Marekani ina maslahi gani kwa jumuiya ya uamusho Zanzibar? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marekani ina maslahi gani kwa jumuiya ya uamusho Zanzibar?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ileje, Jun 1, 2012.

 1. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Marekani inasemekana kwa kiasi kikubwa kuifadhili jumuiya ya uamusho ya Zanzibar kwa kuipatia fedha na samani za ofisi. Hii ilijidhihirisha wazi kwa ubalozi wa nchi hiyo ikiwa ni pamoja na balozi za Uingereza na Norway kushiriki katika mazungumzo yaliyofanyika hivi karibuni baina n=ya waziri wa mambo ya ndani Dr. Nchimbi, IGP Mwema na viongozi wa kiislamu Zanzibar.

  Je nchi hizi tatu zina maslahi gani na jumuiya ya uamusho?
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,218
  Trophy Points: 280
  Hazina maslahi yoyote na Jumuiya ya Uamsho bali nchi zote hizo zina maslahi na amani na utulivu wa nchi yetu kwa maslahi yao!.

  US ndiye kiranja mkuu, Ghailani alitokea Zanzibar hivyo jambo lolote litakalo hatarisha amani ya Zanzibar, Marekani lazima aingize pua, isije kuwa ni masalia ya Alqaeda!.

  Uingereza yeye ndio former colonial master wetu hivyo Tanzania na Zanzibar ni watoto wake wa kufikia lazima ijiridhishe amani inapatikana huku ili iendelee kuyafanya inayofanya Tanzania kwa amani na utulivu. Norway ina interest na amani ya kweli!.
   
 3. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Nimepita!
   
 4. leroy

  leroy JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 834
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 60
  Kumradhi, naomba unithibitishie hapo pekundu.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Pasco, ni vigumu kuwa categorical kuwa Marekani wanataka hali gani Tanzania. Marekani wakijua una kitu wanachokita haijalishi una amani na utulivu au una vita. Na maadam tumeshawaachia mpaka kwenye uvunguni basi tukae tunyolewe. Kitendo cha waziri wa nchi kuambatana na mabolozi wa nje kuongea na viongozi wa dini huko Zanzibar was rather telling. Sijui tumefikaje hapa lakini kwa hakika ule "umaskini jeuri wetu' umepotea kabisa.
   
 6. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  LIKE LIKE, tena ndani ya 12 hours, maana vurugu zilikuwa usiku na kikao kikawa kesho yake!
   
 7. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Habari za kuaminika kutoka ndani ya uamusho ni kuwa baadhi ya computers zinazotimika katika ofisi yao zimetolewa na ubalozi wa Marekani.

  Aidha leo asubuhi katika Star TV mwandishi maarufu wa makala Bw. Jabir amethibitisha hilo!
   
 8. leroy

  leroy JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 834
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 60
  Ahsante.
   
 9. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Watu wengine wanasema labda sembe tunayokula ndiyo inayoathiri akili zetu na namna yatu ya kufikiri. Kwa yale yaliyotokea Zanzibar mimi nawalaumu wahusika wenyewe - waliokuwa wakihurubiri na kuhamasisha watu ili wafanye kama walivyofanya. Maana tukianza kuwaingiza Wamarekani, Waingereza na Wanorwei baadaye tutaweza pia kuhamisha kuwabariki wale wanaotafuna nchi yetu usiku na mchana kwa ufisadi na kuhamishia maovu hayo kwa "wazungu". Kisha tutaanza kusema "Watanzania ni watakatifu" ila wazungu ndio wanaotuibia, ndio wanaoua albino, ndio wanaolamba fedha za serikali na halmashauri zetu, ndio wanaowapa mimba watoto wetu wa shule na ndio pia waliochoma makanisa na magari nk. "Unless we call the problem by its real name, we will not be able to identify and solve it."
   
 10. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ... mpaka uje uone KIPIGO CHA MMBWA MWIZI kwa kikundi cha kigaidi cha Wana-Uamsho mkuu?? Lazima ipate kuwafahamu na malengo yao hao kwanza ndi mambo mengine kuendelea. We kaa tu hapo
   
 11. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Zina more to loose with terrorism than kupata maslahi. ktk biashara unaweza ongeza faida kwa kuzuia hasara bila kuongeza mauzo.
   
 12. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Nani kakuambia Serikali ya Marekani ina Maslahi na Jumuia ya Uamsho? Nakwambia hata kidogo na Serikali ya Marekani

  Ikijua kuwa Makanisa yalipigwa Mabomu hiyo Jumuia na Watu wake watakwekwa kwenye kundi la Magaidi, na Marekani

  Itawaweka kwenye Black Book itafuatilia wapi hao wanapata wapi pesa; Sijui mnapata wapi hiyo habari kuwa Marekani

  Inapata Maslaki kutokana na kujihusisha na Uamsho; hata kidogo; Juzi nilikuwa State Department na hawaijui....
   
 13. BINARY NO

  BINARY NO JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,776
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  SERIKALI lazima iwafukuze hawa mabalozi kwani kwa kitendo cha waziri kuongozana nao hiyo ni dalili tosha kua hawa jamaa wanaendeleza sera zao za divide n rule...Mfano ni MISRI ilikuja kujulikana kua balozi ya US na wafanyakazi wake walikua wanasupport kwa kutoa fedha kwa NGOs zao ili zifanikishe adhima ikiwemo ku spy....Tukumbuke vita iliyokuepo kati ya URUSI n US those days..US kwa sasa anapenda sana kuweka military base ZENJ na km sio bara kuweka oingamizi sijui sasa wanataka kutuvunja ili watutawale zaidi na uku wao ndo kwanza wanaungana....kwanini ishu ya ndani ya nchi hawa mabalozi wanahusika na bado serikali haijachukua hatua
   
 14. F

  FJM JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tanzania tuna matatizo mengi sana, hilo nakubaliana na wewe kabisa. Lakini siamini kama Marekani wana dawa ya matatizo yetu maana hawana. Na sidhani ile haraka ya balozi wao kuambatana na Nchimbi kwenda Zanzibar ni kwa sababu wanawapenda sana Zanzibari na watanzania kwa ujumla.

  Kumbuka huko nyuma Tanzania ilikuwa bottom of the list ya 'wapenzi' wa Marekani kwa East Afria. Sasa nini kimebadilika ghafla mpaka tukwa number one? Wamegundua sisi ni binamu zao tuliopoteana wakati wa biashara ya utumwa au?
   
 15. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #15
  Jun 1, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  marekani na hizo nchi nyingine lazima ziingilie-maana wanajua wakikaa kimya hapo zenji itakuwa ni heaven nyingine ya alqaeeda na mujaheedin wengine-so lazima achukue tahadharu mapema sana-maana asipopfanya hivyo hao uamsho wote watapafanya hapo kama afghanstani-maana hawana tofauti na taliban
   
 16. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #16
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  Mkuu Pasco,
  Uko sahihi kwa asilimia kubwa, Hata Norway wana interest na amani ya Tz kwa maslahi yao!
   
 17. r

  ralphjn Senior Member

  #17
  Jun 1, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hujui tumefikaje hapa?Chama tawala kimetufikisha hapa hapa tulipo.
   
 18. HUGO CHAVES

  HUGO CHAVES JF-Expert Member

  #18
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 1,852
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  iko kitu imejificha nyuma ya pazia naomba ufafanuzi hiki kikundi SMZ inakitambua uwepo wake .je ikawaje wapewe computer na wakatulia kuna mkataba gani wa siri na hiki kikundi na je ni nani wapo kwenye hiki kikundi ,wako wangapi,wana lengo gani na tanzania tuitakayo ,.tumeona vikundi kama hivi vikiibuka kama boko haram na jinsi vinavyosumbua ,wahusika wakiangalie hiki kikundi na shughuli zake zieleweke kama wapo kwenye category ya NGO WAJISAJILI .kama ni chama cha siasa kifuate taratibu zake kwa msajili wa vyama .pia uamsho wanamuamsha nani ,na kwanini iwe ni wakati huu .huko nyuma walikuwa wapi wamelala .hakuna kuwaza sana angalia boko haram walianzaje wana tofauti gani na hawa uamsho ambao sijui wanamuasha nani na nani kawatuma kwa madhumuni yapi .
   
 19. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #19
  Jun 1, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sijapata wahi kuona Taifa linalochukulia mambo kwa tahadhari kama Marekani.Wameona ya afghanstan na somalia yasije yakatokea tena Zanzibar watahakikisha muungano huutaka kamwe ukavunjika kwa hali na mali.Na usikute walishawasoma kitambo mpaka wakawapa computer ili wawafuatilie kile wanachokifanya.
   
 20. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #20
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,288
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  Ni hofu tu wanayopata kwa kuona ule mzuzu wa yule kiongozi wa wa huo uamusho.
   
Loading...