Marekani: Afisa wa polisi asimamisha gari la polisi kwa kuzidisha mwendo

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,800
Huko Florida nchini Marekani afisa mmoja wa polisi amezua gumzo baada ya kusambaa kwa video yake inayomuonesha akimsimamisha afisa mwingine wa polisi kwa kuendesha gari kwa spidi kali.

Mazungumzo kati yao yalikuwa hivi:

"Nini?" aliuliza afisa huyo baada ya kushuka kutoka kwenye gari la polisi. "Ninakwenda kazini, rafiki yangu. Kwanini unajaribu kunisimamisha?"

"Kwa sababu unaenda kwa spidi 80 kwenye eneo lenye kikomo cha spidi 45," alijibu afisa aliyemsimamisha.

Hata hivyo wakati alipoulizwa kuhusu leseni yake ya dereva, afisa huyo alikataa kisha akarudi ndani ya gari la polisi na kuondoka eneo la tukio.

Taarifa za polisi zinasema afisa huyo aliyezidisha mwendo amesimamishwa kazi wakati uchunguzi ukiendelea.

Je, unadhani kuna wakati maafisa wa Tanzania wataweza kufanya hivi?

 
Huko Florida nchini Marekani afisa mmoja wa polisi amezua gumzo baada ya video yake ambayo anaonekana akimsimamisha afisa mwingine wa polisi kwa kuendesha gari kwa spidi kali.
Tanzania ipi? Hi ambao hata mgambo anawezo wa kupiga raia bila kuhojia.
 
Nchi za wenzetu wametuzidi kila kitu.hata rais wa huko hana kinga ya kutokushitakiwa.ajabu kwa tanzania rais ana kinga ili asishitakiwe ili asiwajibishwe kwenye uchafu wao kama huu wa dp world
 
Police wa Sweden pia walishawahi kumsimamisha na kumpiga fine mfalme wao kwa kuendesha speed.
 
Back
Top Bottom