Taarifa ya kusikitisha: Binti akiri kuwa alisingizia kubakwa na kupelekea mbakaji kufungwa jela miaka 60

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,207
4,703
Ni habari za huzuni na majonzi

Kumbe sio kila aliye jela ametenda makosa

Kumbe mahakama zinaweza muhukumu hata asiye na hatia

Binti akiri kutoa ushahidi wa uongo mahakamani kuwa amebakwa na aliyemsingizia kufungwa jela miaka 60

Taarifa kamili kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi

=====

Amezongwa na majuto akikumbuka kile alichokifanya miaka mitatu iliyopita.

Maria Sanga (20), mkazi wa kijiji cha Kilingi Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, ameamua kuiangukia Serikali kutengua hukumu kwa kijana aliyemsingizia kuwa alimbaka na kumpa ujauzito mwaka 2017.

Kijana huyo alikuwa kidato cha nne huku yeye akiwa kidato cha pili, na baada ya kesi kusikilizwa mwaka 2018 katika kesi namba moja ya mwaka 2017, Tumaini Frank hatimaye alikutwa na hatia ya kumpa ujauzito Maria na kisha kufungwa gerezani miaka 60.

Asimulia ilivyokuwa

Akielezea mkasa wa tukio hilo jana mbele ya wanahabari, binti huyo alisema kuwa mwaka 2017 wakati akiwa kidato cha pili, alirudi nyumbani baada ya kumaliza mitihani, wazazi wake wakamshuku kuwa na ujauzito.

“Mwaka 2017 nilipata ujauzito nikiwa kidato cha pili, mara baada ya kumaliza mitihani yangu, nilirudi nyumbani baada ya kukaa nyumbani wazazi wangu waligundua ni mjamzito. Waliniuliza ujauzito ni wa nani sikuwaambia, wenyewe wakafanya upelelezi wao wakaniambia Tumaini ndiye aliyekupa ujauzito, wakanitishia kunipiga ikabidi niseme.’’ anaeleza.

“Baada ya kukiri waliyotaka niseme Tumaini alikamatwa na kupelekwa polisi, baadaye niliitwa polisi kwenda kutoa maelezo. Niliandika maelezo yangu na kurudi nyumbani na baadaye kesi ilipelekwa mahakama ya wilaya ya Siha na baadaye nikawa nahudhuria mahakamani ndani ya mwaka mmoja,”alieleza binti huyo.

“Nakumbuka mwaka 2018 Agosti Tumain alihukumiwa kwenda jela miaka 60. Kwa kweli niliumia sana licha ya kwamba nilikuwa naujua ukweli kwamba sio yeye anahusika na mimba yangu. Nafsi yangu iliendelea kunishtaki ikanilazimu niende ofisi mbalimbali kusema sio yeye aliyenipa ujauzito,”

“Nilienda ofisi ya kijiji ofisi ya wanasheria Sanya Juu, walinipokea na kuniandika maelezo yangu kuhusu kukataa kwamba hukumu ile hakustahili Tumaini kutokana na kwamba sio yeye alihusika na ujauzito wangu.’’

Anaendelea; “Nimeona niliseme hili kwa kuwa linaniumiza na huyu anateseka kwa kifungo ambacho sio chake. Ninaziomba mamlaka zinazohusika zinisaidie kwa sababu nililazimishwa na wazazi wangu kumtaja ambaye hahusiki na kipindi hicho bado nilikuwa sina akili za utu uzima.

Kauli ya baba wa aliyehukumiwa

Baba wa Tumaini, Frank Mfinanga alieleza kuwa tukio hilo lilimuumiza na alilipokea kwa machungu kutokana na mwanawe kuhukumiwa kwa kusingiziwa.

“Niliumia sana mtoto wangu alipobambikiziwa kesi ya kumpa mimba mwanafunzi mwenzake. Huyu binti ni wa jirani yangu kabisa, kweli hili suala nilipokea kwa machungu na liliniumiza sana baada ya kesi kwenda mahakamani”

“Baada ya kesi kwenda mahakamani tulipambana na ilipofika Agosti 27 mwaka 2018 ilitoka hukumu kuwa mwanangu anatakiwa atumikie kifungo cha miaka 60 jela, hii hali iliniathiri mimi kama mzazi ambapo mimi ni baba mjane, hawa watoto mke wangu aliniachia wakiwa wadogo na nimeteseka nao sana mpaka huyu Tumain alipofika kidato cha nne,” anasema.

Anaendelea; “Kwa kweli niliumia sana maana ni mwanangu wa pili katika uzao wangu wa watoto sita, nilipambana na hii kesi kwa muda mrefu mpaka ilipotoka hukumu ya kifungo cha miaka 60 gerezani.’’

“Nilikuwa sina hili wala lile kama mkulima niliomba msaada kwa ndugu jamaa na marafiki kwa ajili ya kukata rufaa ndipo nilipokata rufaa ikaenda Mahakama Kuu kanda ya Moshi ambapo baadaye alionekana anapasa kuendelea na kifungo ambapo alipunguziwa miaka 30. Kwa kuwa mwanangu hakutenda hili kosa niliendelea kumsaidia kukata rufaa nyingine zaidi , lakini kilichonikwamisha mpaka sasa nimekosa nguvu ya kuendelea kumsaidia ili haki ya mwanangu ipatikane,”alieleza mzee Mfinanga

“Kilio changu kwa Rais John Pombe Magufuli ambaye ni Rais wa wanyonge anionee huruma na anisaidie katika hili ili haki ya mwanangu ipatikane , huyu binti aliyefanya kosa amekuwa akija nyumbani kwangu na kuniomba msamaha kwa kile alichotenda dhidi ya mwanangu kwa vile amekiri mwenyewe naomba Rais wangu mtetezi wangu anisaidie,”alisema baba huyo.

Alipoulizwa sababu kwa nini hawakupima vinasaba (DNA) ili kubaini kama mtoto huyo ni wa mwanawe, baba huyo alisema;

“Hatukupima DNA kwa sababu ukweli aliujua binti ila ukweli ni kwamba hakimu aliyekuwa akisiliza kesi mara ya kwanza alihamishwa hivyo mpango wa kupima DNA ulifia hapo maana aliletwa hakimu mwingine ambaye ndiye aliyetoa hukumu.”

Alichokisema wakili

Elizabeth Minde ambaye ni mwanasheria Mkoa wa Kilimanjaro, alisema endapo kijana huyo atafanikiwa kuachiwa baada ya kukata rufaa, anaweza akamsamehe au akafanya maamuzi mengine kwa kumpotezea muda.

“Ni uamuzi wa mtu aliyeathirika kuchukua hatua, inategemea na uhusiano ndani ya jamii maana kuna leo na kesho maana mpaka asingiziwe kulikuwa na nini hapo?,”alihoji mama Minde
 
Nilimsikia judge mmoja mstaafu akitabanaisha kuwa, kwenye tasnia ya sheria ni bora hakimu/judge awaachie waharifu 100 wenye makosa na hatia kabisa kulikoni kumuhukumu Mtu mmoja asie na kosa au hatia kwa ushahidi wa kubumba

Sheria bhana huwa inainama kwenye pesa sasa hakimu anadaiwa na bodi unategemea nini?

Watumishi wa umma ilitakiwa bodi ya mikopo isiwakate ndio inatutia umaskini na kushawishi mirungula kwa mahakimu wetu!!!!
 
Tutajuaje kama sasa hivi ndio anadanganya?

Medical reports, chief government chemist reports, cross examinations, other material evidence and witnesses, exhibits na court findings zote hizo zilidanganya?

Hebu wacheni ujinga!

By the way hii ni stori ya kweli au hekaya za vijiweni tu zenye malengo ya kutafuta huruma dhidi ya WABAKAJI na WANAJISI?
 
Tutajuaje kama sasa hivi ndio anadanganya?

Medical reports, chief government chemist reports, cross examinations, other material evidence, exhibits na court findings zote hizo zilidanganya?

Hebu wacheni ujinga!

By the way hii ni stori ya kweli au hekaya za vijiweni tu zenye malengo ya kutafuta huruma dhidi ya WABAKAJI na WANAJISI?
Kesi kama hizo mbona zipo nyingi tu.

Kuna moja nimeshakutana nayo.

Binti aliyesemekana kabakwa alipelekwa hospital mbili tofauti na kufanyiwa vipimo mara mbili.

Siku inayosemekana kubakwa alipelekwa Hospitali A akafanyiwa vipimo.

Siku ya pili yake akapelekwa Hospitali B huko tena akafanyiwa vipimo.

Vipimo vilivyotumika ni vya hispitali B, siku ya pili ya tukio.

Vipimo vya siku ya tukio havikutumika, wala daktari aliyemfanyia vipimo hakutoa ushahidi, aliyetoa ushahidi ni wa Hospital B.

Majibu yenyewe yanasema binti alikutwa na vitu vyeupe kama manii.

Hakuna uthibitisho kwamba hivyo vitu vyeupe ni manii na ni vya mtuhumiwa.

Mtuhumiwa alitakiwa kupelekwa kwa mkemia mkuu hakupelekwa.

Majina aliyotajwa mahakamani sio yake na bado akafungwa maisha.

Ila kuna watu waliisimamia ile kesi jamaa akatoka.

Huko mtaani kuna watu wanafungwa bila makosa.
 
Hiyo labda kama ingekuwa alisingiziwa kuua, ukimuua mtu huyo hamna kesi
A defence to a prosecution for a crime, raising the claim that the accused is being placed on trial for a second time for the same offence. The so-called double jeopardy rule stated that no person may be twice put in jeopardy of life or limb for the same offence.

Following the entry into force of the Criminal Justice Act 2003 the double jeopardy rule was altered (s 75). The new measures only apply to serious offences (i.e. those carrying a maximum sentance of life imprisonment and for which the consequences for victims or society as a whole are particularly serious) such as murder, manslaughter, and rape.

 
Kesi kama hizo mbona zipo nyingi tu,

Kuna moja nimeshakutana nayo.

Binti aliyesemekana kabakwa alipelekwa hospital mbili tofauti na kufanyiwa vipimo mara mbili.

Siku inayosemekana kubakwa alipelekwa Hospitali A akafanyiwa vipimo.

Siku ya pili yake akapelekwa Hospitali B huko tena akafanyiwa vipimo.

Vipimo vilivyotumika ni vya hispitali B, siku ya pili ya tukio.

Vipimo vya siku ya tukio havikutumika, wala daktari aliyemfanyia vipimo hakutoa ushahidi, aliyetoa ushahidi ni wa Hospital B.

Majibu yenyewe yanasema binti alikutwa na vitu vyeupe kama manii.

Hakuna uthibitisho kwamba hivyo vitu vyeupe ni manii na ni vya mtuhumiwa.

Mtuhumiwa alitakiwa kupelekwa kwa mkemia mkuu hakupelekwa.

Majina aliyotajwa mahakamani sio yake na bado akafungwa maisha.

Ila kuna watu waliisimamia ile kesi jamaa akatoka.

Huko mtaani kuna watu wanafungwa bila makosa.
Mhhhhhhhhhhhhhh!!!!

Basi huo ni uzembe wa mahakama pamoja na mawakili wa pande zote!

Ripoti ya daktari inapaswa kuwa assertive and authoritative! Short of that, it must be disregarded and expunged off records.

Ripoti ya government chemist ilikuwa ni ya muhimu hapa ku supplement ripoti ya daktari! Unless kama kulikuwa kuna corroborative evidence nje ya hizi ripoti za kitabibu.

Ushahidi wa binti ulipewa uzito usiostahili — uzembe wa mawakilii.
 
Hizo reports zote zinaonesha mtu kaingiliwa hazioneshi mtu Kabakwa,

uthibitisho wa kubakwa ni mfanywaji kuileza mahakama kuwa aliingiliwa bila ya ridhaa au aliingiliwa aliwa below 18

Reports za kitaalam zinaonesha mtu kaingiliwa hazioneshi kaingiliwa na nani!

Kesi za ubakaji wengi wanaotiwa hatiani huwa hawana Mawakili wajuzi wa kesi hizi za Jinai, ukimpata Mtaalam wa Sheria za jinai anakuchomoa mapema kabisa

Jf sio jalala la kujimwambafai, punguza mbwembwe
Tutajuaje kama sasa hivi ndio anadanganya?

Medical reports, chief government chemist reports, cross examinations, other material evidence and witnesses, exhibits na court findings zote hizo zilidanganya?

Hebu wacheni ujinga!

By the way hii ni stori ya kweli au hekaya za vijiweni tu zenye malengo ya kutafuta huruma dhidi ya WABAKAJI na WANAJISI?
 
Kumpa mwanafunzi mimba unafungwa miaka 60. Je, aliyeua atafungwa miaka mingapi?

Afrika, tunapoteza nguvu kazi kwa sheria zisizo na kichwa wala mikia kwa kufikiri wanawakomoa wanaume. Miaka 60, unafunga mtu? Bongo bahati mbaya
 
Back
Top Bottom