Marekani: Mwanamuziki R. Kelly akutwa na hatia ya kunyanyasa watu kingono

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Mwimbaji wa Marekani R Kelly amepatikana na hatia ya kutumia hadhi yake ya kuwa nyota wa muziki wa R&B kuendesha mpango wa kuwadhulumu kingono wanawake na watoto kwa zaidi ya miongo miwili.

Walalamishi 11, ikiwemo wanawake tisa na wanaume wawili, walitumia wiki sita kuelezea udhalilishaji wa kingono na ghasia walizokumbana nazo mikononi mwake.

Baada ya siku mbili ya majadiliano, jaji alimpata R Kelly na hatia katika mashtaka yote yaliyokuwa anakabiliwa nayo.

Hukumu dhidi yake itatolewa Mei 4 na huenda akafungwa maisha.

Majaji walimpata Kelly, ambaye jina lake kamili ni Robert Sylvester Kelly, kuwa kiongozi wa mpango hatari uliyowavutia wanawake na watoto na hatimaye kuwanyanyasa kingono.

Mwimbaji huyo - maaarufu wa wimbo wa I Believe I Can Fly ulioshinda tuzo - pia aligundulika kuwasafirisha wanawake kati ya majimbo tofauti ya Marekani na kuandaa filamu ya ponografia ya watoto.

Mwanamke mmoja aliyetoa ushahidi kuwa Kelly alimfunga, kumpatia dawa za kulevya na kumbaka alisema katika taarifa iliyoandikwa baada ya uamuzi huo kwamba amekuwa "akijificha" "kutokana na vitisho vilivyotolewa dhidi yangu" tangu alipomtuhumu hadharani.

"Niko tayari kuanza maisha huru bila uwoga na kuanza mchakato wa uponyaji," mwanamke aliyetambuliwa mahakamani kama, Sonja, aliongeza.

Nyaraka za kisheria pia zilifichua mateso ya kiakili ambayo Kelly aliwafanyia wahasiriwa wake. Hawakuruhusiwa kula au kwenda msalani bila idhini yake, aliamua nguo walizovaaa na kuwafanya wamuite "Daddy".

Gloria Allred, wakili aliyewawakilisha wahasiriwa kadhaa, aliwaambia waandishi: "Nimehudumu kwa miaka 47. Wakati huu, nimefuatilia wanyanyasaji wengi wa kingono ambao wamefanya uhalifu dhidi ya wanawake na watoto

"Kati ya wanyanyasaji wote niliowafuatilia , Bw. Kelly ni mbaya zaidi."

Tazama: R. Kelly 'ni mnyanyasaji hatari zadi wa kingono.'

Katika mkutano na wanahabari nje ya mahakama siku ya Jumatatu, mwendesha mashtaka Jacquelyn Kasulis alisema kuwa jaji alituma ujumbe mkali kwa wanaume wengine wenye uwezo kama Kelly.

"Haijalishi itachukua muda gani, mkono mrefu wa sheria utakunasa,"alisema Bi. Kasulis.

Uamuzi huo unakuja miaka 13 baada ya Kelly kufutiwa mashtaka ya ponografia ya watoto baada ya kushtakiwa katika jimbo la Illinois.

Madai mengi yaliyosikilizwa katika kesi hiyo yalitolewa kwanza katika simulizi ya mwaka 2019 ya Surviving R Kelly.

Wahasiriwa wakati mwingine waliteuliwa miongoni wa watu waliohudhuria tamasha lake, au walishawishika kuungana naye baada ya kupewa msaada na kazi zao mpya za muziki baada ya kupata bahati ya kukutana na mwimbaji huyo.

Lakini baada ya kujiunga na wasaidizi wake, waligundua kwamba walikuwa chini ya sheria kali na waliadhibiwa vikali ikiwa walikiuka kile timu yake iliita "Sheria za Rob".

Huu ulikuwa uamuzi wa haraka wa majaji wa wanaume saba na wanawake watano.

Walichukua saa tisa kwa zaidi ya siku mbili kufikia uamuzi,ikimaanisha lazima walikuwa wameungana sawa katika uchunguzi wao wa ushahidi.

Mara kabla ya uamuzi kutolewa, mashabiki wachache wa R. Kelly walivuja rekodi ya muziki wake nje ya mahakama. Nawauliza wanajihisi vipi baada ya kumpatikana na hatia. Wanaonekana kuwa na huzuni na bado wanamuunga mkono.

Kwa upande mwingine wahasieiwa wa R. Kelly wamepata faraja japo kidogo.

Mmoja wao ambaye - hakutambulishwa kipindi chote cha kesi hiyo - alitoa taarifa kusema sasa anahisi anaweza kuanza mchakato wa uponaji. Uamuzi huu bila shaka ulitegemea ushuhuda wao na nia ya kusimulia kiwewe cha kibinafsi.

Kwa miongo kadhaa wanawake hawa weusi waliendelea kuuliza lini watasikilizwa, sauti zao zitakuwa muhimu lini. Uamuzi huu ni ushindi wa kampeni ya Me Too.

Wakati wa kusikizwa kwa kesi hiyo mahakama pia ilifahamishwa jinsi alivyopata nyaraka kinyume cha sheria kuoana na mwimbaji mchanga Aaliyah, ambaye alifariki katika ajali ya ndege mnamo Agosti 2001 baada ya kuolewa na Kelly akiwa na umri wa miaka 15.

Wakili wa Kelly, Deveraux Cannick amewaambia wanahabari kwamba mwimbaji huyo hakutarajia atapatikana na hatia.

Kelly pia anakabiliwa na mashtaka mengine katika mahakama ya Chicago kuhusiana na ponografia ya watoto na kuvuruga ushahidi wa mashtaka dhidi yake. Mwimbaji huyo pia kukabiliwa na mashtaka ya unyanyasaji wa kijinsia huko Illinois na Minnesota.

Washirika wake wawili wa zamani wamekiri makosa katika kesi nyingine inayohusiana na jaribio la kuwanyamazisha wanaomtuhumu Kelly.

BBC Swahili
 
US singer R Kelly has been found guilty of exploiting his superstar status to run a scheme to sexually abuse women and children over two decades.

Eleven accusers, nine women and two men, took the stand over the searing six-week trial to describe sexual humiliation and violence at his hands.

After two days of deliberation, the jury found Kelly guilty on all the charges he was facing.

Sentencing is due on 4 May and he could spend the rest of his life behind bars.

The jury found Kelly, whose full name is Robert Sylvester Kelly, was the ringleader of a violent and coercive scheme that lured women and children for him to sexually abuse.

The singer - most famous for the award-winning song I Believe I Can Fly - was also found to have trafficked women between different US states.

Along with eight counts of sex trafficking, Kelly was found guilty of racketeering - a charge normally used against organised crime associations.

During the trial prosecutors detailed how his managers, security guards and other entourage members worked to assist him in his criminal enterprise.

One woman who testified that Kelly imprisoned, drugged and raped her said in a written statement after the verdict that she had "been hiding" from Kelly due to threats made against her since she went public with her accusations.

"I'm ready to start living my life free from fear and to start the healing process," added the woman, identified in court as Sonja.

Another woman who testified in court, Lizette Martinez, said she was "relieved" by the verdict.

"I'm so proud of the women who were able to speak their truths," she added.

Legal documents have revealed the mental torment that Kelly subjected his victims to. They were not allowed to eat or use the bathroom without his permission, he controlled what clothes they wore and made them call him "Daddy".

Gloria Allred, a lawyer who represented several victims, told reporters: "I've been practicing law for 47 years. During this time, I've pursued many sexual predators who have committed crimes against women and children.

"Of all the predators that I have pursued, Mr Kelly is the worst."

At a news conference outside the court on Monday, prosecutor Jacquelyn Kasulis said that the jury had sent a message to other powerful men like Kelly.

"No matter how long it takes, the long arm of the law will catch up with you," said Ms Kasulis.

The verdict comes 13 years after Kelly was acquitted of child pornography charges after a trial in the state of Illinois.

Many of the allegations heard in the trial were first laid out in the 2019 documentary Surviving R Kelly.

Victims were sometimes selected from his concert audiences, or were enticed to join him after being offered help with their fledgling music careers after chance encounters with the singer.

But after joining his entourage, they found that they were subjected to strict rules and aggressively punished if they violated what his team had dubbed "Rob's rules".

This was a swift decision by the jury of seven men and five women.

They took nine hours over two days to reach a verdict, meaning they must have been fairly united in their examination of the evidence.

Right before the verdict was read, a handful of R. Kelly's fans blasted his music outside the courthouse. I asked them how they felt after he was found guilty. They were visibly sad and told me they still supported him.

On the other hand, R. Kelly's victims are feeling some measure of comfort.

One - who remained anonymous throughout the trial - issued a statement saying she felt like she could now start the healing process. This verdict no doubt hinged on their testimony and willingness to recount personal trauma.

For decades these black women kept asking when they would be heard, when their voices would matter. This conviction is their Me Too victory.

During the federal trial, the court also heard how he had illegally obtained paperwork to marry underage singer Aaliyah, who died in a plane accident in August 2001 after marrying Kelly at age 15.

Kelly's lawyer Deveraux Cannick told reporters that the singer did not expect to be found guilty.

"The government cherry-picked their version that they thought would support the continuation of the narrative," said Mr Cannick. "Why would he expect this verdict given all the inconsistencies that we saw?"

Kelly is separately facing trial in Chicago on child pornography and obstruction charges. He is also due to face sex abuse charges in Illinois and Minnesota.

At least two former Kelly associates have pleaded guilty in separate cases related to attempts to silence Kelly's accusers.
 
Mara nyingi watu wenye vipaji vya hali ya juu kwenye fani tofauti wakati mwingine huonyesha tabia zisizo za kawaida kwa jamii

Tabia hizo extraordinary zikiwa chanya inakua ni vizuri, lakini ikiwa kinyume chake inakua balaa.

Kwa haiba yake, kwa pesa zake, kwa umaarufu wake, kwa kipaji chake jamaa angeweza kumpata aina ya mwanamke yeyote anaemtaka sio tu US bali pote ulimwenguni. Hakua na sababu ya ku abuse minors wala kufanya unyanyasaji wa wanawake

Aidha kuna conspiracy theorists wanadai kwamba eti kilichomponza R. Kelly ni kukataa na kubeza kwake tuzo za Grammy na Oscar

Kwamba alikataa kuingizwa kwenye mchuano wa tuzo husika akisema hakuna mwanamuziki wa kuchuana nae, na kumshindanisha yeye na wanamuziki wengine ni kumshushia hadhi yake!

Kwamba waandaji (or waanzilishi rather) wa hizi tuzo ni miongoni mwa watu very powerful duniani na wao ndio humpandisha msanii na kuweza kumshusha wakati wowote wakihisi ameota mapembe

BUT I DON'T BUY THESE CONSPIRACIES
 
Wazungu ni watu wabaya sana,,,wanakupenda pale tu wakiwa na maslahi na wewe,,
Ukienda kinyume na wao basi,,,,wanakumaliza .
Hili la R.Kelly si jipya au si yeye wa kwanza kufanyiwa hujuma za aina hii,,,
Wapo MICHAEL JACKSON,,,,BOB MARLEY na wengineyo wameshushwa na wengine kuuawa kwa kwenda nao kinyume,,,
Kinachomponza R.Kelly kwa sasa ni misimamo yake kwao,,,
 
huyu kajitenga na Freemason lazima wamnyooshe kama ilivo ada kwako ujijifanya mjuaji lazima wakufuanyie chochote wanachojisikia ...

Michael Jackson, Bob , 2 Pac,Kanumba na wengine wengi yaliwakuta kwetu sio mageni ...
 
huyu kajitenga na Freemason lazima wamnyooshe kama ilivo ada kwako ujijifanya mjuaji lazima wakufuanyie chochote wanachojisikia ...

Michael Jackson, Bob , 2 Pac,Kanumba na wengine wengi yaliwakuta kwetu sio mageni ...
Nadhani ungemtoa Kanumba kwenye hiyo list
 
Wazungu ni watu wabaya sana,,,wanakupenda pale tu wakiwa na maslahi na wewe,,
Ukienda kinyume na wao basi,,,,wanakumaliza .
Hili la R.Kelly si jipya au si yeye wa kwanza kufanyiwa hujuma za aina hii,,,
Wapo MICHAEL JACKSON,,,,BOB MARLEY na wengineyo wameshushwa na wengine kuuawa kwa kwenda nao kinyume,,,
Kinachomponza R.Kelly kwa sasa ni misimamo yake kwao,,,
Kuna yule Mzee Cosby, nae pia yakimkuta, Ila naskia anaachiwa, ameshinda rufaa
 
Back
Top Bottom