Hakuna Mtu Anayeweza Kuiangusha Marekani Kwenye Medani ya Kivita na Kiutawala katika hii Dunia ya sasa

Annunaki

JF-Expert Member
Dec 30, 2021
1,911
3,171
Marekani ndiye Super Power halisi katika dunia hii, Marekani amekomesha Utumwa, Marekani anapambana na Ugaidi duniani, Marekani anatetea Demokrasia na Uhuru wa maoni kwa kila mtu, Marekani anapinga vikali sera za utawala wa kimabavu na udikteita duniani ambazo zinafuata sera za kijamaa, Marekani anasaidia nchi masikini na zinazoendelea ili zijikwamue kiuchumi, Marekani ni taifa lenye uchumi imara, Jeshi imara na teknolojia ya hali ya juu kwenye masuala mbalimbali.

Kutokana na udhaifu na udogo wa nchi ya Ukraine kama Marekani angekuwa anapigana vita hii angekuwa ashamaliza vita zamani toafuti na Russia anayetapa tapa mpaka sasa.

Marekani imewaangusha viongozi wakatili, magaidi, baadhi yao ni kama Sadam Hussein, Gadaffi, Osama, Mobutu, Mgabe.

Marekani amepigana vita ngumu zaidi duniani na kuzishinda kwa uwezo wa hali ya juu sana, baadhi ya vita ngumu alizopigana ni hizi hapa

American Revolution War (1775-1783)
Hii ilikuwa ni vita Kati ya America na Britain, vita hii ilikuwa ni kwa ajili ya Uhuru wa America na ndiyo iliyopelekea kuzaliwa kwa USA , katika vita hii Britain alipokea kichapo kikali sana na kukimbia, hivyo America ikajitangazia uhuru wake.

Vita ya 1812 (1812-1815)
Vile vile vita hii inajulikana kama vita ya pili ya Uhuru wa America. Vita hii ilisababishwa na Britain kutaka kuingilia biashara Kati ya US na Ufaransa, hali hii iliwalazimu Us kumchapa tena Britain.

Mexican-American War (1846-1848)
Mwaka 1845 jimbo la Texas lililo kuwa sehemu ya Mexico lilitangaza kuwa Jamuhuri ya Texas na kujiunga na US hali hiyo ilipelekea majeshi ya Mexico kuvamia jimbo hilo hili kulirejesha, US akaingilia Kati na kuyafurusha majeshi ya Mexico na mpaka sasa limebaki kuwa jimbo la Marekani.

Civil War (1861-1865)
Hii ilikuwa vita ya wenyewe kwa wenyewe Kati ya state ya kusini na state ya kasikazini, vita hii ilisababishwa na mamlaka ya kusini ya US iliyokuwa ikipinga wazo la Rais Abraham Lincoln la kuanzisha Serikali ya shirikisho na kukomesha biashara ya Utumwa.

Spanish-American War(1898)

mnamo karne ya 19, Cuba ilikuwa sehemu ya spanish (hispania ya leo), kutokana na takwa lake la kutaka kujitenga na kuwa huru, miaka ya 1895-1898 uliibuku mgogoro Kati ya Cuba na Spanish, mgogoro huo ulipelekea US kuingilia Kati kwa kuisapoti Cuba kwa sababu alikuwa mshirika wake wa kibiashara. Spanish akapigwa na Cuba akatumiza lengo lake.

Vita ya Kwanza ya Dunia (1917-1918)
US hakuwa na nia kabisa ya kushiriki vita hii,ila ni kama alilazimishwa na Germany na hii ni Baada ya Ujerumani kutuma manuali za kivita katika mediterranean na North atlantic, kutaka kushirikiana na mexico kuivamia US, hali hii ilimlazimisha Rais Woodrow Wilson kutangaza vita dhidi ya Ujerumani na kilichotokea baada ya hapo kinajulikana, Ujerumani alipigwa vibaya hovyo.

Vita ya Pili ya Dunia (1941-1945)

Vita hii ya pili ya dunia ilianza baada Germany kuivamia kijeshi Poland September 1,1939. US alihusika na vita hii baada ya vikosi vya kijeshi vya Japan kushambulia Pearl Harbor mnamo December 8,1941, Japan ambayo ilikuwa na Germany & Italy kama washirika wake huku US akiwa na Britain & Soviet Union kama washirika wake, USA aliimaliza vita hii kwa Kupiga bomu la Nyukilia Hiroshima na Ngasaki, bomu lililo itetemesha Dunia hadi leo hii, Bomu lililo leta mapinduzi makubwa katika silaha za Nyukilia, Bomu ambalo ndilo Putin na madikteita wengine uchwara wanatamba nalo leo hii. US kama alitumia Bomu hili miaka hiyo sijuhi kwa sasa ana Bomu la siri la aina gani

Korean War (1950-1953)
Vita hii US alipigana kwa kuisapoti Korea kusini. Vita ilitokea baada ya Korea kaskazini kwa kushirikiana na China na USSR kama washirika wake kutaka kuivamia Korea kusini ili kuitawala na kuuda Serikali moja yenye utawala wa kijamaa. US aliingilia Kati na kuwafurusha wote.

Vietnam War (1959-1975)
Hii ilikuwa ni vita ngumu sana kwa USA, vita hii iliwalazimu USA kutumia mbinu kali za Mapigano ili kuangusha utawala wa kijamaa wa vietnam. Vita hii ilikuwa ni Kati ya vietnam vs USA & nchi nyingine ambazo hazikuwa chini ya utawala wa kijamaa.

Gulf War (1990-1991)
Vitaa hii ilitokea baada ya Iraq chini ya Sadam Hussein kuivamia Kuwait na kuikalia kimabavu kama afanyavyo leo Putin huko Ukraine. Pamoja na Vikwazo vya kiuchumi alivyowekewa Iraq na UN na vikosi vya nchi 34 wanachama wa UN kupelekwa Iraq haikuzaa matunda mpaka pale USA alipoingilia kati na Iraq ikatandikwa vibaya hovyo.

Vita ya Afghanistan (2001-2021)

Mpaka sasa hii ndo vita ambayo USA amepigana kwa muda mrefu sana. Vita hii ilianza baada ya shambulizi la kigaidi la 9/11 dhidi ya kituo cha kibiashara cha Dunia NewYork & Pentagon Washington DC mwaka 2001 lililo tekelezwa na Al-Qaeda. Shambulizi hilo la kigaidi lilisababisha US kuingia Afghanistan kupigana vita kwa lengo la kuwatoa Al-Qaeda na Taliban madarakani ili kufuta Ugaidi duniani. Mwaka 2011 kiongozi wa Al-Qaeda Osama Bin Laden aliuawa na kikosi maalumu cha USA. Baada ya USA kutekeleza lengo lao mwaka 2021 alihamua kuondoa majeshi yake na Ndege ya mwisho iliondoka Afghanistan August 30, 2021.

Iraq War (2003-2011)

Baada ya shambulizi la kigaidi la 9/11, 2001, mwaka 2003 aliyekuwa Rais wa USA G.W. Bush alitangaza vita dhidi ya Iraq. Iraq iliyokuwa ikiongozwa na Sadam Hussein ikisaidiwa na Korea Kaskazini kutengeneza Silaha za maangamizi (Nyukilia) na kufadhili makundi ya kigaidi, USA ilimkamata Sadam Hussein na kumnyonga huku Dunia nzima ikishuhudiwa na kushangilia kuuawa kwa dikteita Sadam Hussein aliyekuwa akifadhili magaidi duniani.

USA amekuwa kinara wa kuziangusha Serikali na tawala za kimabavu duniani, ili kuleta usawa kwa watu wote, baadhi ya tawala za kikatili Zilizokuwa zimeshindikana na zika angishwa na USA ni hizi zifuatazo:

Germany, 1945
Japan, 1945
Syria, 1949
South Korea, 1953
Iran, 1953
Guatemala, 1954
Congo, 1960
Laos, 1960
Iraq, 1963
Brazil, 1964
British Guiana, 1964
Bolivia, 1964
Dominican Republic, 1965
Indonesia, 1965
Ghana, 1966
Greece, 1967
Cambodia, 1970
Bolivia, 1971
Chile, 1973
Australia, 1975
Portugal, 1976
Argentina, 1976
Jamaica, 1980
Turkey, 1980
Chad, 1982
Fiji, 1987
Nicaragua, 1987
Afghanistan, 1989
Panama, 1989
Bulgaria, 1990
Albania, 1991
Yugoslavia, 2000
Ecuador, 2000
Afghanistan, 2001
Venezuela, 2002
Iraq, 2003
Haiti, 2004
Libya, 2011

"Thrifty Authoritarians: U.S. Regime Change 1945-Present - JournalQuest" Thrifty Authoritarians: U.S. Regime Change 1945-Present - JournalQuest

Hakuna taifa la kuingusha Marekani katika dunia hii, Marekani itajiangusha yenyewe.

5357522048_35c1db3008_z.jpg
CIA.jpg
 
Russia & China Bado sana kuwa super power wa Dunia, hizi Nchi zote Mifumo na sera zao zimekaa kidikteita, haziwezi kukubalika sana duniani, kiufupi hizo nchi zinatapa tapa tu, madikteita pekee ndiyo wanakubali sera zao.
 
Huko lengo la vita lilikamilika, haikuwa na haja ya kuendelea kupakalia, kwa sababu Marekani inatetea Demokrasia duniani.
Pamoja na democrasia unayosema anatetea duniani,lkn pale kwao, Yule mwanamke aliposhinda uchaguzi wakaona hapana Bora tumpe kiti huyu mtu mweusi,na hapo juzi aliposhinda tena kamati ya jaji Lubuva wa US ikaona haiwezekani Bora tumpe huyu Mzee kichaa Trump
 
Aliyepiga marufuku viroba alikuwa yupo sahihi kabisa,ila aliyeruhusu DOUBLE KICK na RIVELLA kiukweli katuletea matatizo duniani.hii ni moja ya positive effect ya DOUBLE KICK na RIVELLA
Bwana mohamedidrisa789 umekwazika na nini kwenye hii makala
 
Pamoja na democrasia unayosema anatetea duniani,lkn pale kwao, Yule mwanamke aliposhinda uchaguzi wakaona hapana Bora tumpe kiti huyu mtu mweusi,na hapo juzi aliposhinda tena kamati ya jaji Lubuva wa US ikaona haiwezekani Bora tumpe huyu Mzee kichaa Trump
Hakuna namna yeyote ile unayoweza kutumia kuthibitisha madai Yako. Demokrasia ipo juu sana Marekani, anayeshinda, anashinda kihalali
 
Back
Top Bottom