kujibu tuhuma za ufisadi wa babilioni ya fedha uliofanyika BOT uko mikononi mwa serikali ya Tanzania.

"kwanza kabisa hatuna uhakika kwamba Ballali yuko Marekani, lakini hata hivyo ni wajibu wa serikali kutuambia kama wanataka kumrejesha na sisi tutawasaidia kufany hivyo", alisema balozi huyo.

Alisema tokea awali nchi yake ilishasema kwamba itashirikiana na Tanzania katika vita yake dhidi ya rushwa hivyo wako tayari kumrejesha Ballali kama yuko Marekani kwa matibabu au kwa shughuli zozote.

Viongozi wa serikali na wa BOT wamenukuliwa mara kwa mare wakisema kwamba Ballali yuko nchini Marekani kwa ajili ya matibabu, lakini wameshidwa kutaja hospitali anayotibiwa jambo ambolo limekuwa likizua maswali mengi kuliko majibu.

Kwa nyakati tofauti, pia ubalozi wa Marekani nchini umenukuliwa ukisema kwamba umekuwa ukisoma kwenye vyombo vya habari kuhusiana na Ballali kuwepo nchini Marekani, lakini hauna uhakika.

Pia kumekuwa na madai kwamba Ballali ni raia wa Marekani, licha ya kufutiwa viza alipopewa kwa wadhifa wake wa gavana wa BOT.

Akizungumzia hiyo balozi Green alisema kwamba kama Ballali angekuwa raia wa Marekani basi asingweza kuomba visa .

"Hakuna raia wa Marekani ambaye anaomba visa na hana haja ya kuomba visa hivyo Ballali si raia wa Marekani . Visa ya Ballali aliiomba mwaka jana". Alisema balozi huyo.

Kabla ya kujerea Tanzania Ballali alikuwa akifanya kazi nchini Marekani kwa zaidi ya miaka 20 katika mashirika ya kimafaifa. Ballali aliondoka nchini miaka ya 70 kwenda Marekani wakati huo akiwa Mkurugenzi wa Utaifa wa BOT.

Kuhusiana na nchi ya Marekani kusaidia kurejesha fedha zilizoibwa BOT kama zimeweka katika mabenki ya nchi hiyo, Balozi alisema kwamba nchi yake ipo tayari kufanya masako katika mabenki na kurejesha fedha zote ambazo zitabainika kwamba zilichukuliwa BOT.

"Marekani itasaidia kutafuta fedha zote ambazo zimeibwa na kuzirejesha nchini , hiyo ni sera yetu kwamba haturuhusu fedha za aina hiyo kuwepo katika nchi yetu.
 
Haya sasa ndugu zangu, Mh. Rais yeye alijua anaanzisha hili kujisafisha kisiasa na kurudisha matumaini kwa wananchi, ila sasa jambo limekwa serios, na sio lakisiasa tena. TUNASUBIRI KUSIKIA Mh. AKIWAAMBIA WAMAREKANI WAMRUDISHE BALLLALI NA TUONE ITAKUWAJE.
 
Simba wa kuchora, ukweli ni kwamba hata serikali yetu haijui Balali yuko wapi, halafu hawa US waache unafiki mbona hawalilii kina Mramba, Mgonja, na Mama Meghji kukamatwa kwani repoti si iko clear walioiba ni nani? Wanyamaze tu, maana sasa I am getting the juice ni Balali peke yake ndio mwenye final desicion ya what happens next, wengine wote waongo ndugu zangu tunadanganywa tu!

Balali 3, Mafisadi 2, Wananchi 0!
 
Mhh lets hope dat he meant what he said isije ikawa longolongo, si mnakumbuka tume ya Mzee Warioba na mianya ya rushwa! hatari
 
Simba wa kuchora, ukweli ni kwamba hata serikali yetu haijui Balali yuko wapi, halafu hawa US waache unafiki mbona hawalilii kina Mramba, Mgonja, na Mama Meghji kukamatwa kwani repoti si iko clear walioiba ni nani? Wanyamaze tu, maana sasa I am getting the juice ni Balali peke yake ndio mwenye final desicion ya what happens next, wengine wote waongo ndugu zangu tunadanganywa tu!

Balali 3, Mafisadi 2, Wananchi 0!

Mimi ninachodhani ni kwamba Serikali inajua Ballali yupo wapi haitaki kusema cos imetupiga bao la kisigino na ndio maana tume imeunda ya miezi sita ndio tupewe jibu la nini hatma ya hawa mafisadi.

Kuhusu Wamerakani mimi sidhani kama ni wanafki, Serikali kila siku inadai Ballali yupo marekani kwa matibabu, sasa wao wameona bora waseme kama serikali itataka Ballali arudishwe Tanzania na ina uhakika kwamba yupo Marekani basi wao watamrudisha ili aje ajibu tuhuma zake.

Tatizo lipo kwa Serikali yetu iseme ukweli Ballali yupo wapi????

Je ni kweli yupo Marekani? kama kweli liwaruhusu wamarekani wamrudishe?????

Na je hivi Ballali yupo hai au wamesham-restisha in peace?

Au wanadhani baada ya hiyo miezi sita(6) Ballali ndio atakuwa Ame-rest in peace ndio watoe majibu ya nini hatma ya hao mafisadi cos maiti haiwezi kujitetea????

Inabidi Watanzania tujiulize maswali kwanza.
 
Mkuu nilikuwa ninajaribu kuifuatilia hii ishu, nikaamua kuacha baada ya kukuta ukweli kibao ambao hausemwi wazi, ikiwa ni pamoja na serikali yetu kutojua Balali yuko wapi hiyo ni fact mkuu, wala serikali yetu ilikuwa haijui kuwa balali ana Green Card, Ni uzushi mkubwa kuwa eti RO alienda kuonana naye huko US, serikali ya US haiwezi ngo' kumrudisha bongo Balali kama yupo US,

My conclusion, ni kwamba Balali sasa hivi ndiye mwenye total control ya fate yake, na ninaaamini kuwa hatarudi bongo not soon!
 
Nashauri waliokwapua BoT, wasianze kama balali, bali waende PSRC wakaonyeshwe mashirika ya kununua kisha wawekeze humu ndani!!!

bora nusu hasara wajameni!!!!

Haki ya nani, wazungu watamkamata na kumrudisha balali, only kama hana mshiko wa nguvu lakini kama bado ana mafweza yote hayo, harudishwi ng'ooo!!

Hivi mwadhani, kina mabutu pesa zao walitunziwa na kina nani??? wazungu hawakujua kama mabutu hana mshahara wala biashara ya kumkusanyia mapesa yote hayo?? kwa taarifa yenu, viongozi walioongoza kwa ubadhilifu afrika ni wale watawala wa mwanzo (maliojidai eti wameleta uhuru) afrika. ndio walioiweka afrika hapa. wote walikumbatiwa na wazungu hao hao, either wa west or east!!

Namsikitikia asemae wamarekani si wanafiki!!!!
 
Kwani huyu Balali kashitakiwa? katuhumiwa na serikali au simply kafukuzwa kazi tuu? mie nimichanginyikiwa, nisaidieni nielewe.
 
mh, kazi ipo

Mkuu Domo Kaya,

Ninaiheshimu sana kazi yako bongo ya kulilia mabadiliko muhimu kisiasa na kisheria, na pia uwajibikaji, ninatka ujue kuwa mimi ni a big fan wa article zako na huwa ninazifuatilia sana kwa ukaribu na makini, maana huwa huchanganyi maneno wala kupunguza,

Kuhusu hii ishu ya Balali na wa-US, habari sio za kweli kabisa zinazoandikwa hapa bongo, na kuhusiana na serikali na hii ishu ndio kabisaa hakuna ukweli hata chembe, kwa hiyo mkuu wangu usiangukie mtego huo wa panya,

Huyo mkuu harudi leo, na what happens to him next ni uamuzi wake, US hawana ubavu wa kumuondoa, so far wanaimba tu filimbi maaan ACLU wakiwasikia itakuwa kasheshe ya mwaka kwamba wanamtishia African, mwenye green card na mke mwenye permanent residence huko US, itasemwa kuwa ni ubaguzi, mkuu wafungwa wa-Taliban wanapewa haki huko Guantanma Bay, iatkuwa Balali mtu huru ambaye hajavunja sheria za US, wala kushitakiwa na serikali ya bongo? Achana na hizi porojo mkuu wangu, hiii ishu ni complicated mno kuliko inavyosemwa mkuu.

Ahsante Mkuu!
 
Kwani huyu Balali kashitakiwa? katuhumiwa na serikali au simply kafukuzwa kazi tuu? mie nimichanginyikiwa, nisaidieni nielewe.
Amefukuzwa kazi na bosi wake..na anatakiwa arudi kujibu mashtaka mahakamani..nini kigumu kuelewa hapo?
 
Mkuu Domo Kaya,

Ninaiheshimu sana kazi yako bongo ya kulilia mabadiliko muhimu kisiasa na kisheria, na pia uwajibikaji, ninatka ujue kuwa mimi ni a big fan wa article zako na huwa ninazifuatilia sana kwa ukaribu na makini, maana huwa huchanganyi maneno wala kupunguza,

Kuhusu hii ishu ya Balali na wa-US, habari sio za kweli kabisa zinazoandikwa hapa bongo, na kuhusiana na serikali na hii ishu ndio kabisaa hakuna ukweli hata chembe, kwa hiyo mkuu wangu usiangukie mtego huo wa panya,

Huyo mkuu harudi leo, na what happens to him next ni uamuzi wake, US hawana ubavu wa kumuondoa, so far wanaimba tu filimbi maaan ACLU wakiwasikia itakuwa kasheshe ya mwaka kwamba wanamtishia African, mwenye green card na mke mwenye permanent residence huko US, itasemwa kuwa ni ubaguzi, mkuu wafungwa wa-Taliban wanapewa haki huko Guantanma Bay, iatkuwa Balali mtu huru ambaye hajavunja sheria za US, wala kushitakiwa na serikali ya bongo? Achana na hizi porojo mkuu wangu, hiii ishu ni complicated mno kuliko inavyosemwa mkuu.

Ahsante Mkuu!
IFUATAYO NI KAULI YA BALOZI WA MAREKANI TZ;Hata hivyo, alisema wao wako tayari kumsaidia Rais Jakaya Kikwete kushughulikia ombi litakalofanikisha utekelezaji wa azma hiyo kama ipo.
 
Tunaweza kuunganisha hii na ile ya "JK akataa Balali asirudi"..?
NO!WAZEE HII ISIUNGANISHWE!KWANI KIONGOZI WA SERIKALI SI NI KIKWETE?NA KAMA HAJAKATAA MBONA MAREKANI WANASEMA HAJAWAULIZA?NA KAMA HAJAWAULIZA..KWANINI ASITUELEZE NI KWANINI HAMTAKI BALALI TANZANIA?SPIN IKO WAPI HAPO?
 
Mara ya kwanza nilianzisha thred hapa ya kutaka serikali ishinikizwe..ikaunganishwa na nyingine..anyways mantiki bado ni ileile..Mimi hapa nina mtazamo wa tofauti na ninataka hoja kwa hoja!Nilitangulia kusema kwenye thred ile ya mwanzo kwamba kuna juhudi za kuzishinikiza serikali za magharibi ili kumbana Kikwete kawasababu ndio watu anaowasikiliza!Kuliko wananchi wake!Sasa Marekani wamerespond..wamesema Kikwete hajawataka wamrudishe..sasa spin iko wapi?Kikwete ndio attueleze ni kwanini alimfukuza Balali wakati hana makosa!
 
Kikwete hawezi kutoa tamko kwa serikali ya Marekani wamrudishe Ballali Tz kwa sababu hizo hela sio Ballali aliyehusika na kuzitafuna ila yeye (Ballali) alikuwa napewa order na wakubwa wake. Sasa kama Ballali atarudishwa TZ na akasema ukweli wa hali ilivyokuwa wengi watajikuta wamo matatizoni akiwome Rais Kikwete mwenyewe.

Yeye alidhani anaigiza kwenye maisha halisi sasa wananchi nao wamecharuka hawataki maigizo.
 
Mnaikumbuka hii, serikali ilisema ikimtaka Balali itamrudisha, sasa wameshindwa kurudisha hata maiti yake.
 
Mnaikumbuka hii, serikali ilisema ikimtaka Balali itamrudisha, sasa wameshindwa kurudisha hata maiti yake.

Ndo maana serikali inabidi ijisafishe maana haiwezekani kusema kuwa wakimtaka watamrejesha halafu washindwe hata kuwadhibitishia watanzania kuwa kweli amekufa, kuna ujanja unatumika hapa.
 
Back
Top Bottom