Marekani yafanya mashambulizi ya angani dhidi ya washirika wa Iran huko Iraq na Syria, kunani?

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
18,687
29,416
Marekani imeanzisha mashambulio ya angani dhidi ya wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran huko Iraq na Syria, Pentagon imetangaza.

Mashambulizi hayo yalilenga "Eneo la kuhifadhi silaha", kwa kujibu mashambulio ya wanamgambo dhidi ya vikosi vya Marekani, ilisema taarifa.

"Rais Biden amekuwa wazi kuwa atachukua hatua kuwalinda wafanyikazi wa Marekani," Pentagon ilisema.

Hii ni duru ya pili ya mashambulio ya angani Joe Biden ameidhinisha dhidi ya wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran tangu aingie madarakani.

Vikosi vya Marekani vilivyoko Iraq vimeshambuliwa mara kadhaa katika miezi ya hivi karibuni kupitia mashambulizi ya ndege zisizo na marubani. Iran imena kuhusika.

Karibu wanajeshi 2,500 wa Marekani nbdo wapo nchini humo kama sehemu ya muungano wa kimataifa unaopambana na kundi la Islamic State (IS).

Kulingana na taarifa ya Pentagon, "shambulizi hilo sahihi' lililenga maeneo mawili huko Syria na moja huko Iraq. Imesema kundi la wanamgambo linaloungwa mkono na Iran ikiwa ni pamoja na Kataib Hezbollah na Kataib Sayyid al-Shuhada walitumia vifaa hivi.

Tangu 2009, Marekani iliitangaza Kataib Hezbollah kama shirika la kigaidi, ikilishtumu kwa kutishia amani na utulivu wa Iraq.

Marekani ilichukua hatua hiyo ili kujilinda, taarifa hiyo ilisema, ikichukua "hatua muhimu, zinazofaa, na za makusudi ili kupunguza hatari kuongezeka - lakini pia kutuma ujumbe wa wazi na dhahiri wa kuzuia mashambulizi kutoka kwa makundi hayo".

Pentagon haikusema ikiwa mtu yeyote aliuawa au kujeruhiwa katika mashambulio hayo. Lakini kwa mujibu wa shirika la habari la AFP Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Syria, kikundi cha ufuatiliaji chenye makao yake Uingereza, kilisema kwamba wapiganaji watano wa wanamgambo waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa nchini Syria "katika shambulio la ndege za kivita za Marekani".

Shirika la habari la serikali ya Syria Sana wakati huo huo liliripoti kuwa mtoto alifariki na watu wasiopungua watatu wamejeruhiwa, AFP ilisema.

Ushawishi wa Iran juu ya mambo ya ndani ya Iraq umekua kwa kasi tangu uvamizi ulioongozwa na Marekani uliomuondoa madarakani Saddam Hussein mnamo 2003.

Shambulizi hilo limekuja wakati Iran imekuwa ikifanya mazungumzo na madola ya ulimwengu ikiwa ni pamoja na Marekani juu ya kufufua makubaliano ya nyuklia ya 2015, ambayo yaliondoa vikwazo dhidi ya serikali ili Iran isitishe shughuli zake za Kinyuklia

Nchi zingine - pamoja na Israeli - zinaamini Iran inajaribu kujenga bomu la nyuklia, jambo ambalo Iran imekanusha

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump aliamua kuiondoa nchi yake kutoka makubaliano hayo mnamo 2018 na kuiwekea tena Iran vikwazo.

Utawala mpya Tehran

Mashambulizi hayo ya Marekani dhidi ya makundi yanayodaiwa kuwa karibu na Iran yamekuja wakati ambapo Tehran ipo chini ya rais mpya Ebrahim Rais aliyeshinda uchaguzi wiki mbili zilizopita .Marekani na Israel tayari zimemtaja kama tishio kwa usalama wao na Ebrahim mwenyewe ameonyesha kuendelea na msimamo mkali wa taifa lake dhidi ya matakwa ya mataifa ya magharibi kuhusu mpango wa taifa lake wa nyuklia .

Wahafidhina wana mashaka na nchi za Magharibi, lakini Bw Raisi na Kiongozi Mkuu Khamenei wanafikiriwa kupendelea kurudi kwa makubaliano ya kimataifa kuhusu shughuli za nyuklia za Iran.

Mpango wa Pamoja wa Utekelezaji, uliosainiwa mnamo 2015, uliipa Iran unafuu kutoka kwa vikwazo vya Magharibi kwa sababu ya kupunguza shughuli zake za nyuklia.


Marekani iliondoa mpango huo mnamo 2018, na utawala wa Rais Trump uliweka tena vikwazo vya kulemaza uwezo wa Iran wa kufanya biashara.

Mpango wa Pamoja wa Utekelezaji, uliosainiwa mwaka 2015, uliipa Iran unafuu kutoka kwa shughuli za Magharibi kwa sababu ya shughuli za shughuli zake za nyuklia.

Baada ya kuchaguliwa kwa Raisi waziri mkuu wa Israel alisema kwamba jamii ya kimataifa inafaa kuamka kufuatia ushindi wake.

Naftali Bennet alisema kwamba utawala wa Iran umekuwa ukitaka silaha za kinyuklia - kitu ambacho Iran inakana.

Iran na Israel zimekuwa zikipigana vita baridi , hali iliyosababisha mataifa yote mawili kukabiliana lakini yote yakizuia kutokea kwa vita vitakavyoshirikisha mataifa mengine.

Hivi majuzi , hatahivyo , uadui kati ya mataifa hayo mawili umeongezeka tena. Hali ni ngumu , lakini chanzo kikuu cha wasiwasi uliopo ni vitendo vya kinyuklia vya Iran.

Iran inalaumu Israel kwa mauaji ya mwanasayansi wake mkuu mwaka uliopita na shambulio katika kinu chake cha madini ya Uranium mwezi Aprili.

Israel haiamini kwamba mpango wa kinyuklia wa Iran ni wa amani na ina ushahidi ina mipango ya kutengeneza silaha za kinyuklia.
 

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,056
19,615
Narudi kueleza maana ya hii
map_26Jan2021.width-480.png
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

2 Reactions
Reply
Top Bottom