Marekani: Auawa kwa kuumwa na nyoka anaowafuga nyumbani kwake kwa siri, Polisi wakuta nyoka 124

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Mwanaume mmoja katika maeneo ya Maryland huko Marekani amekutwa amekufa baada ya kung’atwa na nyoka aliokuwa akiwafuga.

Polisi wamesema kuwa wamekuta mwili wa mwamba huyo ukiwa chini huku kukiwa na nyoka zaidi ya 100 wenye sumu na wasio na sumu katika nyumba yake ambapo mwili ulipopimwa ulikutwa na sumu nyingi mwilini

Imeelezwa kuwa, mtu huyo David Riston, 49, aliumwa na nyoka mwenye sumu kali.

Polisi walipata taarifa kutoka kwa majirani ambao hawakumuona jamaa huyo kwa zaidi ya saa 24, ndipo ikabidi waende kwake kuchunguza na kumkuta ameshapoteza maisha

Mmoja wa nyoka aliokutwa akifugwa ni Burmese python mwenye urefu wa futi 14 na wengine ambao ni kinyume cha sheria kufugwa kwa mujibu wa sheria za Maryland, wakiwemo cobras, black mambas na rattlesnakes.

Baadaye maofisa wa usalama na Wanyama walipofanya hesabu walikuta kuna nyoka 124 nyumbani hapo na hakukuwa na Jirani ambaye alikuwa akijua kilichokuwa kinafugwa na jamaa huyo kwenye nyumba yake.

Source: People
 
Huyo sasa si Angemezwa kabisa na huyo Nyoka ili baadae ageuke Mavi
 
Huna chanzo, people maana yake nini unaleta gumzo la mtaani hapa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom