The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,355
- 17,321
Mzee Joe Ligon alikamatwa mwaka 1953 na kufungwa kifungo cha maisha bila uwezekano wa kupata msamaha.
Bwana Joe alikamatwa huko Pennsylvania kwa kukosa la mauaji ambalo mwenzake alifanya mauaji na kwa sheria za jimbo hilo, mtu akifanya mauaji hata wale walioshirikiana nao wanahukumiwa sawa na mtenda kosa.
Mzee Ligon amekaa jela miongo 7, mwaka huu ameachiwa kwa kushinda kesi na ameachiwa huru na serikali ya jimbo imesema itamfidia dollar Milioni 3 kama kifuta machozi.
Mzee anasema jamaa zake na karibu ndugu zake wote walishakufa. Anasema amekuta Dunia imebadilika sana, anaona vitu vya ajabu lakini anakubali kuwa alitegemea kukuta Dunia iko tofauti na alivyoiacha.
Kukaa jela miaka 70 sio mchezo.
Marekani kuna vituko, kuna yule askari polisi ana miaka 94 na anasema hana mpango wa kustaafu na gari la patrol anaendesha mwenyewe, karibu wakazi wote wa mtaa wake hadi vitukuu anavijua.