Marekani: Atoka jela baada ya kufungwa karibia miaka 70, atoka jela akiwa na miaka 83

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Jela.jpg

Mzee Joe Ligon alikamatwa mwaka 1953 na kufungwa kifungo cha maisha bila uwezekano wa kupata msamaha.

Bwana Joe alikamatwa huko Pennsylvania kwa kukosa la mauaji ambalo mwenzake alifanya mauaji na kwa sheria za jimbo hilo, mtu akifanya mauaji hata wale walioshirikiana nao wanahukumiwa sawa na mtenda kosa.

Mzee Ligon amekaa jela miongo 7, mwaka huu ameachiwa kwa kushinda kesi na ameachiwa huru na serikali ya jimbo imesema itamfidia dollar Milioni 3 kama kifuta machozi.

Mzee anasema jamaa zake na karibu ndugu zake wote walishakufa. Anasema amekuta Dunia imebadilika sana, anaona vitu vya ajabu lakini anakubali kuwa alitegemea kukuta Dunia iko tofauti na alivyoiacha.

Kukaa jela miaka 70 sio mchezo.

Marekani kuna vituko, kuna yule askari polisi ana miaka 94 na anasema hana mpango wa kustaafu na gari la patrol anaendesha mwenyewe, karibu wakazi wote wa mtaa wake hadi vitukuu anavijua.

 
Life style la huko linawabeba sana, mtu anakula karibia Uvinza yote ila bado ana nguvu za kutosha.

Kwetu huku ni majanga, mzee wa miaka 60 utadhani ana miaka 100
 
Miongo saba ni mingi sana aliingia jela kukiwa hamna TV za rangi sahivi kuna Flat screens na simu za kugusa vioo.
 
Hapo ndiyo utajua wanawake watakavyoanza kujisogeza sababu ya pesa
 
Back
Top Bottom